KWANINI HUFANIKIWI
Endelea na kupata elimu huru bila malipo hapa baada ya kuangalia hatua mbili wiki iliyopita leo tunaendelea hapa.
3.UTOAJI
Tunashidwa kufanikiwa kwasababu bado hatujajua nini maana ya utoaji,katika
jambo ambalo linaonekana ni kawaida kwa baadhi ya watu ni kutoa,pasipo
kujua katika kutoa kuna kitu ambacho kipo kimejifisha ambacho ndipo
mafanikio yetu yalipo,utoaji wa mazoea kwa sisi watu ndipo tatizo
lilipo.
Mtu anatoa pasipo kujua anatoa kwa kwa minajili ipi, na katika kutoa
kuna utoaji wa aina nyingi ambapo sidhani kama wote tutakuwa tunafahamu,
je ?ni pesa pekee ndio utoaji? leo nataka kukupa aina nyingine kabisa
za kutoa mbali na hiyo tuliyo izoea.
Kutoa muda kwa ajili ya kufanikisha jambo Fulani muhimu,kutoa elimu
uliyonayo kwa ajili ya kuisaidia jamii,kutumia vipaji vyetu kama sanaa
ya uigizaji,uimbaji,uchoraji na sanaa zingine ambazo zinalenga kubadilisha
mtazamo kwa jamii kwa mtazamo chanya,hata kutoa njia ambazo zimekuwezesha
wewe kufanikiwa napo pia ni utoaji,kwa kifupi hizo ndio aina za utoaji
kama ulikuwa hujafahamu bado.
Haijalishi unatoa kikubwa kiasi gani lakini kama bado hujajua kanuni
za utoaji bado hautakuwa umefanya jambo badala yake utakuwa ukiongeza
matatizo,tunapotoa tujifunze kujisemea kwa natoa ili iweje na sadaka
yako hiyo unahitaji mungu atufanyie kitu gani,kwa kufanya hivyo hakika
tutafungua milango ya mafanikio yetu.
4.KUTOKUWA NA MFANO WA MTU UNAYE TAKA KUWA KAMA YEYE[ROLE MODAL].
Unajua tulio wengi bado hatuoni nini maana ya kuwa na mtu unayetaka
kuwa kama yeye katika sehemu wewe ulipo na hichi ndicho kinatufanya
kutofanikiwa maisha.
Hakuna kitu cha muhimu kama kuwa na mfano wa mtu unayetaka kuwa,unajua
ni kwasababu gani? Kwanza endapo utakuwa ukimtazama atakuwa anakutia
hamasa ya wewe kufanikiwa kupitia kazi zake ambazo anakuwa akizifanya,iwe
ni katika biashara,sanaa au sehemu yoyote ambayo yeye amefanikiwa kupitia
hapo.
Wakati nikiwa mdogo nilikuwa nikisoma vitabu vya waandishi mbalimbali
ambao walikuwa wakiandika kuhusu jambo la kuwa na mfano wa mtu ambaye
unataka kuwa kama yeye,binafsi sikuwa na elewa alikuwa anamaanisha nini
lakini sasa nimejua nini maana ya kuwa role modal nami nataka nikujuze
kidogo.
Inakujengea uwezo wa kufanya kitu kama yeye alivyofanya japo haitakuwa
kivile lakini utaonesha kitu ambacho kupitia yeye utakuwa unaweza kufanikiwa.
Mimi binafsi mtu ambaye natamani kuwa kama yeye katika uandishi ni
mtummoja anaye itwa Erick Shigongo sio siri ni mtu ambaye naweza kusema
ninafata nyayo zake na ipo siku naamini namimi nitapata kujulikana kupitia
nyayo za Erick Shigongo,hongera kaka kwa kunifanya nipende kazi zako,japo
usikasilike endapo nitakuzidi.
Jamani tujifunze kuishi na mfano wa mtu unayetaka kuwa,tusiishi kwa
mazoea,usiishi wewe kama wewe,naomba niileweke baada ya kuzungumza haya
wapo ndugu zangu wengine watafikiri hata kumuiga mtu ambaye anafanya
vitendo viovu napo utafanikiwa laahasha sanasana utaambulia kwenda jela
au kupoteza maisha kabisa,tufate vitu ambavyo vinaweza kutuletea maendeleo
tu na sio vingenevyo.
5.KURIDHIKA NA HALI ULIO NAYO.
Katika hili wapo wengi watajiuliza,hee huyu jamaa vipi,wakati tunaambiwa
na vitabu vya dini kuwa turidhike na tulivyo navyo? Sasa mimi leo nitakwenda
kinyume na maandiko hayo,sio kwamba na dharau neno la mungu hapana,ila
nikatika kuwekana sawa kifkra.
Wenda usemi huu ndio unaofanya sisi tushidwe kufanikiwa unajua ni
kwasababu gani? Ni kwasababu watu wanashidwa kufikiria hatua za mbele
zaidi kimaendeleo na badala yake uzembe ujitokeza hatimaye kuukaribisha
umasikini.
Mimi waga najiuliza kwamba,hivi kwanini hawa wafanyabiashara wakubwa
wanazidi kuleta bidhaa mpya sokoni kila uchwao badala ya kuridhika na
mamilioni walionayo, kwanini wasilale tu wakala maisha?
Lakini nikaja kukundua jambo ambalo hawa jamaa hulifanya,unajua ni
kitu gani? Hawa jamaa huogopa sana kufirisika,pamoja na ushindani
sokoni ndio unaowafanya wasilale wabaki wakifikiri jinsi ya kufanya
bidhaa yake kuwa bora zaidi kuliko mwingine.
Na ndio maana huona wakizidi kuongezeka siku hadi siku,leo sisi tunapata
elfu kumi kwa siku tunasema turidhike na tulicho kipata badala ya kuumia
na kuona uchungu na kufikiria jinsi ya kuongeza zaidi,tuna sema turidhike
natukipatacho,ipo haja ya kubadilika sasa na kuwa kama hawa jamaa.
Nadhani kukosekana kwa ushindani baina yetu katika kufanya kazi ndio
chanzo cha sisi kuridhika na tunacho kipata na hivyo kuzidi kujididimiza
katika janga la umasikini.
Inashangaza sana kuona mtu anaishi kwa mjomba,au kwa ndugu yoyote
halafu anaridhika na maisha yapale nyumbani, hili lipo sana kwetu sisi
vijana ambao ndio tunapitia sana katika maisha ya kukaa kwa ndugu pindi
tukiwa tunasoma.
Mimi nadhani tuanze kuona aibu sasa,badala ya kukaa na kuridhika
na maisha ya hapo nyumbani tuamke na kuanza kutafuta vitu vyetu na kuona
hapo ulipo si pako.
Binafsi huwa Napata shida sana hasa ninapokuwa naishi na kwa ndugu,huwa
najiona hapa nilipo sio kwetu wala kwangu,nguvu Fulani huniijia ya kupambana
na maisha ili namie nipate kuwa na kwangu,sehemu ambayo nitalala na
nitajisikia amani,hivi unapo kuwa ukiishi kwa mtu utakuwa na amani kweli?
Hata kama unaishi vizuri lazima tu amani yako ipungue kwa asilimia Fulani.
Tunapaswa kubadilika na kutoridhika na hali ulionayo ili uweze kupata
nguvu ya kuweza kupambana na maisha na hatimaye tuweze kufikia ndoto
na malengo tuliyojiwekea katika maisha,yapo mengi yanayo kwamisha
mafanikio yetu lakini kwa haya machache nina imani utakuwa umejifunza
kitu ambacho kitakuwa msaada katika maisha yako,Hakuna kitu kitakacho
fanikiwa bila ya kumuomba mungu,mungu kwanza halafu mimi halafu wewe
tutafanikiwa.
KUSOMA.
Hili ni jambo ambalo watanzania wengi hushidwa kulifanya pasipo kujua
kuna umuhimu gani katika kusoma maandiko,leo hii mtu yupo radhi kushinda
disko hata siku nzima akicheza muziki lakini ukimpatia kitabu hata cha
hadithi achilia mbali vitabu vingine ambavyo najua ataishia kutazama
picha ya juu tu na kuondoka zake hata kama akisoma basi ataishia ukurasa
wa tano lazima tu, utamuona anasinzia.
Kuna Mwalimu wetu mmoja wa dini alikuwa akitufundisha katika vipindi
vya shule ya jumapili au inavyojulikana kama[ Sunday school] namkumbuka
kwa jina aliitwa Mwinjiristi Jackson,huyu mwalimu bwana alikuwa akituambia
kwamba,kabla hatujaanza kusoma Biblia ni lazima tuombe kwanza kwasababu
shetani huwapiga watu na pepo la usingizi na hivyo kushidwa kusoma neno
ambalo mungu amepata kunena kupitia biblia ili liweze kuwa msaada katika
maisha yetu.
Nadhani pepo hili ndilo linalotushambulia kututesa Watanzania tulio
wengi tushidwe kusoma vitabu ambapo mimi naamini kupitia vitabu tunaweza
kufanikiwa kupitia maandiko yanayo andikwa na wataaramu mbalimbali duniani.
Mwaka jana niliweza kufanya uchunguzi mdogo nikishirikiana na marafiki
zangu wa karibu kwa lengo la kutaka kujua ni marika gani yanayo ongoza
kwa usomaji wa vitabu, naomba kuwataja marafiki zangu hao kwa sababu
ya mchango wao mkubwa walio uonesha,Tumaini na Grace mungu awabariki
sana.
Katika utafiti wetu tulioufanya tuliweza kubaini kuwa asilimia 70
ya watu wanaoongoza kwa usomaji wa vitabu ni wazee na asilimia 30 ni
vijana,kwa kweli inashangaza sana kuona vijana tunakuwa nyuma kiasi
hiki ambapo Dunia inatutegemea katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Lakini hata kama tunakwepa gharama za ununuaji wa vitabu bado vijana
tuna fursa nyingi za kuweza kusoma vitabu na tukaweza kuongeza uwezo
wa kujitambua zaidi.
Hivi sasa Teknolojia inaendelea kukua siku hadi siku sasa unaweza
kuona kila kitu kinacho endelea duniani kwa kupitia simu za mkononi
za kijitali,komputa na vifaa vingine vyenye uwezo wa intanenti,kupia
kwa vifaa vivyo tunaweza kusoma vitabu na tukaongeza mbinu ambazo zinaweza
kutusaidia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha,swali
je? sisi vijana tekonojia hii tunaitumia ipaswavyo?au ndio tunaitumia
kwa kurushiana picha za utupu tu,jibu utakuwa nalo kaa chini utafakari
kasha chukua hatua.
Maoni
Chapisha Maoni