BEHIND OF MY EYES (NYUMA YA MACHO YANGU) SEHEMU YA NNE.

TITLE :BEHIND OF MY EYES
(NYUMA YA MACHO YANGU)
MWANDISHI JOHN JACKSON
SEHEMU YA NNE.
 BAADA YA WIKI 2 KUPITA
Meshaki analudi na Joyce walikwenda kupokelewa na ndugu zake na baadye kuanza maisha
Joyce alikua hajakamilisha shughuliza zake za uamisho hivyo alikuwa anafanya kazi za umama nyumbani akisaidiana na mama Mkwe wake,Wakati akisubilia mambo yake yakamilike aanze kazi.
Siku moja Mama Meshaki akiwa jikoni, Oscar aliingia na kumshika kiunoni na shughuli za upishi zilikwama maana walianza kupeana mapenzi jikoni.
Kwa kelele za vyombo kuanguka anguka ovyo vilimfanya Joyce kuamka usingizini na kwenda kutazama nini kinachoendelea.
Joyce alipokaribia maeneo ya jikoni alipishana na Oscar akionekana kuufunga mkanda wa suluali yake, alishangaa na lipoingia jikoni alimkuta Mama Meshaki akiahangaika kujifunga khanga  vizuri.
Joyce kwa hali hiyo ilihisi kutakuwa na jambo linaendelea na Mama Meshaki alipoulizwa na Joyce  kama kuna tatizo?
Mama Meshaki alicheka kicheko cha wasiwasi “hapana kitu mwanangu”
Joyce: aliondoka na kurudi chumbani kwake alipopita sebuleni alimuona Oscar ameketi akitazama runinga.
Oscar: alijua wazi kwa jinsi alivyokuwa joyce atakuwa ameona  kilichotokea haraka alimfuata Mama Meshaki na kuzungumza naye.
Oscar: beby vip huyu shemeji ameshajua mchezo wetu
Mama: Meshaki “ usijali hakuna kilicho haribika
Oscar: kwa woga hasa itakuwaje
Mama: Meshaki “Niachie mimi nitayamaliza.”
  
     BAADA YA WIKI 2
Meshaki ameketina Mama sebuleni, wakizungumza
Meshaki “Mama vip kazi zinaendeleaje”?
Mama “Nashukuru mungu zinaendelea vizuriila jumamosi nataka niende Tanga nikanunue kiwanja kingine ila naomba niondoke na Oscar ili akanisaidie mambo furani”
Meshaki “Mtatumia siku ngapi”? maana Oscar anaitajika ofisini.
Mama Aah mwanangu ni siku chache tu
Meshaki  alimruhusu kuondoka na Oscar.
Siku moja kabla ya safari usiku mama meshaki akiwa chumbani kwake alimpigia simu Oscar ili aje.
Oscar naye alitoka chumbani kwake na kuingia chumbani kwa mama meshakki ili wakafanye mapeenzi
Asubuhi alfajiri mida ya saa kumi na moja Oscar anatoka chumbani kwa mama meshaki, na alipokuwa anatoka alikutana na joyce akitoka msalani
Joyce alijuwa wazi kuwa kuna uhusiano wa mapenzi kati ya Oscar na mama mkwewake kwa tendo hilo Oscar naye ndipo alijua wazi kuwa joyce anajua kila kitu .
Muda wa kuondoka ulifika Oscar na mama meshaki lakini joyce alikuwa haoneshi imani na safari yao, Meshaki Hakuwa anajua kitu kinachoendelea.
TANGA  
Wakiwa wamepanga katika hoteli moja , mjini humo, wakijivinjari siku moja Oscar  alimuacha Mama Meshaki na yeye aliondoka, Oscar kwa kuwa anaogopa,  mchezo anaoufanya, na alijua wazi Joyce  anajua kinachoendelea, alikwenda kwa mganga, kwa lengo la kumfanya Joyce  kuwa chizi ili asitoe siri  kwa Meshaki, alipokuwa anatoka kwa mganga. Jamaa mmoja rafiki yake Meshaki aitwae Tom  alimuona na alikuwa  akimpiga picha kila tukio afanyalo.
UPANDE WA PILI DAR ES SALAAM.
Meshaki alikuwa bichi na Joyce,
Joyce: alionekana kutaka kusema jambo kwa Meshaki, lakini katika hali ya kushangaza  Joyce  alibadilika nakuanza kurukaruka  misili ya mtu aliyechizi,
Meshaki: Alifikiri ni hali ya kawaida  lakini kadri muda unavyozidi kwenda.
 Joyce: Alizidi kubadilika, 
Meshaki: Alipiga kelele kuomba msaada kwa watu, ndipo anafanikiwa kumkamata, na kumpeleka hospitali , Meshaki akiwa amechanganyikiwa, asijue afanye nini,
Tegete: Anapata taarifa na kwenda Hospitali ili kusaidizana.
TANGA
Oscar: Anarudi katika hoteli  aliyopo mama Meshaki na kuendelea na mapenzi kama kawaida yao, huku mama Meshaki asijue Oscar kafanya jambo gani.
Tomasi: Rafiki yake Meshaki  aliendelea  kupeleleza na sasa aliwatumia wahudumu  ili wampe taarifa na kupiga picha matukio yote yanayoendelea kuhusu Oscar.
 wakiwa wamepumzika Mama Meshaki anapokea simu kutoka kwa Tegete akimpa taarifa kuhusu hali ya Joyce,
Mama Meshaki :Alishtuka sana  kisha alimpa taarifa Oscar,
Oscar: hakuonesha kujali kauli huku akimtaka aendelee kula raha. Siku iliyofuata walianza safari krudi Dar.
DAR ES SALAAM.
Joyce akawa ni mtu wa kukaa ndani na kwa hali aliyokuwa nayo hakuweza kufanya jambo lolote, hali ile ilimfanya Meshaki ashindwe kufanya kazi vizuri  maana kila muda alikuwa nl mtu mwenye mawazo , marafiki zake Tegete na wafanyakazi wenzake  walikuwa wakimtia moyo na Oscar akiwemo. Siku moja meshaki alikuwa kazini kwake, na siku hiyo  rafiki yake Tomasi alikwenda kumsalimia lakini katika mazungumzo yao.

Tomasi ;”Kaka juzi nilikuwa Tanga , lakini nilishangazwa kumuona Mama na Oscar wakiishi hoteli moja.
Meshaki “Eehnee”.
Tomas: Na siku moja nililmuona Oscar akitoka kwa mganga.
Meshaki : kwa mganga! alikuwa akifanyaje?’
Tomasi : sijui ila nahisi Oscar atakuwa na mahusiano ya kimapenzi na mama, pia wenda atakuwa amehusika katika ugonjwa wa Joyce”.
Kauli hiyo ilimfanya Meshaki acheke 
Meshaki: “Acha zako bwana, nitaaminije?”ndipo
Tomasi: anatoa baadhi ya picha za Oscar na mama Meshaki wakiwa katika hali ya kimapenzi,
Meshaki No, no, no, no, haiwezekani kweli kaka hapana “Meshaki aliondoka hapo hapo na kuchukua gari yake kurudi nyumbani, Meshaki aliingia ndani na kumkuta Joyce ametelekezwa sebuleni, Meshaki aliita “mama, mama bila majibu alikwenda kufungua mlango wa chumba cha mama yake, alimkuta mama yake akifanya mapenzi na rafiki yake Oscar.
Meshaki: alipigwa na butwaa”Mama hiki nini? Akitokwa machozi, huku akimuangalia rafiki yake Oscar,
Oscar akiwa na uso wa aibu, Mama naye akianguka kwa presha, Meshaki akiwa amesimama mlangoni, akimshika shati Oscar huku  akitokwa machozi, alishindwa kuzungumza, Oscar kwa aibu alikimbia chumbani kwake,
Tegete: naye aliingia ndani na kuona hali  ya tofauti  Meshaki bado akiwa chumbani kwa mama yake, akilia sana, Tegete alikwenda chumbani kwa Oscar, na alipoingia alimkuta Oscar amekunywa sumu na akitokwa na mapovu mdomoni akiwa tayari amekufa, Tegete alipiga kelele,
Meshaki: naye alikwenda na kukuta hali hiyo huku kukiwa na ujumbe ulioandikwa na Oscar ukimtaka radhi Meshaki kwani hata  ugonjwa wa Joyce alihusika,
BAADA YA SIKU 3:
Mama Meshaki akiwa hositali sasa amepata nafuu, alikuwa akimuomba msamaha Meshaki kwa kosa alilolitenda, Meshaki alimsamehe mama yake.
BAADA YA MIAKA 2.
Joyce alipona baada ya kuombewa na sasa wamepata mtoto, huku
Tegete: amepewa madaraka  makubwa ya kiofisi, maisha yakaendelea kuwa mazuri zaidi.
            MWISHO.
USIKOSE KUSOMA HADITH TAMU HAPA HIVI KARIBUNI..........

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4