Mama atelekeza watoto wake
JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke
linamshikilia mkazi wa Mbagala Kwa Azizi Ally, Mariam Issa, kwa kosa la
kutelekeza watoto wake watatu katika kituo cha
Masista Kurasini, kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki mjini Dar es Salam.
Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Temeke, Sabastian Zacharia, alisema mtuhumiwa alikamatwa juzi
katika eneo la Kwa Azizi Ally, katika nyumba aliyokuwa akiishi.
Alisema taarifa za awali zilizofikishwa kituoni hapo
na Masista wa kituo hicho, zilieleza kuwa mama huyo alifika katika kituo
hicho akiwa na wawoto wake kwa lengo la
kuomba msaada ili aweze kusaidiwa kulelewa.
Alisema mtuhumiwa huyo aliondoka kimyakimya na kuwaacha
watoto watatu, akiwamo wa kike mmoja na kutokomea kusikojulikana.
“Watoto hawa
ni wadogo, mkubwa ana umri wa miaka mitatu na nusu, wa pili ana miaka miwili na
nusu na wa mwisho ana mwaka mmoja na nusu.
“Watoto hao baada ya kutelekezwa na mama yao masista
wa kituo hicho waliripoti katika kituo chetu cha Polisi hapa Chang’ombe na
tuliwapeleka Ustawi wa Jamii huku tukiendelea na msako mkali wa kumtafuta
mtuhumiwa.
“Tulimkamata mtuhumiwa jana akiwa katika harakati ya
kuhamisha vitu vyake vilivyokuwepo katika chumba alichokuwa akiishi na
kumfikisha kituoni,” alisema Zacharia.
Alisema uchunguzi wa awali, ulibaini Mariamu
alikuwa akidaiwa kodi katika nyumba aliyokuwa akiishi na mzazi mwenzake
ambaye alimkimbia akiwa na ujauzito-Mtanzania
Maoni
Chapisha Maoni