Hadithi BEHIND OF MY EYES (NYUMA YA MACHO YANGU sehemu ya pili
TITLE : BEHIND OF MY EYES
(NYUMA YA MACHO YANGU)
MWANDISHI : JOHN JACKSON
SEHEMU : YA PILI
Iliwachukua takribani
masaa nane na walifanikiwa kufika nchini Canada majira ya asubuhi
huku msimu wa barafu kuanguka ulishika hatamu, wakiwa wamevalia makoti
walikuta wenyeji wao wanawasubiria, walichukuliwa na wenyeji wao na
kuanza safari ya kuelekea jijini maska, mji ambao upo nje kidogo ya
mjini wa Canada takribani masaa mawili hadi kufika Maska.
Walifika Maska mpaka
sehemu ambayo watakuwa wakiishi kila familia ilipewa nyumba ya kuishi.
Mama Meshaki na mwanaye , Matha na mdogo wake Joyce maisha ya Canada
yalianza.
Siku iliyofuata Meshaki
na Joyce walipelekwa katika chuo ambacho watakuwa wakisomea na kutambulishwa
kwa wanafunzi wenzao na kupewa siku ya kuanza masomo. Joyce yeye alikuwa
ni raia wa Kenya hivyo walikutana na wanafunzi ambao ni raia wa Kenya
na watanzania kadhaa hivyo walijenga nao urafiki,
Meshaki na Joyce walianza
rasmi masomo yao japo hawakuwa wamezoeana sana, ikizingatia Meshaki
kiingereza kilikuwa kidogo kinampiga chenga hivyo muda mwingi
alijitahidi kuwa na joyce kwa kuwa Joyce kiingereza alikuwa anakifahamu
maana aliishi Kenya ambao wao walijua kukizungumza.
BAADA YA MWEZI MMOJA
Meshaki na mama yake
walikuwa wameanza kuzoea mazingiria ya huko , huku mama Meshaki
naye akiendelea na biashara walizokuwa wakizifanya na dada Matha.
Siku moja Meshaki na
Joyce walipotoka darasani walikwenda maeneo ya Stiwathall sehemu walipokuwa
wanapika chakula cha kiafrika walifika na kuagiza chakula huku wakizungumza
Kiswahili sehemu hiyo ilikuwa ni sehemu ambapo waafrika wanaoishi huko
huenda kwa kula chakula cha nyumbani wanakotoka, baada ya kutoka sehemu
ile walipanda tax na kurudishwa majumbani kwao kila mmoja alirudi kwa
ndugu yake.
BAADA YA MIEZI MINNE
Ilikuwa ni siku ya jumapili,
Meshaki na mama yake walikuwa wanatoka nyumbani kwao wanataka kuelekea
kanisani wakiwa wamependeza meshaki aliingia ndani ya gari na kuanza
kuendesha huku akiwa amempakia mama yake walipokuwa wanatoka getini
walisikia mlio wa risasi huku sauti ikisema “mamaaaaa” sauti hiyo
ilitokea nyumbani kwa Matha .
Meshaki alishuka ndani
ya gari upesi na kuelekea nyumbani kwa Matha , mama yake alibaki
kwenye gari amejificha,
Meshaki aliingia getini
na kumkuta mlinzi amekufa alipigwa na butwaa lakini alitaka kuingia
ndani ili kujua kinachoendelea alifanikiwa kuingia ndani kwa kupitia
dirishani, alipoingia aliona wazungu wawili wakiwa wamewaweka
chini ya ulinzi akina Joyce na Matha huku wameshika bastola na kumuuliza
Matha “ kwa nini unafuatilia maisha yetu” matha alijibu kwa woga
“ hapana sio mimi”, shughuli nyingine ya Matha alikuwa akiandika
makala katika magazeti ya nchini humo , hivyo aliandika makala kuhusu
mashirika yanayojihusisha na uuzaji wa watoto, wakiendelea na mazungumzo
Meshaki alitokea na kumrukia begani jambazi mmoja na kuanza kupambana
nao, jambazi mmoja alimpiga risasi ya tumbo Matha wakati akiwa
katika harakati ya kujikomboa ,
Matha alianguka papo
hapo Joyce alimkimbilia shangazi yake huku Meshaki akiendelea
kupambana nao alifanikiwa kumpiga risasi jambazi mmoja mwingine
alitokomea.
Mama Meshaki naye akiwa
tayari ameingia ndani huku taarifa zikiwa tayari zimefika polisi,
polisi nao walifika haraka kisha kumchukua jambazi Yule aliyepigwa
risasi ya mguu na meshaki na kuondoka naye huku Meshaki naye akimchukua
Matha na kumuweka ndani ya gari ili kumkimbiza hospitali wakiwa njiani
wanakaribia hospitali Matha alizidiwa sana hivyo alipoteza maisha akiwa
mikononi mwa mama Meshaki,
Mama Meshaki alijua
wazi Matha rafiki yake amekufa alitoa sauti ya kilio walifika hospitalini
na kupokelewa na madaktari lakini madaktari walishindwa wafanyaje maana
alikuwa tayari ameshakufa, madaktari walitoa taarifa ya kudhibitisha
kifo cha Matha, wote walibaki mikono juu huku wakiangusha kilio, Shirika
lililowafadhili nalo lilimtuma mkurugenzi wake kuleta salamu za rambi
rambi.
BAADA YA MWEZI MMOJA
Meshaki akiwa na Joyce
darasani aliona hali ya Joyce sio nzuri maana alionekana ni mwenye mawazo
sana baada ya kifo cha shangazi yake, Meshaki alimfuata na kuanza kumpa
maneno ya kumfariji huku akionesha kumchekesha kwa kumkumbusha baadhi
ya vichekesho kwa maisha waliokuwa wanaishi Joyce na Meshaki watu
hasa wanafunzi wenzao walikuwa wakiwatania mke na mume.
BAADA YA MIAKA MITANO
Ilikuwa ni siku ya mahafali
katika chuo hicho ambapo darasa la akina Meshaki ndio walikuwa wakihitimu
shahada zao za kwanza, Meshaki katika taaluma ya usanifu majengo na
Joyce katika mambo ya usimamizi wa fedha,
sherehe hizo zilifana
sana , mama Meshaki akiwa ndio mzazi wao, walipiga picha za ukumbusho
wote pamoja, ilikuwa ni furaha sana, mama meshaki pia aliwaandalia zawadi.
Wakiwa nyumbani baada ya sherehe hizo kuisha, muda wa usiku ulifika,
Meshaki akimsindikiza
Joyce kurudi nyumbani wakiwa njiani wakitembea kwa miguu, Meshaki alimueleza
Joyce hisia zake. Maongezi yao yalikuwa hivi
Meshaki; “ Joyce najua
tumeishi na wewe takribani miaka kadhaa sasa, lakini sijawahi kukuonesha
hisia zangu”.
Joyce anatabasamu,
“unajua sikuelewi hisia gani ulizonazo kwangu?”
Meshaki; “kutoka
moyoni kweli Joy nakupenda sana nahitaji siku nikuoe uwe mke wangu”
Joyce; “ haitawezekana
Meshaki, wewe kwangu ni kama kaka tu hivyo naomba uniache”.
Joyce alifungua geti
na kuingia kwake,
Meshaki akiwa anatokwa
na machozi akisema “Joyce nakuomba nikubali basi” alipiga geti na
teke alirudi nyumbani kwao alifika na kuingia chumbani kwake moja kwa
moja bila hata kumsemesha mama yake aliyekuwa ameketi sebuleni.
Maisha ya Meshakin yalibadilika
sana akawa ni mtu wa mawazo hali iliyomfanya hata kushindwa kutafuta
kazi akawa ni mtu wa kulala muda wote , mama yake alikuwa akimuuliza
kila siku kitu kinachomsumbua lakini Meshaki hakutaka kuwa muwazi kwa
mama yake, siku moja mama Meshaki alikwenda kumtembelea Joyce nyumbani
kwake, aliingia ndani moja kwa moja bila hodi alimkuta Joyce akilia
machozi huku akiwa na picha ya meshaki,
Joyce alikurupuka na
kuificha picha hiyo na mto wa makochi., mama Meshaki alimuliza
“ vipi mama mbona unatokwa machozi” joyce akiwa amekaa karibu na
mto alipoficha picha ya Meshaki,
Joyce ; “hapana mama
niko sawa” mama
Meshaki “kweli
mwanangu”
Joyce; “ndio mama”.
Mama Meshaki alimuomba
Joyce kumletea maji ya kunywa.
Joyce aliingia ndani
ili kumletea mama Meshaki lakini akiwa anataka kuinuka kitini aliudondosha
mto na picha ya Meshaki ilianguka , yeye hakujua hivyo alifata maji
lakini mama Meshaki aliona picha ile na kuiangalia huku akijiuliza kichwani,
Joyce alipokuwa anarudi
alimkuta mama Meshaki akiangalia picha hiyo,
joyce alishtuka sana,
mama Meshaki ; “ Meshaki
picha hii alipendeza sana”
Joyce; “ni kweli
mama”.
Mama Meshaki alimletea
Joyce chakula kama zawadi,
Joyce naye alishukuru
sana baadaye mama meshaki alimuaga joyce na kurudi nyumbani kwake.
BAADA YA MWEZI MMOJA
Joyce akiwa nyumbani
kwake alipokea simu kutoka kwa rafiki yake aliyekuwa anafanya kazi katika
shirika la kusaidia watoto yatima akimtaka kwenda ofisini kwake ili
kupeleka vyeti vyake vya elimu maana kulikuwa na nafasi ya kazi ilikuwa
imotolewa haraka haraka joyce anajiandaa na kwenda katika ofisi ile
alikutana na rafiki yake huyo na kumpatia vyeti vyake , katika hali
ya ya kushangaza meshaki naye alifika katika sehemu hiyo hiyo
naye alileta vyeti vyake kwa rafiki yake,
Joyce na Meshaki waliambiwa
wasubiri nje ili vyeti vyao vikaguliwe, wakiwa katika mabenchi wakisubiria
majibu meshaki alimsemesha Joyce,
Meshaki; “ vipi mbona
kimya kimya hatuambiani?”,
joyce; “ nikwambie
wewe kama nani” kauli hiyo ilionyesha kumvunja moyo Meshaki huku akibaki
akimuangalia tu Joyce.
Majibu yaliletwa wote
wamefaulu hivyo wakatakiwa kurudi kesho yake ili wapangiwe sehemu za
kufanyia kazi, wote kwa pamoja walirudi nyumbani. Siku iliyofuata walifika
katika ofisi ile ili wapangiwe sehemu za kufanyia kazi, Meshaki alipangwa
kufanyia Dar es salaam Tanzania na Joyce alipangiwa kufanyia kampala
Uganda, hivyo kila mmoja alirudi tayari kwa kwenda kujiandaa na safari
maana walipewa siku tatu za maandalizi, meshaki alirudi na kumpa taarifa
mama yake huku Joyce naye akimpa taarifa mama Meshaki, mama alifurahi
sana.
BAADA YA SIKU TATU
Mama Meshaki akiwa na
Meshaki uwanja wa ndege wakijiandaa kuondoka huku Joyce naye akiwa hapo
hapo naye akisubiri ndege ya kwenda Uganda. Ilikuwa ndege ya kwanza
ya meshaki na mama yake kufika hivyo waliondoka mama Meshaki akiwa ametangulia
alimuacha Meshaki nyuma akizungumza na Joyce,
Meshaki alisema neno
moja “ nakupenda” na aliondoka.
Joyce alikuwa akitokwa
machozi muda ulifika naye aliondoka.
ITAENDELEA KIPINDI KIJACHO USIKOSE....................
Maoni
Chapisha Maoni