KWANINI HUFANIKIWI,SOMA HAPA


KWA NINI HATUFANIKIWI?
Hili ni swali ambalo baadhi ya watanzania

wenzangu hujiuliza kila siku pasipo kupata

jibu lililo sahihi hasa baada ya kufanya kazi

kwa muda mrefu pasipo hata kuona dalili za

mafanikio na kubaki tukiwangalia wenzetu

wakipiga hatua kila siku.

Baada ya kuona mafanikio kwa wenzetu sisi

hukaa na kuanza kujadili mali za mtu huyo

alipozipata,badala ya kukaa na kujiuliza wapi

tumekosea na nini tufanye na kwa nini huyu

afanikiwe sisi tusifanikiwe wakati wote ni sawa

na tumeletwa chini ya jua?

Sikatai kwamba si kila mtu aliyefanikiwa katika

dunia hii basi amepata mali hizo kihalali,ukweli

ni kwamba mafanikio yanaweza kupatikana

kwa njia nyingi tofauti mfano wapo ambao

huua,wengine kudhurumu,wengine kufanya

matukio ya ujambazi,wengine kujiunga na

makundi ya kishetani,hapo napo mafanikio

huwepo lakini mara nyingi mafaniko yao huwa

ni muda mfupi yaani hayadumu.

Leo ni meamua kundika makala hii

nikitaka kuzungumzia mafanikio ambayo

hutokana na bidii na jitihada za mtu mmoja

mmoja,mafanikio ambayo hutolewa na

mungu,sasa basi ni kwa nini tulio wengi

hushindwa kufikia mafanikio ambayo

mungu ametupa? Ndio mada kuu yangu

ya leo na sio mafanikio ambayo tumetoka

kuyatazama ,mafanikio ya muda.

Sasa basi fahamu mambo ambayo tulio wengi

hushidwa kufikia mafanikio yetu.

1.KUJIDHARAU

Hili ni jambo kubwa ambalo limekuwa

likikwamisha kufikia mafanikio na malengo tuliyo

jiwekea,leo kuna majina ambayo watanzania

tulio wengi hupenda kuya tumia kulingana

na maisha tuishio ambayo mimi binafsi

siyapendi,majina kama walala hoi,wasaka

tonge na mengine mengi,nakumbuka nilipo

kuwa shuleni mwalimu wangu mmoja aliwahi

kuniambia kuwa neno lolote unalo litamka

kutoka kinywani mwako linajenga na linaumba

uhalisia wa wewe unavyotaka kuwa.

Sasa sisi hujiita tu pasipo kujiuliza nini maana

ya tunachokisema,utakuta na kijana wa marika

kama yangu naye akijiita majina kama hayo,ni

bora kwa mzee lakini kwa kijana ambaye

anauchungu na mafanikio hawezi akajiita

hivyo kwani yeye ndiye nguvu katika jamii

inayomzunguka.

Kabila la kichaga kwa namna moja au nyingine

naweza kusema kama kidogo kama wameanza

kuelewa nini maana ya kutamka majina japo

nao sina uhakika sana kama wanajua kwa

undani zaidi katika kujiita majina,hujiita [bosi]

hata wakiwa wanasalimiana.

Unajua kujiita neno kama hilo kuna faida

zake,faida yake ya kwanza kujiita neno kama

hilo bosi hata kama huna sifa za hilo jina lakini

utapata nguvu ya kutafuta pesa kwani hutotaka

uitwe jina hilo wakati huna kitu,unapanua

uwezo wa kufikiri kwani utakuwa ukiwaza levo

za juu za mafanikio,utataka kujiona wewe ni

tofauti na wengine hivyo utapata nguvu mpya

ya kutafuta ili uweze kuendana na jina hilo.

Je tunapo jiita majina kama walala hoi nini

kinatokea? Hushidwa kufikiria mafanikio

katika levo za juu daima utafikiria kulingana na

jina ulivyojiita,mwenendo wako wa utafutaji

utakuwa ni wakilala hoi yaani unarizika hata

kama ni kidogo sana,utapunguza uwezo wa

kufikiria hata kama ukijalibu kuwaza kikubwa

hutakuwa na nguvu kiasi hicho cha kufikia

malengo yako.

Badala ya kujiita majina hayo ya kilala hoi sasa

tunapaswa kubadilika kujiita majina mazuri

yatakayosaidia kufanya mafanikio yetu kufika

kwa wakati na hatimaye kufikia malengo.

2.KUDHUBUTU NA KUTOJIAMINI KUWA

TUNAWEZA.


Mungu katika kutuumba alitupa vitu vya ziada

kila mmoja katika kichwa chake ambacho

anaweza kukifanya,halafu sasa Mungu

alivyo waajabu akutapa vitu ambavyo si

kila mtu anaweza kuvifanya,kila mtu kwa

upendeleo,mwingine akapewa kipawa cha

kuimba,mwingine kutangaza,mwingine

kuigiza,mwingine kucheza mpila,ambavyo si kila

mtu anaweza kuvifanya hivyo.

Cha kufulahisha zaidi katika nchi ambayo

mungu ametupa upendeleo wa kuwa na vipawa

vingi Tanzania ni moja wapo,kuna vipaji vya

kila aina kama nilivyotangulia kuviorodhesha

baadhi hapo mwanzo,lakini shida inakuja pale

katika kuvionesha na ndio sababu kuu ya sisi

kutofanikiwa.

Uoga kwamba labda watu watanicheka

nikionesha kipaji changu cha kucheza muziki au

jamii itanichukuliaje,maswali kama hayo ndiyo

yanayozuia udhubutu kwa watu na kusababisha

kutojiamini hatima yake ni kuendelea kushidwa

kufikia malengo.

Hakuna kitu cha msingi kama kweli unataka

kufanikiwa maishani kama kudhubutu na

kujiamini hii ndio silaa kubwa iliyotumiwa na

watu ambao ni maarufu kwa sasa katika Nyanja

zozote za maendeleo,hebu sasa tubadillike

na tujione tunaweza japo katika mafanikio

yoyote changamoto haziwezi kukwepeka

zipo zitakazo kukatisha tamaa lakini wewe

usiogope,dhubutu,jiamini songa mbele.
USIKOSE KUSOMA KIPINDIKIJACHO....................

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4