Kwa wale wapenda hadithi mzigo huu hapa...

TITLE :BEHIND OF MY EYES
(NYUMA YA MACHO YANGU)
MWANDISHI JOHN JACKSON
SEHEMU YA 1.

Oscar ,Tegete na Meshaki ni marafiki waliokuwa wakisoma pamoja katika shule ya sekondari Mbuyuni  wilayani Bagamoyo na wote walikuwa kidato cha tatu.
Maisha ya nyumbani kwao kwa kina Meshaki yalikuwa mazuri, kwani Baba yake alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa mbao amabapo alikuwa akizisafirisha kutoka Mtwara  na kuzileta Dar es Salaam.
wakati  huo Mama yake ambaye hakuonekana na umri mkubwa alikuwa na Maduka ya Vipodozi mjini hapo, Oscar na Tegete wao maisha ya wazazi wao  hayakuwa Mazuri kivile kwani muda mwingine  Familia ya  Meshaki ilikuwa ikiwalipia ada marafiki wa Meshaki.
Famila zote zilielewana kutokana na undugu walioujenga vijana hao, Siku moja  Oscar na Tegete walikuwa wakitoka Shule kuelekea majumbani kwao ilikuwa  ni kwaida yao kupitia katika vibanda vya kuuzia Mihogo ili wale kisha ndio  waende nyumbani kwao walikuwa wanakula huku wakizungumza.
Oscar = daah washikaji mimi nampenda sana Naomi hivi nifanyaje ? wengi walimcheka sana lakini.
Meshaki aliahidi kumsaidia waliondoka sehemu  hiyo na kuanza kurudi  nyumbani. wakiwa barabarani mvua ilianza kunyesha ili bidi wajikinge  ili mvua iishe waanze safari , wakiwa wamesimama kwenye kibanda kimoja cha wakala wa M.pesa .
Oscar anamuona mtoto mdogo aliyekuwa amesimama katikati ya Barabara  akionesha kuzidiwa na mvua huku analia,
Oscar kwa huruma akaona aende kumuokoa mtoto  Yule, Oscar alikwenda kumtoa mtoto Yule barabarani lakini alipokuwa akirudi  huku amembeba mtoto  Yule, ilitokea gari gafla na kumgonga Oscar pamoja na mtoto Yule.
wenzake walitahamaki kuona hali ile  huku na watu wengine waliokuwa maeneo hayo wakiendelea na shughuli zao nao walishangaa.
Tegete  na Meshack wakiwa hawajui wafanya nini walikuwa wakilia tu gari lililofanya tukio liliondoka kwa kasi na  ndipo askari walifika haraka na kuwachukua Oscar pamoja na Yule mtoto  pamoja na mashahidi,
zilikuja gari mbili  moja ilikuwa  gari  ya kubebea wagonjwa  na nyingine ya kawaida iliyowabeba mashahidi  huku damu zikiwa zimetapakaa kwenye ardhi, mvua nayo ikiendelea kunyesha Oscar na Yule mtoto walifikishwa Hospitalini huku.
Oscar akionekana kuumia vibaya sehemu  ya kichwa chake na mtoto Yule akionekana kutokwa na damu nyingi puani na maskioni.

Habari ziliwafikia wazazi wa marafiki hao na kuondoka kwenda kujua nini kilichowapata marafiki hao, walifika Hospitali na kuwakuta Tegete na Meshack wakiwa chini ya usimamizi wa askari.
Huku mama yake akiwa analia akitaka kwenda kumuona mtoto wake Nesi aliyekuwa zamu , akimwambia atulie huku wazazi  wenzake akina mama Meshack na Mama Tegete nao wakijalibu kumtia moyo ,
Mkuu wa askari aliwaamuru maskari wenzake wawachukue akina Meshack na Tegete waondoke nao kwenda kituoni kwa ajili ya maelezo huku askari mmoja akiamuliwa kubaki hospitali illi kujua kinachoendelea.
Akina mama meshaki  na mama Tegete nao walianza kuwalilia watoto wao lakini askari mmoja aliwaambia kuwa wapo kwenye usalama  kwa hiyo wasijali, wakiwa nje wakisubilia ripoti ya daktari mara gafla daktari anatoka walipomuona daktari walimkimbilia ili awape hali inavyoendelea kwa wagonjwa.
Jibu alilowapa daktari kuwa wavute subira bado wanaendelea na uchunguzi iliwabidi warudi wakaketi huku wakiwa bado hawajui hali ya mtoto wao, muda  ulizidi kwenda  na tazama sasa  yapata saa mbili usiku, huku madaktari wakiingia na kutoka katika wodi ya wagonjwa mahututi, punde aliingia
Baba Meshaki akiwa na watoto wake akina Tegete na Meshaki  na muda huo manesi nao walikuwa wakimtoa Oscar katika chumba cha watu mahututi  na kumpeleka kwenye wodi za kawaida ilikuwa ni kimbembe kwani kila mtu alikuwa anataka kumuona huku majonzi yakiwatawala,
lakini madaktari waliwakataza  kumuona kwa sasa mpaka hapo baadaye baba  meshaki  na baba Oscar walimfuata daktari mmoja ambaye alikuwa akitoa huduma kwa Oscar  na Yule mtoto ili awape majibu naye aliwajibu  yeye si anayetakiwa kutoa taarifa  bali wawe na subira tu.
Iliwabidi wawaambie wake zao waludi nyumbani watakuja kujua taarifa rasmi kesho  na wao walikubali lakini meshaki na Tegete wao waligoma kuondoka na kutaka kulala hapo hapo huku meshaki akiwa amekaaa kwenye mlango alipolazwa rafiki yake , lakini walibembelezwa  na hatimaye  waliondoka na kurudi nyumbani ili wakapumzike na kujiandaa kwa kesho.
Hapo hospitalini alibaki askari mmoja ambaye alikuwa akisimamia kila matukio yaliyokuwa yakifanywa na madktari , usiku mida kama saa 7 madaktari walimwita askari Yule na kumuambia hali ya wagonjwa ilivyo .
Daktari bwana tumekuita kukuambia hali halisi ya afya ya Oscar inaendelea vizuri lakini Yule mtoto amepotea katika mazingira ya kutatanisha wakati tunajalibu kumtibu na kilicho tushangaza kuna ujumbe  uliokuwa kwenye shati la mtoto Yule umeandikwa “ukome kumfuatilia binti yangu”.
Polisi “uwenda huu ukawa ni mchezo  ambao familia ya Yule binti ilikuwa kumuangamiza Oscar”
Daktari “Ni kweli  kabisa huyu Oscar alikuwa anamtaka binti furani  ndio maana walitaka kumuua kwa njia ya huyu mtoto aliyepotea”
Polisi “Ndio maana yake”
Wakati wamemaliza maongezi hayo sasa polisi anataka kwenda kupumzika akiwa bado na daktari Yule wakitoka pamoja, upepo mkali ulitokea huku sauti za ajabu  zikisikika zikisema “Oscar achana na mwanangu Naomi” wote walilala chini na sauti
Oscar ilisikika kwa mbali ikisema “ mamaaaa nakufa “ daktari na yule polisi baada ya kusikia hiyo ya Oscar walikwenda kumuangalia oscarwalimkuta Oscar akitokwa na jasho la ajabu iliyomfanya daktari kuchukua baadhi ya dawa na kumpa anywe , gafla hali yake ililudi sawa.
Daktari alip[omuuliza Oscar ninin tatizo?
Oscar ahkuweza kuongea bali alikuwa akionesha ukutani daktari pamoja na polisi walijaribu kuangalia ukutani hawakuona kitu  waliona sasa ni bora wabakinaye wodini mpaka kesho yake.
Asubuhi palikucha ilikuwa ni saa kumi na moja alfajiri  familia zote za marafiki hao zilikuwa zimekwisha fika katika hospitali hiyo ili kujua hatma ya ndugu yao siku hiyo waliruhusiwa kwenda kumtazama  Oscar, wote waliingia huku wakiwa wamebeba vyakula mbalimbali na matunda walimkuta Oscar yupo kitandani , naye alipowaona marafiki zake alitabasamu japo kuzungumza kwake kulikuwa ni kwa kusuasua ,
ikawa saa mbili asubuhi  kengele ikagongwa kuashiria muda wa kuona wagonjwa umeisha, nesi aliingia na kuwaomba watoke nje kwani madaktari wanakuja kutoa huduma , wakiwa wanatoka.
Baba meshaki na baba Oscar walikwenda kwa daktari anaye muhudumia Oscar ili awape ripoti walimkuta daktarI akiwa amesinzia ofisini kwake walimshtua ndipo alipoamka na kuwapa taaarifa kamili kuhusu maendeleo ya Oscar.
Daktari: aliwapa mkasa uliowakuta  usiku wa kuamkia leo, kila mmoja baada ya kuambiwa habari hizo alishangaa sana, baada ya muda kidogo walitoka nje na kuwakuta wenzo wapo nje wakiwasubili walipanda gari nakuondoka.
Usiku uliingia meshaki alikuwa chumbani kwake akiperuzi kwenye mtandao  na kompyuta yake mara mama yake aliingia na kumwita kwamba baba  ana mazungumzo naye, meshaki alitoka chumbani kwake na kwenda kumsikiliza baba yake.
Baba meshaki mwanangu nimekuita hapa nataka uniambie huyu Naomi ni nani kwenu?
Meshaki alishang’aa kusikia jina hilo kwa baba yake huku akijiuliza amemjuaje?
Meshaki “Ni mwanafunzi mwenzetu tunasoma naye “
Baba “Ahaa! anafahamiana vip na Oscar
Meshaki alijibu huku huklum akiwa ana mashaka mashaka “NI nini alikuwa anataka kuwa mchumba wa Oscar”
Baba “Ahaak kumbe basi msije kurudia tena huyo msichana familia yake sio nzuri walitaka kumuua mwenzako”
Meshaki akiwa anashangaa alijibu kwa uoga sawa baba “ sawa na baadae aliludi  chumbani kwake huku akionekana kuwa ni mwenye mawazo.
BAADA WIKI KUPITA
 Madaktari walimruhusu Oscar kutoka baba Oscar alifika kwa daktari ili kuweza kulipa gharama za matibabu kiasi alichoambiwa kilikuwa ni shilinhi laki 5, pesa hiyo hakuwa nayo  hivyo alimuomba daktari kulipa kiasi nyingine atamlizia baadae lakini bado wakiwa na mazungumzo alikuja baba meshaki na kulipa kiasi shote sha pesa, baba Oscar alimshukuru sana baba  meshaki lakini alijibu tunasaidiana  tu waliondoka na kurudi nyumbani Oscar alikuwa akipewa matibabu madogo madogo nyumbani kwa akina meshaki
BAADA YA MIEZI 2 KUPITA
Hali ya Oscar ilirudi sawa kama alivyokuwa zamani ,huku akiwa anafanya mazoezi madogo madogo, alianza kuhudhuria masomo shuleni  kama kawaida na kushirikiana na wenzake, siku moja marafiki hao walikutana maeneo ya ufukwe wa bahari kwa lengo la kwenda kusoma na kubadilishana mawazo.
Maongezi yao yalikwenda hivi
Oscar ‘washikaji mimi huu msala ulionitokea sita usahau maishani mwangu “
Meshaki na Tegete: kwa pamoja “kwa nini?
Oscar: “unajua mkasa wote huu chanzo ni Naomi”!  
Tegete: Naomi kafanyaje?
Oscar: alitaka kuniuana sijui ningekuwa naye  kabisa ingekuwaje
Tegete: kwa mshangao “ inamaaana familia yake yote ndio uliyo ucheza mchezo huu?
Oscar: ” Ndio maana yake lakini namshukuru mungu , hakutaka  nife mapema“
Tegete na Meshaki: walicheka huku wakimtania “ Haah ndio tukome kuvizia watoto wa watu“
Baada ya hapo waliondoka  nakuanza kurudi majumbani kwao huku wame mbebea madaftari yao.

BAADA YA MWAKA MMOJA
Oscar, meshaki na Tegete walikuwa wapo  katika maandalizi ya mtihani wao wa mwisho wa kumaliza elimu ya sekondari yaani kidato cha nne(form four), walikuwa wakisoma wote kwa pamoja  kwa akina Meshaki ndio ilikuwa sehemu ya yao kuu ya kujisomea, walisoma mchana mpaka usiku, tena usiku ndio walisoma sana, walikuwa wakiamshana ili wasome .Muda uliokuwa umebaki ili waanze mtihani wao wa Taifa ni wiki moja, hivyo kila mtu alikuwa bize kusoma ili wafaulu mtihani.
Siku ya ya mtihani ilifika Oscar, Tegete na Meshaki wakiwa nyumbani wakijiandaa, baba Meshaki naye siku hiyo alikuwa na safari ya kwenda Mtwara kufuata mbao, hivyo kabla hajaondoka aliwaita na kuwasihi kuwa makini katika mtihani wao na aliwapatia kila mtu elfu ishirini huku akiwaahidi endapo watamaliza mtihani salama atawapatia zawadi nzuri kila mtu, baadaye aliondoka huku akisindikizwa na mkewe.
Akina Meshaki wao walifika shuleni na kuwakuta wakaguzi tayari wamefika , kabla ya kuingia katika chumba cha mtihani  walikaguliwa kama wameingia na kitu cha kuangalizia na baadaye walianza mtihani, ilichukuwa takribani masaa mawili na nusu kumaliza mtihani huku kila mtu akijigamba kufaulu vizuri, Tegete na marafiki zake walikwenda kunywa chai sehemu ili wajiandae na mtihani wa pili, mara kengele ikagongwa warudi kwenye vyumba vya mtihani kuendelea na mtihani unaofuata, waliingia na kufanya mtihani huo.
BAADA YA SIKU TATU
Wakiwa wamebakiza mitihani miwili wamalize mitihani yao, siku hiyo zililetwa taarifa shuleni hapo na ndugu wa meshaki kwa mkuu wa shule kuwa baba yake Meshaki amefariki  kwa ajali ya gari, wakati huo Meshaki akiwa yupo kwenye chumba cha mtihani akiendelea na mtihani walipo maliza wanafunzi wote wakitoka madarasani, Meshaki alikuwa na rafiki zake wakipiga stori kuhusu mtihani mara anatokea mwanafunzi mmoja akimpa taarifa Meshaki kuwa anahitajika na mwalimu mkuu ofisini kwake.
Meshaki alikwenda  kumsikiliza mwalimu kitu gani anamuitia, lakini alipokuwa akielekea ofisini kwa mwalimu mkuu alishangaa kumuona mfanyakazi wao bosco aliyekuwa na tax, amesimama kwenye mlango, alimwita bosco vipi” bosco akiwa amevaa miwani nyeusi alijibu “poa kaka”.
Meshaki kwa hali aliyomuona nayo bosco alihisi kitu lakini aliingia ofisini kwa mwalimu mkuu na kumkuta mwalimu mkuu ameketi akiendelea na kazi.
Mwalimu mkuu: alianza mazungumzo na Meshaki, “ hongera Meshaki kwa hatua uliyofikia kwani wapo wengi wameshindwa kufikia hatua uliyopo”.
Meshaki :akiwa anashangaa “Asante mwalimu”  
Mwalimu mkuu; “Nina hakika na ninvyokujua mpaka hapo ulipo tayari umefaulu.
Meshaki; “ Asante mwalimu”
Mwalimu mkuu; “ Meshaki wewe ni mtoto wa kiume na unatakiwa kuwa jasiri katika kila hali”
Meshaki; “sijakuelewa mwalimu unamaanisha  nini kusema hivyo”
Mwalimu mkuu; “ Ni kwamba mzee amefariki dunia yaani baba yako mzazi”
Meshaki akiwa ametoa macho mithili ya mtu aliyeganda  huku akitokwa na machozi na kupiga meza, Meshaki; “ Haiwezekani mwalimu, kwa nini imekuwa hivyo?”
Mwalimu mkuu akimbembeleza kwa kumshika mgongo “ jikaze ndo hali ya dunia” mwalimu alimtoa nje ili apelekwe  nyumbani, wakati wanatoka nje marafiki zake walikimbia haraka ili kujua rafiki yao kapatwa na nini, walipewa taarifa nao waliingiwa na uchungu huku wakilia, kengele nayo ikagongwa kuashiria mtihani wa pili unakwenda kuanza, ilibidi walazimishwe kwenda kufanya mtihani huku hali yao ikiwa ni ya huzuni na majonzi,
Meshaki alibebwa maana alishindwa kusimama kabisa ndipo Bosco akisaidizana na mwalimu mkuu walimuingiza ndani ya gari na kuanza kurudi nyumbani. Walifika nyumbani huku watu wakiwa wameshafika tayari kwa ajili ya kumfariji mfiwa, alipofika Meshaki alianza kilia mpaka muda mwingine alikuwa akizimia, watu walifurika huku wanandugu wakijadiliana kuuleta mwili kutoka katika sehemu ulipokuwa umehifadhiwa, baada ya muda muda muda wanafunzi wenzake walifika ili kumfariji ndugu yao, Muda ulipita na sasa yapata saa tano usiku mwenyekiti wa kamati ya mazishi akatoa ratiba kuhusu siku mwili utakapokuwa unaletwa  na siku ya mazishi yatakapofanyika.

BAADA YA SIKU MBILI
Mida ya saa nne asubuhi mwili uliletwa kutoka mochwari huku ukiwa ndani ya gari la kubebea maiti ilikuwa ni majonzi na vilio ndugu, marafiki walijitokeza kuuaga mwili wa marehemu na baadaye ulipelekwa katika makaburi ya Miami tayari kwa kuupumzisha mwili wa marehemu, mapadri nao walikuwepo kumuombea marehemu na baadaye watu walitawanyika kurudi  majumbani kwao.
BAADA YA MWEZI MMOJA
Ndugu wa marehemu walikuwa na mkutano wa kifamilia kuhusu hatma za mali za marehemu katika mkutano huo uliochukua takribani masaa manne walikubaliana  kuwa mke wa marehemu ndiye atakuwa mrithi wa mali zote za marehemu, baadaye ndugu walitawanyika na kuendelea na shughuli zao. Maisha yalianza upya huku ndugu na marafiki wakijaribu kuja kuwafariji n a kuwatia moyo.

BAADA YA MWAKA MMOJA
Matokeo ya akina Meshaki yalikuwa tayari yametoka, Meshaki siku hiyo alipewa taarifa na mama yake kuhusu matokeo ndipo alipowapigia marafiki zake waje kujiangalia punde.
Tegete na Oscar  walifika kuangalia matokeo yao , hayakuwa ya kuridhisha kwani wote walikuwa wamefeli, walihuzunika sana hasa wakifikiria jinsi walivyokuwa wakisoma lakini ndugu zao waliwatia moyo. Siku moja Meshaki alikuwa ameketi na mama yake wakishauriana nini wafanye baada ya kuwa matokeo yake kuwa mabaya, wakizungumza
Meshaki; “ Mama mimi sijafanikiwa kufaulu lakini bado nataka kusoma”
mama; “usijali nitakutafutia chuo utasoma” maneno  hayo yalimfariji sana Meshaki na kusema “ Nitashukuru sana mama”.
Siku iliyofuata mama meshaki alianza kumtafutia mwanaye chuo na kwa kuwa Meshaki alisema anapenda sheria, basi mama yake alikuwa akimtafutia chuo cha sheria. Wakati akiwa katika harakati hizo huku akiongozana na Meshaki mwenyewe ilimbidi kusafiri  mpaka Dar e s salaam kwani huko vyuo vingi ndio vilikuwa vinapatikana  kulinganisha na sehemu zingine, wakati anatoka katika chuo kimoja, sasa anataka kuingia ndani ya gari yake akiwa na Meshaki mwenyewe, mara dada mmoja alimuita kwa jina “mama Meshaki” .
Mama Meshaki anageuka nyuma na anamuona dada huyo ambaye yeye asili yake alikuwa ni mkenya, mama Meshaki alkimtazama kwani hakuwa amemfahamu.  Maongezi yao yalikwenda hivi “ wewe ni nani na umenijuaje”
Yule dada na Kiswahili chake cha kikenya anajibu “ mimi ni Yule mtu niliyekuja kutoa semina kwa wanawake kanisani bagamoyo”, mama Meshaki; “ ahaaaa dada Matha” Huku wakikumbatiana kwa furaha.
Mama Meshaki “ Habari za siku na huku Tanzania umekuja kwa semina au vipi”,
dada; “ hapana nimekuja kufuatilia cheti cha kuzaliwa cha mdogo wangu”
Mama Meshaki ; “ kwani imekuwaje?”
dada; “ Amepata nafasi ya kusomeshwa na shirika moja nchini Canada sema imekosekana nafasi moja”.
Mama Meshaki; “ ndugu yangu muunganishe mwanangu naye akasome huko”
Dada; “ usijali nitakujulisha tena naweza kukuunganisha na wafanyabiashara wa vipodozi kutoka Canada”.
Mama Meshaki akionyesha tabasamu la furaha alisema “ nitafurahi sana ndugu yangu”
dada; “ usijali cha msingi tuwasiliane”. Baada ya maongezi hayo dada Yule aliendelea na shughuli zake huku mama Meshaki na meshaki wakiondoka wakiwa na furaha ya ajabu.
BAADA YA SIKU TATU
Mama meshaki akiwa na mwanae Meshaki wakiendelea kuhudumia wateja dukani kwao, mama Meshaki anapokea simu kutoka kwa dada matha ikimtaka aanze maandalizi ya kujiandaa kwa safari ya kwenda Canada kwani mipango yote dada Yule aliweka sawa huku wote wakitakiwa kwenda siku inayofuata.
Mama  Meshaki alianza maandalizi ya kutafuta viza na mambo mengine yanayohusiana na safari  huku akiwa  amepewa wiki moja kukamilisha mambo yote .
Meshaki aliwajulisha marafiki zake  wakina Oscar na Tegete kuhusu safari ya kwenda nje ya  nchi kwenda kusoma hivyo hatakuwepo  akina  Oscar na Tegete   wao hawakuwa na uwezo wa kujiendeleza kielimu kutokana na wazazi wao kutokuwa na uwezo mkubwa kifedha.
Meshaki aliwatia moyo kuwa majasiri na waendelee kushirikiana katika kila jambo huku akiwasisitiza upendo.  
Siku iliyofuata mama Meshaki aliwaita ndugu zake na kuwapa habari kamili na kuwagawanisha baadhi ya vitu, ndugu walimshukuru sana.
Siku ikafika mama Meshaki na mwanaye Meshaki walikuwa tayari wanajiandaa kuondoka , huku Oscar na Tegete nao wakiwa mstari wa mbele wakimsindikiza  rafiki yao, walipanda gari kuelekea  Dar  es salaam huko walikutana na dada Matha akiwa  na mdogo wake wa kike Joyce wakisubiri ndege kwenye uwanja wa Mwalimu Nyerere, majira ya saa 5 usiku walianza safari kuelekea nchini Canada.
 itaendelea kipindi kijacho.......

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4