Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2014

Mume mgomvi aandaliwa mlo wa kondomu

Picha
Mwanamke mmoja mwenye watoto watatu katika wilaya ya Kole nchini Uganda alimuandalia mumewe mlo wa mipira ya kondomu kufuatia ugomvi usiokwisha kati yao. Mwanamke huyo ambaye ni mkaazi wa eneo la Arao aliripotiwa kununua paketi tatu za kondomu aina ya "Trust" kutoka duka jirani kabla ya kuzipika na kumuandalia mumewe kama chakula baada ya kurudi nyumbani akiwa amelewa chakari. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda, mwanamke huyo aliikata kata mipira hiyo ya kondomu ambayo ilikuwa haijatumika katika vipande vidogo vidogo na kuvichemsha kwa muda kabla ya kuvikaanga kwa mafuta ya kupikia na viungo vingine. Wakati mumewe alipowasili kutoka kubugia pombe katika eneo jirani la kibiashara la Odede,aliandaliwa mlo huo katika sahani tofauti moja ikiwa na mipira hiyo kama mboga na nyingine ikiwa na mkaa. Lakini jamaa huyo alibaini njama za mkewe baada ya kuonja mlo huo na kugundua ulikuwa na ladha tofauti. Hatua hiyo ilikuwa ikilenga kumfunza mume hu

Najivunia kuwa shoga mkuu wa Apple

Picha
Mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook   Mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook ametangaza jinsia yake akisema kuwa ''anajivunia kuwa shoga''. . Bwana Cook alitoa tamko hilo ili kujaribu kuwasaidia watu wanaong'ang'ana kutangaza jinsia zao katika ripoti iliochapishwa katika gazeti la biashara la kila wiki la Bloomberg. Amekuwa wazi kuhusu jinsia yake,lakini pia amejaribu kuweka maisha yake katika faragha hadi sasa alisema.   Wiki hii Bwana Cook alitoa changamoto kwa jimbo lake la Alabama kuhakikisha kuwa haki za mashoga na wale wanaobadili jinsia zinaheshimiwa. ''Mimi sijitambui kama mwanaharakati,lakini nimegundua nilivyofaidika na mikakati iliowekwa na wengine'',alisema bwana Cook. ''Kwa hivyo iwapo watu wakisikia kwamba mimi ni shoga kutawasaidia baadhi yao ,ama kumpa faraja yule anayejisikia mpweke ama kuwashinikiza wengine kupigania haki zao,basi afadhali kutangaza maisha yangu ya faragha''aliongezea. Bwana Cook amese

Bunge la Burkina Faso lachomwa

Picha
  Rais Blaise Campaore Waandamanaji nchini Bukina Faso wameteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, kupinga hatua ya kuongeza muhula wa Rais Blaise Compaore ambaye ametawala nchi kwa miaka 27. Runinga ya itaifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika la utangazaji. Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi. Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto. Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa. Rais Blaise Compaore ameomba utulivu ,katika ujume aliotumwa kwa Twitte   Burkina Faso Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore kuwania tena Urais mwaka ujao. Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa Blaise Compaore. Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge. Compaor

Man jailed for four years for cutting son’s ear

Picha
James Sishia Wanda who was jailed for four years for cutting his son's ear. A man has been jailed for four years for cutting his son’s ear and forcing him to drink blood from the wound. James Sishia Wanda is said to have cut his six-year-old son’s right ear claiming he had stolen his money, drew blood from the wound and forced the boy to drink it. He was found guilty of grievous harm and subjecting the boy to cruel treatment by Nairobi Senior Resident Magistrate Lucy Mbugua. He committed the offence on June 29, 2014 at Mathare 4B area in Nairobi County. In mitigation, the accused pleaded for leniency saying he has six children who depend on him. But State Counsel Dancun Ondimu urged the magistrate to hand the accused a custodial sentence as cases of child abuse were on the rise.

Ballon d'Or:Bale na Ronaldo waorodheshwa

Picha
  Ronaldo na Bale Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale ndio mchezaji wa kipekee wa Uingereza kuorodheshwa kati wachezaji wanaoshindania tuzo la mchezaji bora zaidi duniani Ballon d’Or huku mshambulizi matata wa Real Madrid Christiano Ronaldo akitarajiwa kuhifadhi taji hilo Bale, mwenye umri wa miaka 25, aliweza kuifungia Real Madrid mabao 22 msimu uliopita na kuwezesha Real Madrid kunyakua kombe la kilabu bingwa duniani Lionel Messi ambaye ameshinda taji hilo mara tatu pia yuko miongoni mwa orodha hiyo akiwa na mwenzake Neymar Orodha hiyo ya wachezaji 23 itapunguzwa hadi watatu ambapo mshindi atatangazwa mnamo Januari 12, 2015 huko mjini Zurich . Hatahivyo hakuna nafasi ya mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kuisadia timu yake ya nyumbani Uruguay kufika katika robo fainali ya michuano ya kombe la dunia nchini Brazil,lakini akasimamishwa kwa mda kushiriki katika soka yoyote kwa miezi mine kwa kumng’ata mlinzi wa I

Msichana asimulia ya Boko Haram

Picha
Baadhi ya wasichana waliotekwa nyara Ni miezi sita sasa baada ya wanamgambo wa kiislam wa kundi la Boko Haram kuwateka wanafunzi wasichana Zaidi ya 200 kaskazini mashariki mwa Nigeria, wasichana watatu ambao wametoroka wamezungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa ya BBC. Tukio hili linakuja wakati serikali ya Nigeria ikiwa katika makubaliano ya kusimamisha mapigano dhidi ya Boko Haram hatua itakayo saidia kuwaachilia huru wasichana waliotekwa na kundi hilo . '' nilikuwa nataka kurukia nje wakati msichana mwenzangu aliponikamata kwa nyuma na kusema watakupiga risasi kama utafanya hivyo. Nikasema, nini utofauti wataniua mimi hapa na kuacha maiti yangu ikusachukuliwa nilikuwa nalia na kuomba mpaka tulipoifikia kambini" Anasimulia msichana mmoja alitoroka mikononi mwa Boko Haram Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa ya BBC, Msichana huyu anakumbuka jinsi alivyokuwa nyuma ya Lori wakati wanapinaji wa Boko Har

Angalia video ya akina mama wakisukwa nywele gerezani

Picha

Raila Odinga alivyotandikwa bakora

Picha

Kesi ya Ngassa yapigwa kalenda

Picha
Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Dar es salaam imeipiga kalenda kwa siku 35 kusikiliza kesi ya talaka ya madai namba 30/2014 inayomkabili mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa. Mrisho Ngassa GAZETI la Bingwa Alhamisi, Oktoba 23,limeripoti.

Mvua yakatisha masomo kwa wanafunzi

Picha
Mbeya   MTANZANIA limeandika Wanafunzi 320 katika kijiji cha Maendeleo ,kata ya Ruiwa,wilayani Mbarali,wamelazimika kukatiza masomo kwa zaidi ya wiki mmoja kutokana na mvua ambayo imewatenganisha na shule yao. Taarifa zaidi zinasema kuwa wanafunzi hao ambao ni wadarasa la kwanza hadi la sita,wanalazimika kufundishwa na mwalimu mmoja ,Laiton Ngoli,katika kituo cha masomo ya awli ,ambapo pia hata hivyo hana taaluma hiyo. Ripoti kamili iko kwenye Gazeti la MTANZANIA Alhamisi Oktoba 23.

Mchina mbaloni kwa ujambazi

Picha
Jeshi la polisi mkoa wa pwani linawashikilia watu watano akiwemo raia mmoja wa china ,Wu Shengbin wakituhumiwa kufanya ujambazi katika maeneo ya Mkuranga na Bagamoyo mkoani Pwani. Gazeti la MTANZANIA, alhamisi Oktoba 23, linalipoti limeripoti.

Ugali wa mhogo waua bukoba

Picha
Gazeti la MTANZANIA leo alhamisi Oktoba 23, limeripoti kuwa watuwawili wamefariki dunia katika kijiji cha milanda ,Tarafa ya Nshamba ,Wilaya ya Muleba mkoani Kagerabaadaya kula ugali wa mhogo unaosadikiwa kuwa na sumu.-

Vodacom yaja na teknolojia ya password ya sauti.

Picha
Kampuni ya simu za mkononi ya VodaCom imezindua ya teknolojia mpya ya kurekodi sauti kutunza namba ya siri badala ya ile ya maandishi iliyozoeleka. Huduma hiyo ambayoimeanza kutumika rasmi nchini afrika kusini ni asalama zaidi kwa utunzaji wa namba za siri katika simu ikilinga nishwa na ya maandishi ambayo hutumiwa na watu wengi. Mtendaji mkuu wa huduma kwa wateja afrika kusini wa kampuni hiyo Dee Nel amesema dar es salaam leo kuwa mteja wa vodacom anetumia teknollojia hiyo anauwezo wa kuituinza namba yake ya siri bila mtu mwingine kuitambua. "ili kujiunga na huduma hii mteja anatakiwa kurekodi nambaya siri inayotamkwa na sauti yakekwenye my vodacom App au kwa kupiga simu katika kituo cha huduma kwa wateja namba ya simu 111/082111,pindi mteja akisajili password yake kwa sauti yake basi ndiyo itakuwa inatumika siku zote anapotaka kufanya mhamala wowote na mtu yeyeote akitaka kuiga sauti ya mhusika itakuwa viogumu kutambulika kufanya mhamala wowote"amesema Nel. teknolo

'Busu' lamtia mashakani Obama

Picha
Rais wa Marekani, Barack Obama, ametoa kauli yake kuhusu mwanamume aliyeshikwa na wivu baada ya yeye kumbusu mpenzi wake kwenye mashavu. "rais tafadhali usimguse mpenzi wangu," alisema mwanamume, aliyetambuliwa na CNN kama Mike Jones. Yote hayo yalitokea wakati Obama alipokuwa anapiga kura ya mapema katika jimbo la Illinois karibu na mwanamke aliyetajwa tu kama Aia Cooper. ''Kusema kweli sikuwa nimepanga kufanya hivyo,'' alisema Rais Obama , huku akiendelea kupiga kura yake huku Copper akiangua kicheko. Baadaye Copper aliyeonekana kushikwa na aibu aliomba radhi kwa niaba ya mpenzi wake. Obama alionekana naye kashikwa na aibu na kusema kwa tabasamu kuwa ,''hiki ni kisa tu cha mwanamume ndugu yangu kutaka tu kuniabisha bila sababu,'' Baada ya maongezi ya muda mfupi kati ya Obama na Cooper, wawili hao walimaliza kupiga kura, na kamera ikaonyesha Obama akimbusu Cooper mashavuni na kumpa mpenzi wa Coopper sababu nyingine ya kuonge

Mufti:''Twitter ni chanzo cha maovu''

Picha
  Mufti Sheikh Abdul Aziz al-Sheikh anasema Twitter imejaa taarifa za uongo na zisizo na msingi Mtandao wa kijamii wa Twitter unaosifika sana miongoni mwa wanawake na wanaume nchini Saui Arabia, umesemekana kuwa chanzo cha maasi na uovu. Hii ni kauli ya mufti mkuu wa Sadi Arabia katika taarifa kwenye mtandao wa 'Al Arabiya news'. ''Ikiwa mtandao huo ungetumiwa kwa njia inayostahili , ungekuwa na manufaa makubwa kwa jamii, lakini badala yake mtandao huo unatumika kwa mambo ya kipuuzi.''   Twitter hutumiwa na watu wengi kupashana habari kote duniani Alisema sheikh Abdul Aziz al-Sheikh katika kipidni chake cha televisheni kiitwacho Fatwa siku ya Jumatatu. ''Twitter ni chanzo cha maovu na uharibifu,'' alisema Mufti huyo. ''Watu wanakimbilia mtandao huo wakidhani ni sehemu ya kupata taarifa za uhakika wakati mtandao huo umejaa uongo na porojo tupu,'' aliongeza kusema Mufti huyo. Saudi Arabia hutu

BEHIND OF MY EYES (NYUMA YA MACHO YANGU) SEHEMU YA NNE.

Picha
TITLE :BEHIND OF MY EYES (NYUMA YA MACHO YANGU) MWANDISHI JOHN JACKSON SEHEMU YA NNE.   BAADA YA WIKI 2 KUPITA Meshaki analudi na Joyce walikwenda kupokelewa na ndugu zake na baadye kuanza maisha Joyce alikua hajakamilisha shughuliza zake za uamisho hivyo alikuwa anafanya kazi za umama nyumbani akisaidiana na mama Mkwe wake,Wakati akisubilia mambo yake yakamilike aanze kazi. Siku moja Mama Meshaki akiwa jikoni, Oscar aliingia na kumshika kiunoni na shughuli za upishi zilikwama maana walianza kupeana mapenzi jikoni. Kwa kelele za vyombo kuanguka anguka ovyo vilimfanya Joyce kuamka usingizini na kwenda kutazama nini kinachoendelea. Joyce alipokaribia maeneo ya jikoni alipishana na Oscar akionekana kuufunga mkanda wa suluali yake, alishangaa na lipoingia jikoni alimkuta Mama Meshaki akiahangaika kujifunga khanga  vizuri. Joyce kwa hali hiyo ilihisi kutakuwa na jambo linaendelea na Mama Meshaki alipoulizwa na Joyce  kama kuna tatizo? Mama Meshaki alicheka k

Video ya mchezaji wa India aliyepoteza maisha uwanjani

Picha

Mchezaji afariki akisherehekea bao

Picha
  Ligi ya Mizoram ikimuombolea mchezaji Peter Biaksangzuala Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake. Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kw atimu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC. Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki. Mechi hiyo ambapo alipata jerehe la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo. Taarifa kutoka kwa ligi hiyo kpitia kwa mtandao wa Facebook, ilisema : ''imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa soka na mashabiki wa Mizoram. '' "Peter alikuwa mchezaji mzuri na milizni mzuri sana, na pia alikuwa mchapa kazi.''-bbc swahili  

Boko Haram waendelea na mashambulizi

Picha
Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram, wamewapiga risasi na kuwachinja watu katika vijiji vitatu Kaskazini Mashariki ya Nigeria licha ya serikali kudai mwishoni mwa wiki kuwa ilifikia makubaliano na kundi hilo. Wapiganaji wa Boko Haram, walivamia vijiji viwili Jumamosi na kupandisha bendera yao kwa mara ya tatu. Hii ni kwa mujibu wa wanakijiji wa eneo hilo. Serikali ilisema kuwa itaendelea kufanya mazungumzo na Boko Haram licha ya madai ya kundi hilo kuvunja makubaliano. Inatumai kuwa kundi hilo litawaachilia zaidi ya wasichana miambili waliowateka nyara amwezi Aprili. Boko Haram hawajasema chochote kuhusu tamko la serikali ya Nigeria Ijumaa kwamba wamekubali kusitisha vita na kuwaachilia wanafunzi hao miambaili waliotekwa nyara katika eneo la Chibok. 'ahadi yatimizwa' Wasichana wa Chibok waliotekwa nyara na Boko Haram mwezi Aprili mwaka huu Inaarifiwa Boko Haram wanawakilishwa kwenye mazungumzo ya upatanishi yanayofanyika nchini C

Hadithi BEHIND OF MY EYES (NYUMA YA MACHO YANGU) sehemu ya tatu

Picha
TITLE :BEHIND OF MY EYES (NYUMA YA MACHO YANGU) MWANDISHI JOHN JACKSON SEHEMU YA 3. BAADA YA MIEZI SITA 6 DAR ES SALAAM Meshaki Akiwa Msanifu Majengo Wa Shirika Hilo alipatiwa Nyumba ya Kuishi Maeneo  ya Masaki akiishi  na mama yake  kiujumla maisha yao meshaki na mama yake yalikuwa mazuri sana siku  moja meshaki akiwa ofisini kwake alipokea simu kutoka makao makuu ya shirika ikimtaka awatangazie wafanyakazi wake semina ya siku tano itakayo wakutanisha wafanyakazi wote wa Bara la Afrika na mkutano huo utafanyika Afrika kusini hivyo waanze maandalizi, Muda huo huo meshaki aliitisha mkutano wa dhalula na walitakiwa watu wawili watakao iwakilisha ofisi akiwemo na meshaki , baabda ya mkutano huo meshaki alipanda gari yake na kurudi nyumbani alimkuta mama yake ameketi kwenye sofa  huku akiuvuta sigara na kunywa pombe. Meshaki: alistaajabu na kumuuliza mama yake kulikoni na ameanza lini mambo ya kunywa pombe Mama: “ hapana mwanangu nafanya ili kujiburudish

KWANINI HUFANIKIWI

Picha
Endelea na kupata elimu huru bila malipo hapa baada ya kuangalia hatua mbili wiki iliyopita leo tunaendelea hapa. 3.UTOAJI Tunashidwa kufanikiwa kwasababu bado hatujajua nini maana ya utoaji,katika jambo ambalo linaonekana ni kawaida kwa baadhi ya watu ni kutoa,pasipo kujua katika kutoa kuna kitu ambacho kipo kimejifisha ambacho ndipo mafanikio yetu yalipo,utoaji  wa mazoea kwa sisi watu ndipo tatizo lilipo. Mtu anatoa pasipo kujua anatoa kwa kwa minajili ipi, na katika kutoa kuna utoaji wa aina nyingi ambapo sidhani kama wote tutakuwa tunafahamu, je ?ni pesa pekee ndio utoaji? leo nataka kukupa aina nyingine kabisa za kutoa mbali na hiyo tuliyo izoea. Kutoa muda kwa ajili ya kufanikisha jambo Fulani muhimu,kutoa elimu uliyonayo kwa ajili ya kuisaidia jamii,kutumia vipaji vyetu kama sanaa ya uigizaji,uimbaji,uchoraji na sanaa zingine ambazo zinalenga kubadilisha mtazamo kwa jamii kwa mtazamo chanya,hata kutoa njia ambazo zimekuwezesha wewe kufanikiwa napo pia ni ut

KWANINI HUFANIKIWI,SOMA HAPA

Picha
KWA NINI HATUFANIKIWI? Hili ni swali ambalo baadhi ya watanzania wenzangu hujiuliza kila siku pasipo kupata jibu lililo sahihi hasa baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu pasipo hata kuona dalili za mafanikio na kubaki tukiwangalia wenzetu wakipiga hatua kila siku. Baada ya kuona mafanikio kwa wenzetu sisi hukaa na kuanza kujadili mali za mtu huyo alipozipata,badala ya kukaa na kujiuliza wapi tumekosea na nini tufanye na kwa nini huyu afanikiwe sisi tusifanikiwe wakati wote ni sawa na tumeletwa chini ya jua? Sikatai kwamba si kila mtu aliyefanikiwa katika dunia hii basi amepata mali hizo kihalali,ukweli ni kwamba mafanikio yanaweza kupatikana kwa njia nyingi tofauti mfano wapo ambao huua,wengine kudhurumu,wengine kufanya matukio ya ujambazi,wengine kujiunga na makundi ya kishetani,hapo napo mafanikio huwepo lakini mara nyingi mafaniko yao huwa ni muda mfupi yaani hayadumu. Leo ni meamua kundika makala hii nikitaka kuzungumzia mafanikio ambayo hutokana na bidii na jitihada za mtu mmoja

Hadithi BEHIND OF MY EYES (NYUMA YA MACHO YANGU sehemu ya pili

Picha
TITLE                   :  BEHIND OF MY EYES (NYUMA YA MACHO YANGU)  MWANDISHI  :  JOHN JACKSON   SEHEMU          :  YA PILI Iliwachukua takribani masaa nane na walifanikiwa  kufika nchini Canada majira ya asubuhi huku msimu wa barafu kuanguka ulishika hatamu, wakiwa wamevalia makoti walikuta wenyeji wao wanawasubiria, walichukuliwa na wenyeji wao na kuanza safari ya kuelekea jijini maska, mji ambao upo nje kidogo ya  mjini wa  Canada takribani masaa mawili hadi kufika Maska. Walifika Maska mpaka sehemu ambayo watakuwa wakiishi kila familia ilipewa nyumba ya kuishi. Mama Meshaki na mwanaye , Matha na mdogo wake Joyce maisha ya Canada yalianza. Siku iliyofuata Meshaki na Joyce walipelekwa katika chuo ambacho watakuwa wakisomea na kutambulishwa kwa wanafunzi wenzao na kupewa siku ya kuanza masomo. Joyce yeye alikuwa ni raia wa Kenya hivyo walikutana na wanafunzi ambao ni raia wa Kenya na watanzania kadhaa hivyo walijenga nao urafiki, Meshaki na Joyce walianza

Mwanamke amtoa mwanaume ulimi kisa ngono

Picha
Kijana mmoja mkazi wa Kimandolu jijini Arusha, Paulo Simon (18) amelazwa hospitali ya mkoa Mount Meru, baada ya kubakwa na kisha kukatwa ulimi na mwanamke mmoja aliyekuwa akimtaka kimapenzi. Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia Jumanne majira ya saa 6.30 katika eneo la Tindigani, Kimandolu, wakati mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina moja la mama Abuu alipofika katika baa hiyo kama mteja na baadae kumlazimisha mhudumu wa baa hiyo kufanya mapenzi bila ridhaa yake. Simoni ambaye ni mfanyakazi katika baa hiyo, inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Mtaa, Joel Mbasha, alisema mnamo majira usiku alikuja mwanamke huyo na kuagiza kinywaji na kumuhudumia. Alisema ilipotimu majira ya saa 6.30 wateja waliisha na kuamua kufunga baa, hata hivyo mwanamke huyo alieendelea kunywa pombe taratibu katika eneo la kaunta. “Mimi sikuwa na mazoea kabisa na mwanamke huyo kwanza ukimwangalia ni kama mama yangu,wakati nikifunga baa na kujaribu kuondoka alinifuata na kuniambia an

Ronaldo tishio Facebook

Picha
Mchezaji mahiri wa soka Cristiano Ronaldo amekuwa akichana uwanja kwa kuingiza mabao 18 katika mechi 14 msimu huu. Ronaldo ambaye amewahi kushinda taji la FIFA la mchezaji bora wa mwaka mara mbili, yuko kifua mbele na mabao 13 katika mechi sita za ligi ya Italia. Yeye sio nyota tu uwanjani bali pia kwenye mitandao ya kijamii na Jumanne hii alitajwa kwa mchezaji wa kwanza kufikisha Likes milioni miamoja kwenye Facebook. Mtu mwingine anayeonekana kuenziwa sana kwenye mitandao ya kijamii ni mwanamuziki Shakira. Wanamuziki wengine kama vile Eminem ana Likes milioni Rihanna Likes milioni 90 na ndio wanamuizki ambao labda huenda wakafikisha idadi hiyo ya mashabiki, labda wakiwa na bahati sana. Ronaldo alitengeza video ya kuwashukuru mashabiki wake na kusema ni hatua kubwa sana maishani mwao. "nimefurahi sana nimefikisha mashabiki milioni 100 kwenye Facebook. Ni jambo zuri sana kuweza kufikia maishani mwangu hasa kwa kuwa inaniunganisha na watu kote duniani,''

Ujerumani yabanwa mbavu na Ireland Ulaya

Picha
mambo yalipokuwa mazuri hapo kabla Baada ya kupata matokeo ya kuchefua katika mchezo uliopita, mabingwa wa dunia Ujerumani hali bado si shwari baada ya usiku wa kuamkia leo kuvutwa shati wakiwa nyumbani na Jamhuri ya Ireland katika mchezo wa kufuzu kombe la mataifa Ulaya wakati mchezo huo ulipoisha kwa sare ya bao 1-1. Goli la dakika ya tisini lilitosha kuisaidia Jamhuri ya Ireland kuondoka na point moja kibindoni. Kwingineko mchezaji bora wa dunia na nahodha wa Ureno Cristian Ronaldo huenda akastarehe vema baada ya kuisaidia timu yake ya taifa kuondoka na ushindi wakiwa ugenini kucheza dhidi ya Denmark. Ronaldo alifanikwa kufunga goli pekee katika mchezo huo katika dakika ya tisin na kuiwezesha timu yake kuondoka na point zote tatu. Nayo Scotland ilitoshana nguvu ilipocheza dhidi ya Poland baada ya kutoka sare ya 2-2. Romania iliishushia kipigo Finland kwa kuifunga mabao 2-0. Huku Switzerland ikiigalagaza San Marino kwa jumla ya mabao 4 kwa msh

Kwa wale wapenda hadithi mzigo huu hapa...

Picha
TITLE :BEHIND OF MY EYES (NYUMA YA MACHO YANGU) MWANDISHI JOHN JACKSON SEHEMU YA 1. O scar ,Tegete na Meshaki ni marafiki waliokuwa wakisoma pamoja katika shule ya sekondari Mbuyuni  wilayani Bagamoyo na wote walikuwa kidato cha tatu. Maisha ya nyumbani kwao kwa kina Meshaki yalikuwa mazuri, kwani Baba yake alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa mbao amabapo alikuwa akizisafirisha kutoka Mtwara  na kuzileta Dar es Salaam. wakati  huo Mama yake ambaye hakuonekana na umri mkubwa alikuwa na Maduka ya Vipodozi mjini hapo, Oscar na Tegete wao maisha ya wazazi wao  hayakuwa Mazuri kivile kwani muda mwingine  Familia ya  Meshaki ilikuwa ikiwalipia ada marafiki wa Meshaki. Famila zote zilielewana kutokana na undugu walioujenga vijana hao, Siku moja  Oscar na Tegete walikuwa wakitoka Shule kuelekea majumbani kwao ilikuwa  ni kwaida yao kupitia katika vibanda vya kuuzia Mihogo ili wale kisha ndio  waende nyumbani kwao walikuwa wanakula huku wakizungumza. Oscar = daah washikaj