Ujerumani yabanwa mbavu na Ireland Ulaya
Baada ya kupata matokeo ya kuchefua
katika mchezo uliopita, mabingwa wa dunia Ujerumani hali bado si shwari
baada ya usiku wa kuamkia leo kuvutwa shati wakiwa nyumbani na Jamhuri
ya Ireland katika mchezo wa kufuzu kombe la mataifa Ulaya wakati mchezo
huo ulipoisha kwa sare ya bao 1-1.
Goli la dakika ya tisini lilitosha kuisaidia Jamhuri ya Ireland kuondoka na point moja kibindoni.Kwingineko mchezaji bora wa dunia na nahodha wa Ureno Cristian Ronaldo huenda akastarehe vema baada ya kuisaidia timu yake ya taifa kuondoka na ushindi wakiwa ugenini kucheza dhidi ya Denmark.
Ronaldo alifanikwa kufunga goli pekee katika mchezo huo katika dakika ya tisin na kuiwezesha timu yake kuondoka na point zote tatu.
Nayo Scotland ilitoshana nguvu ilipocheza dhidi ya Poland baada ya kutoka sare ya 2-2. Romania iliishushia kipigo Finland kwa kuifunga mabao 2-0.
Huku Switzerland ikiigalagaza San Marino kwa jumla ya mabao 4 kwa mshituko.
Na Katika hatua nyingine baada ya kuibuka kidedea katika mechi dhidi ya Cyprus, mchezaji ghali kabisa duniani Uingereza Gareth Bale amesema ushindi iliyoupata timu yake ya taifa ya Wales katika mechi za kufuzu mataifa ya Ulaya usiku wa kuamkia jana, inaonesha umoja uliopo ndani ya kikosi hicho.
Winga huyo wa miamba ya soka Ulaya Real Madrid amesema Wales ilipata ushindi japokuwa mchezaji Andy King alitolewa kwa kadi nyekundu katika dakika za mwanzo za-bbc
Maoni
Chapisha Maoni