Waliopeperusha bendera ya ’Yaa Hussein’ wafungwa Saudia
Vijana watano nchini Saudi Arabia wamehukumiwa adhabu ya
kifungo cha miaka 21 na miezi 6 jela kila mmoja kwa kosa eti la
kupeperusha bendera iliyoandikwa ‘Yaa Hussein’ nchini humo.
Ahmad ar Rabbah mwanaharakati na mkuu wa Taasisi ya Kutetea
Haki za Binadamu nchini Saudi Arabia amelaani vikali adhabu hiyo dhidi
ya vijana hao Waislamu wa Madhehebu ya Shia na kusisitiza kuwa, kitendo
hicho kinakiuka misingi ya haki za binadamu. Rabbah amesisitiza kuwa,
adhabu hiyo haina mfungamano wowote na sheria za ndani ya nchi hiyo wala
za kimataifa, bali inaonyesha chuki za wazi na ubaguzi wa kimadhehebu
unaofanywa na utawala wa kifalme wa Aal Saud dhidi ya Waislamu wa
madhehebu ya Shia. utawala wa Saudi Arabia mara kwa mara umekuwa ukitoa
adhabu ya vifo au vifungo vya muda mrefu dhidi ya maulamaa, waandamanaji
na wafuasi wa madhehebu ya Ahlul Bayt AS nchini humo.
Imam Hussein bin Ali bin Abi Talib AS, ni mjukuu wa Mtume Mtukufu Muhammad SAW.
Maoni
Chapisha Maoni