Wafanyakazi waidai Muhimbili Sh mil 121
HOSPITALI
ya Taifa Muhimbili inadaiwa zaidi ya Sh milioni 121.5 ambazo ni malimbikizo ya
fedha za likizo za wafanyakazi ambao ni wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa
Serikali Kuu na Afya (TUGHE).
Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Aminieli
Eligaesha, amesema uongozi wa hospitali hiyo umeanza kupunguza deni hilo tangu
Juni, mwaka huu.
“Tumeanza
Juni, mwaka huu kupunguza deni hilo ambalo lilitokana na hospitali kutokuwa na
fedha za kutosha za kuwalipa, ndiyo maana tumeshindwa kuwalipa kwa wakati,”
Eligaesha.
Amesema
awali deni hilo lilikuwa kubwa ikilinganishwa na kipindi hiki, lakini uongozi
ulifanikiwa kulipunguza.
Eligaesha
amesema kutokana na hali hiyo, wafanyakazi wote wanaoendelea kuomba likizo
hawataweza kulipwa fedha zao hadi deni hilo litakapomalizika.
“Kwa
wafanyakazi ambao wataomba likizo hawatalipwa fedha zao hadi deni la
wafanyakazi wanaodai litakapolipwa,” amesema Eligaesha.
Kutokana
na hali hiyo, amewasihi wafanyakazi kuwa wavumilivu wakati huu.
Wafanyakazi
hao wanadai fedha zao za likizo mwaka
mmoja sasa, jambo ambalo limewaweka katika mazingira magumu katika utendaji.
Maoni
Chapisha Maoni