Makamu wa Rais Zimbabwe atimuliwa ndani ya chama
Makamu wa Rais wa Zimbabwe Joice Mujuru ambaye anatuhumiwa
kupanga njama ya kumpindua Rais Robert Mugabe leo amevuliwa ustahiki wa
kuwania uanachama katika kamati kuu ya chama tawala ZANU-PF.
Nyaraka alizowasilisha Mujuru kwa ajili ya kuwania uanachama katika kamati hiyo muhimu zimekatiliwa na kamati ya utendaji. Hatua hiyo inakuja kabla ya kongamano la kitaifa la ZANU-PF ambalo limepangwa kufanyika wiki ijayo.
Katika siku za hivi karibuni magazeti yaliyo karibu na Rais Mugabe yamekuwa yakimtuhumu Mujuru kuwa anapanga njama za kumuondoa Mugabe madarakani. Hivi sasa kuna mvutano mkubwa katika chama tawala kuhusu ni nani atakayechukua nafasi ya Mugabe mwenye umri wa miaka 90 endapo atajiuzulu au afariki dunia.
Novemba 17 Mujuru alijitetea na kusema hajahusika na njama zozote za kutaka kumuua Rais Mugabe. Imedokezwa kuwa Mujuru na Waziri wa Sheria Emmerson Mnangagwa, ndio wanasiasa waandamizi wanaowania kuchukua nafasi ya Mugabe ambaye ameitawala Zimbabwe tokea mwaka 1980.-irn

Maoni
Chapisha Maoni