Gazeti la MTANZANIA leo alhamisi Oktoba 23, limeripoti kuwa watuwawili wamefariki dunia katika kijiji cha milanda ,Tarafa ya Nshamba ,Wilaya ya Muleba mkoani Kagerabaadaya kula ugali wa mhogo unaosadikiwa kuwa na sumu.-
TITLE: MWALIMU MAGDALENA SEHEMU ya kwanza Kwa wasomaji wapya Maisha ya shule yalimwendea vibaya John Sahau akajikuta akiangukia kwenye dimbwi la mapenzi ya mwalimu wake, Mwalimu Magdalena, shuleni hapo lakini kuhamia kwa mwalimu mpya wa somo la hisabati kuna badilisha maisha ya John kiasi cha kushindwa kuendana na kasi ya masomo kama alivyokuwa awali. Nini Mwalimu anafanya baada ya kugundua mwalimu mpya ndiyo chanzo cha kushuka kiwango kwa John? Fuatilia hadithi hii ya kusisimua ya Mwalimu Magdalena. Endelea BAADA ya kuisha kwa hadithi ya ‘ BEHIND OF MY EYES ’ leo tunawaletea hadithi mpya inayokwenda kwa jina la ‘ Mwalimu Magdalena ’. John anawahi mapema kufika shuleni akiwataka wenzake wakamalizie kipande walichokiacha siku iliyopita ili mvua zitakapoanza wawe wameshamaliza kazi hiyo. Inawachukua muda mfupi kumaliza kipande hichowanaingia darasani kwa ajili ya masomo. Lakini kipindi cha mwalimu Magdalena kinapofika hali ya John inab...
ilipoishia Mazungumzo yao yaliendelea, wakafika nyumbani kwa mwalimu Magdalena, wakapitiwa na usingizi, kutokana na uchovu waliokuwa nao mwalimu Magdalena na mwalimu Joka wakajikuta wakiamka saa 4 asubuhi, tena baada ya John kuwagongea kutokana na kutomuona mwalimu Magdalena shuleni. “Sasa itakuwaje, nje kuna hodi inagongwa na sauti ya huyo mtu namjua ni wa shuleni, kama akikuona itakuwa balaa upya, watahisi kuna kitu kimefanyika kati yangu na wewe, sasa naomba ujifiche humu humu ndani mi natoka kumsikiliza.’’ “Sawa.” sasa endelea Mwalimu Magdalena alipotoka nje akakutana na John, mwanafunzi anayempenda, John hakutaka kuhoji chochote hadi aingie ndani lakini mwalimu Magdalena alionyesha hofu kama ya kusita, lakini akakubaliana na yote, John akaingia akakaa kitandani huku mwalimu Joka akiwa amejificha chini ya uvungu wa kitanda cha mwalimu Magdalena. “Mwalimu mbona hadi sasa hujafika shuleni kila mtu anahofu nawe, hakuna anayeelewa somo lolote hadi wakuone, mwa...
Ilipoishia Mwalimu Magdalena alikimbia huku akipiga kelele bila kujua anakokimbilia angepata msaada ama la! Alishaanza kuchoka na ilikuwa giza sana, lakini alichoambulia kugundua ni kwamba mtu aliyekuwa akimkimbiza alikuwa amevaa kinyago na nguo nyeusi ili asitambulike. Sasa Endelea GHAFLA mwalimu Magdalena akajikuta akikamatwa na kufumbwa mdomo, alikukuruka ili ajitoe katika mikono iliyombana vema, lakini hakuweza kuitoa, alijitahidi kujitoa mbele ya mtu huyo aliyemfumba mdomo, sauti pia miguu yake havikumsaidia kufanya chochote kujikwamua kutoka eneo hilo. Mwenyekiti alishangaa kutosikia sauti ya mwalimu Magdalena, akaangaza huku na kule, lakini hakuweza kutambua wapi alipo mwalimu Magdalena, alinyanyua macho huku na huko, lakini hakufanikiwa. Taratibu Mwalimu Magdalena alikuwa akipoteza nguvu kutokana na kubanwa na asiyemjua, mtu yule alimvuta eneo lingine ili kumkwepa mwenyekiti aliyekuwa akimsaka mwalimu Magdalena ili atimize ahadi yake. Mwenyekiti alianza kuhama...
Maoni
Chapisha Maoni