Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2014

CAF yaondoa marufuku ya Gambia

Picha
Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) limeondoa marufuku ya miaka miwili iliyokuwa imeiwekea The Gambia. Kauli hiyo inafuatia uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki na kumchagua aliyekuwa waziri wa michezo Modou Lamin Kabba Bajo kuywa mwenyekiti wake. Kamati kuu ya CAF iliondoa marufuku hiyo kufuatia kutekelezwa kwa masharti yaliyokuwa yamewekewa shirikisho hilo la Gambia. CA Filikuwa imeipiga marufuku Gambia kufuatia udanganyifu wa umri w wachezaji wake . ''Lazima visa vya udanganyifu wa umri wa wachezaji vikome kabisa''barua hiyo ya CAF ilisema. GFF ililazimika kuanza upya baada ya kamati ya dharura ya FIFA kuifutilia mbali uwakilishi wa shirikisho la Gambia GFF ukiongozwa na Mustapha Kebbeh kufuatia kupatikana udanganyifu wa wa umri wa wachezaji. Kamati ya muda iliyoundwa ndiyo iliyoshughulika na maandalizi ya uchaguzi huo. Matukio ya hivi punde yatajadiliwa katika mkutano wa kamati kuu ya FIFA huko Zurich. Kabba Bajo, 50,alitawazwa mshindi baa...

Wolves yamsajili Sagbo kwa mkopo

Picha
Klabu ya Wolves imemsajili mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Yannick Sagbo kwa mkopo kwa kipindi cha miezi mitatu kutoka kwa Hull City. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, aliyezaliwa mjini Marseille Ufaransa, na ambaye anatarajiwa kucheza katika mchuano wa Jumatano, dhidi ya Huddersfield,atachezea Wolves hadi mwezi Januari. Sagbo aliingiza mabao manne alipokuwa anachezea Tigers msimu uliopita, baada ya kuhama kwa kima cha pauni milioni 1.6 kutoka kwa ligi ya daraja ya kwanza nchini Ufaransa. Kocha wa Wolves, Kenny Jackett alisema Sagbo ana uwezo mkubwa na kipawa kucheza vizuri na anaamini kuwa atashirikiana vizuri na wachezaji wengine wa timu. Sagbo, ambaye bado hajacheza katika ligi kuu ya premier msimu huu, alichezea Hull katika ligi ya Uropa na pia katika mezhi ambayo wlaishindwa mabao 3-2 na West Bromwich Albion katika awamu ya tatu ya kombe la ligi. Tulitazama mechi dhidi ya West Brom wiki jana,'' alisema kocha mkuu wa Wolves Kenny Jackett. ...

Aadhibiwa kwa kusujudu uwanjani

Picha
  Mchezaji wa Kansas City Husain Abdullah aadhibiwa kwa kuomba baada ya kufunga bao  Mchezaji wa Kansas City Chiefs Husain Abdullah aliadhibiwa vikali na refarii baa da ya kupiga sijida baada ya kufunga bao katika mchezo wa soka ya Marekani Kansas walipoinyuka New England Patriots 41-14. Refarii alimwadhibu papo hapo Abdullah alipoinuka baada ya kusheherekea kwa kupiga sijida. Aliyekuwa refarii wa zamani wa NFL Mike Pereira alisema kuwa sio hatia mtu kupiga sijida. Tukio hilo linawadia wakati ambapo ligi hiyo inapigwa msasa kufuatia utovu wa nidhamu mbali na tuhuma chungu nzima kuhusiana na wachezaji wa ligi hiyo. Tayari wandani wa NFL wanadai kuwa kuna upendeleo kwani mchezaji mwengine nyota Tim Tebow hakuadhibiwa baada ya kuonesha ishara yake al maarufu “Tebowing” msimu wote wa mwaka wa 2011. Abdullah amejitokeza kutetea dini yake ya Uislamu sawa na vile Tebow huonesha wazi kuwa ni Mkristo. Aidha Abdula alihiji mwaka uliopita alipoambatana na kakake Hamza,k...

Raila Odinga atandikwa kiboko

Picha
Hali ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kwale nchini Kenya, baada ya mwanamume mmoja kwenda ukumbini na kuanza kutandika bakora kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine. Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa wanacheza densi ya kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa jimbo la Kwale Pwani ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa. Walikuwa wameambatana na viongozi wengine, wakiwemo, Seneta Juma Boy, Hassan Omar, Agnes Zani, James Orengo, Johnstone Muthama na wengineo.   Kiongozi wa upinzani Raila Odinga Mwanamume huyo alimshambulia Odinga ambaye ni waziri mkuu wa zamani na kumchapa mara mbili kabla ya kumgeukia gavana wa jimbo hilo na pia kumchapa mara mbili. Hata hivyo mwanamume huyo alishindwa nguvu na walinzi wa Raila Odinga. Polisi walithibitisha kuwa walimkamata mwanamume huyo na kumwachilia baada ya kugundua kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili. Haijulikani kwa nini mwan...

Facebook yapata mpinzani

Picha
Mtandao wa kijamii wa Ello unapokea maombi 31,000 ya watumiaji wanaotaka kujiunga kila saa moja hali ambayo inaibua ushindani mkubwa kwa mtandao wa Facebook. Muanzilishi wa mtandao huo Paul Budnitz ameiambia BBC kuwa wakati mtandao huo unaazishwa ulilenga watu kuhudumia marafiki 90 tu. Mtandao huu kwa mjibu wa muanzilishi umeanzishwa August mwaka huu ukiwa ambapo hauna gharama yoyote kwa mtumiaji iwe matangazo ama kulipia data. Hata hivyo baadhi ya watumiaji wameubatiza kwa jina la Anti-Facebook mtandao huo, wakimaanisha kwamba ndiye mpinzani mkubwa wa Facebook. Baadhi ya wataalam wa masuala ya kimitandao wamekosoa mfumo wa Ello kutotoza gharama yoyote wakidai kuwa katika siku za usoni huenda mtandao wa Ello utalazimika kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa watumiaji wake. Paul Budnitz mtengenezaji wa baiskel za kampuni ya Vermont ameiambia BBC kuwa wapo imara katika ushindani wa kimitandao na kujigamba kuwa ana wataalamu wa kutosha kukabiliana na makampuni pinzania. Ha...

Mwanamke apigwa mawe hadi kufa Somali.

Picha
  Wapiganaji wa Alshabaab  Mwanamke mmoja ameuawa kwa kupigwa mawe nchini Somalia na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab. Ripoti zinasema kuwa takriban watu 200 akiwemo gavana wa eneo hilo walishuhudia watu wakimpiga mawe mwanamke huyo kwenye mji wa Barowe. Mwanamke huyo wa umri wa miaka 30 alikuwa ameshutumiwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa. Wadadisi wanasema kuwa mauaji hayo ini ishara ya ushawishi wa kundi la Al shabaab hata baada ya kushambuliwa na serikali ya Somalia pamoja na vikosi vya muungano wa Afrika. Mji wa Barowe ambao uko umbali wa kiomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu umekuwa ngome ya Al Shabaab.-BBC SWAHILI

Zimbabwe yanyimwa mkopo na IMF

Picha
Nemboya IMF  Hazina ya fedha duniani IMF imesema kuwa haitatoa fedha zaidi kwa serikali ya Zimbabwe kwa kuwa serikali hiyo ina madeni chungu nzima. Kundi la wataalam wa hazina hiyo barani afrika liko mjini Harare kukamilisha mpango wa kuisadia serikali kuimarisha uchumi wake huku maelezo ya mpango huo yakitarajiwa kutolewa wiki ijayo. Naibu mkurugenzi wa hazina hiyo anayesimamia Afrika Domenico Fanniza ,ameiambia BBC kwamba utoaji wa mikopo mipya haupo katika mpango wao kwa sasa.. Bwana Fanizza pia alionyesha wasiwasi wake kuhusu hatua ya serikali kutumia robo tatu ya fedha za kodi kulipa mishahara ya takriban wafanyikazi laki mbili na nusu wa serikali.-bbc swahili

Van Gaal:tuna mlinzi wa kati mmoja tu

Picha
Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal Kocha wa machester United, Louis van Gaal amesema Manchester united ina mlinzi wa kati mmoja tu mwenye uzoefu wakati huu kikosi hicho kinapotarajia kukipiga na west ham katika michuano ya ligi kuu ya England. Marcos Rojo yuko fiti, lakini timu hiyo ina majeruhi kama Chris Smalling ana jeraha la mguu, Phil Jones ana jeraha kwenye, Jonny Evans ana jeraha la kifundo cha mguu na Tyler Blackett hatacheza mchezo huo. Van Gaal analazimika sasa kuchukua wachezaji kwenye kikosi cha vijana ili kuziba mapengo yaliyopo kwenye timu yake.miongoni mwao ni vijana Tom Thorpe na Paddy MacNair ambao wataungana na kikosi cha kwanza cha Manchester United kwa mara ya kwanza.

Kenyatta asita kwenda kikao ICC

Picha
  Kesi dhidi ya Rais Kenyatta bado haijaanza kusikilizwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta,amesema kuwa hawezi kuhudhuria kikao alichoagizwa kuhudhuria na mahakama ya kimataifa ya ICC mwezi ujao kutokana na kazi nyingi aliyonayo. Mahakama hiyo ilimtaka afike mbele yake kujibu madai kuwa serikali yake imekataa kuwasilisha shatakabadhi zinazohitajika na mahakama hiyo katika kesi inayomkabili. Kenyatta kupitia kwa mawakili wake ameitaka mahakama ya ICC kuahirisha kikao hicho. Alikuwa ameamrishwa kufika mbele ya kikao hicho cha siku mbili baada ya upande wa mashitaka kulalamika kuwa rais huyo amekataa kuwasilisha ushahidi mbele ya makahama hiyo. Hata hivyo mawakili wa rais Kenyatta wameitaka mahakama hiyo sasa kumruhusu mteja wao imma ashiriki kikao hicho kupitia video ama skype, au wao wajibu masuali kwa niaba yake. Rais Kenyatta amesema kuwa yeye yuko na shughulio n yingi sana kuweza kuhudhuria kikao hicho mwezi ujao. Amesema kuwa mikutano miwili muhimu ya kiserikali ...

Wembley kuandaa Euro 2020

Picha
Uwanja wa Wembley utakuwa mwenyeji wa nusu fainali ya kombe la Euro2020  Uwanja wa Wembley ulioko Uingereza utakuwa mwenyeji wa nusu fainali ya kombe la Euro2020 Uefa imethibitisha. Wembley pamoja na uwanja ulioko Glasgow Hampden Park na ule ulioko Dublin Aviva zitaandaa mechi 16 na tatu zingine za makundi. Shirikisho la Soka la Uingereza lilipewa uwenyeji wa mechi hiyo baada ya kuishinda shirikisho la Ujerumani. Hata hivyo Shirikisho hilo litapata fursa ya kuandaa mechi kadha za makundi. Haya yalibainika baada ya Uefa kutangaza viwanja 13 vitakavyoandaa mechi za Euro . Mechi za robo fainali na tatu za makundi zitaandaliwa mjini Munich (Ujerumani), Baku (Azerbaijan), Roma (Italia) na St Petersburg (Urusi). Miji mingine itakayoandaa mechi 3 za makundi na moja ya mkondo wa pili ni Copenhagen (Denmark), Bucharest (Romania), Amsterdam (Uholanzi), Bilbao (Uhispania), Budapest (Hungary) na Brussels (Ubeljiji).

Ebola:Amri ya kutotoka nje yatekelezwa

Picha
Serikali ya Sierra imetoa amri ya kutotoka nje kwa siku tatu.  Serikali ya Sierra imetoa amri ya kutotoka nje kwa siku tatu. Lengo la amri hii ni kuhakikisha kuwa kila mtu amekaa nyumbani huku wahudumu wa afya wakiendelea kuwatafuta wagonjwa kwa lengo la kuwaweka karantini ili kuzuia kuenea zaidi kwa Ebola. Hata hivyo, wakosoaji wamesema amri hiyo itaharibu uhusiano kati ya madaktari na wananchi. Nchi ya Sierra Leone ni moja kati ya nchi za Afrika Magharibi zilizoathirika sana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola huku zaidi ya watu 2,600 wakipoteza maisha yao. Alhamisi, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa (UN) lilitangaza kuwa mlipuko huo ni tishio kwa usalama na amani duniani. Baraza hilo liliomba mataifa yote kusadia katika harakati za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola. Serikali inapania kutumia muda huo kuwatibu wagonjwa  Mvua kubwa iliyoshuhudiwa mjini Freetown hapo Alhamisi haikuwazuia maelfu ya wananchi wa Sierra Leone kwenda sokoni na pia katika maduka ya ju...

Museveni amfuta Waziri Mkuu kazi

Picha
  Amama Mbambazi Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemfuta kazi waziri mkuu na mwandani wake Amama Mbabazi. Kwenye taarifa yake Museveni alimshukuru bwana Mbabazi kwa mchango wake kwa nchi ya Uganda ambapo pia alimtangaza mrithi wake Ruhakana Rugunda ambaye sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge. Bwana Mbabazi alikuwa anatarajiwa na wengi kuwa mpinzani wa Museveni katika uchaguzi ujao. Rais Museveni ametangaza kuwa amemteua daktari Ruhakaan Rugunda kama waziri mkuu mpya ambaye ataaanza kushikilia wadhifa wake mara moja.   Mbabzi alikuwa mwandani wa karibu wa Rais Museveni.  Mapema mwaka huu chama kinachotawala kiliidhinisha azimio kikisema kuwa rais Museveni ambaye amekuwa uongozini kwa muda wa miaka 28 atakuwa mgombea wa pekee kwenye uchaguzi wa mwaka 2016. Hata hivyo mkewe Mbabazi ambaye pia ni afisa wa cheo cha juu chamani amesema kuwa mumewe ameonewa. Waziri mkuu mpya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya awali alikuwa amehudumu kama waziri wa afya.- ...

Mijeledi 91 kwa kucheza wimbo wa 'Happy'

Picha
  Washukiwa walisema walihadaiwa kuwa walikuwa wanafanya mtihani wa kuigiza  Watu sita nchini Iran waliokamatwa baada ya kuonekana kwenye kanda ya video iliyokuwa inaiga wimbo wa 'Happy' wake mwanamuziki mashuhuri Pharrell William, wamehukumiwa kifongo cha hadi mwaka mmoja jela kila mmoja pamoja na adhabu ya kuchapwa mijeledi 91. Wakili wa sita hao amesema kuwa hukumu hiyo itaahirishwa kwa miezi sita ikmaanisha kuwa watafungwa tu jela ikiwa watarejelea kosa hilo. Kanda hiyo inaonyesha wanaume watatu na wanawake watatu ambao hawajafunika vichwa vyao wakicheza densi kwenye barabara na katika paa za nyumba mjiniTehran. Kanda hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, imetazamwa na zaidi ya watu milioni moja. Wengi wa waliohusika kuitengeza kanda hiyo, walifungwa kwa miezi sita , huku mmoja wao akifungwa kwa mwaka mmoja, alinukuliwa akisema wakili wao Farshid Rofugaran.   Mmoja wa watu waliokamatwa kwa kucheza densi  Kanda hiyo kwa jina, ...

Saa za gharama zawaponza maafisa FIFA

Picha
Shirikisho la soka la dunia FIFA, limewaambia viongozi wanaounda kamati ya utendaji na viongozi wengine wa juu wa shirikisho hilo kurejesha saa zipatazo 65 za gharama walizopokea kama zawadi kipindi cha kuelekea kombe la dunia huko Brazil mwaka huu. FIFA imesema kitendo cha kurejesha saa hizo ni kutunza nidhamu. Saa hizo zinakadiriwa kuwa na gharama ya dolla elfu ishirini na tano kila moja na zinatakiwa ziudishwe Octoba 24 ,mwaka huu. Saa hizo za kumbukumbu ya Parmigiani ziligawiwa na shirikisho la soka la Brazili (CBF) wakati wa mkutano wa maandalizi wa FIFA uliofanyika mjini Sao Paulo. FIFA imesema kuwa kanuni za maadili zinazuia viongozi kupokea zawadi ambazo zinathamani zaidi au zenye kuonesha ishara fulani. Inasemekana kwamba saa hizo zitatolewa kwa taasisi zinazojitegemea na si sile zinazojali maslahi huko Brazili.-CHANZO BBC SWAHILI

Kamanda mwanamke muasi akamatwa

Picha
Waasi wa CharlesTaylor walikuwa wakiwatumia watoto kama wapigana Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameisifu hatua ya kukamatwa nchini Ubelgiji kwa kamanda mwanamke aliyekuwa katika kikundi cha waasi cha Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor. Kamanda huyo amekamatwa kwa makosa ya jinai aliyoyafanya wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia. Hatua ya kukamatwa kwa kamanda huyo, imekuja baada ya malalamiko kuwasilishwa kwa niaba ya waathiriwa watatu wa vita hivyo, mwaka 1992. Martina Johnson, bado hajatoa jibu lolote kwa madai yaliyowasilishwa mahakamani dhidi yake yakiwemo kuwaua watu kinyama na kuwakatakata vipande Taylor amefungwa jela baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita nchini Siera Leone. Mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa ilimpata na hatia Taylor mwaka 2012 kwa kosa la kusambaza silaha kwa waasi nchini Siera Leone huku naye akipewa madini ya Almasi na waasi hao. Alianzisha uasi nchini Liberia mwaka 1989 na hatimaye kuwa Rais mwaka...

Afrika Kusini yafanya uchunguzi wa fedha kutoka Nigeria.

Picha
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma akiwa na mkewe. katika picha  Serikali ya Afrika kusini inachunguza kugunduliwa kwa dola million 9.3 fedha  taslim ambazo maafisa wa forodha walizipata kwenye mzigo kutoka kwenye ndege binafsi iliyoingia kutoka Nigeria . Ugunduzi huo ulifanyika September 5 kwenye uwanja wa ndege wa Lanseria, kaskazini magharibi mwa Johannesburg, baada hitilafu  kugunduliwa kwenye mizigo ya raia wawili kutoka Nigeria na Mwingine kutoka Israel ambao walikuwa kwenye ndege. Maafisa wa forodha walisema  walizitaifisha  fedha hizo zilizokuwa zimefungwa kwenye mabunda 90 ya takriban dola laki moja kila moja, katika masanduku mawili meusi. Idadi ya fedha anazoruhusiwa abiria Afrika kusini ni takriban dola elfu 2 mia 3. Bado hakuna aliyekamatwa. Baadhi ya ripoti zinaeleza kuwa fedha hizo zilikuwa za ununuzi wa silaha kwa idara ya ujasusi ya Nigeria, na kwamba mmoja wa wanaume kwenye ndege hiyo alikuwa na waraka wa bidhaa zilizot...

''Naimarika zaidi Madrid'': Rodriguez

Picha
  James Rodriguez Wakati Real Madrid leo wakitarajiwa kushuka dimbani dhidi ya Fc Basel James Rodriguez ambaye ni mshindi wa kiatu cha dhahabu katika kombe la dunia mwaka huu amesema kuwa anaendelea kuyazoea maisha ndani ya vijana hao wa Benabeu. Mchezaji huyo raia wa Colombia aliyejiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Monaco, Ufaransa kwa kitita cha pound million 71 ameweza kuwapa matumaini baadhi ya mashabiki kwamba huenda akaendelea kufanya vyema ndani ya klabu hiyo pia. Ari ya mchezaji kufanya vizuri imeonekana bayana kama alivyokaririwa akieleze nia yake ya ndani kufanya vyema,'kila siku nazidi kuimarika kimwili na kiakili''ameeleza mshambuliaji huyo. Rodriguez mwenye umri wa miaka 23, amekuwa ni sehemu ya madrid timu ambayo imeshapoteza mechi zake tatu za mwanzo katika ligi ya Hispania na kuifanya timu hiyo kushika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi hiyo.-BBC

Wanajeshi 12 kunyongwa Nigeria

Picha
Wanajeshi 12 wahukumiwa kifo kwa kukiuka kanuni za jeshi  Hii ni baada ya kumfyatuliwa bunduki afisa mkuu anayeongoza operesheni ya kupambana dhidi ya kundi haramu la kiislamu la Boko Haram kati mji wa Maiduguri,kaskazini Mashariki mwa nchi, mwezi wa Mei. Wanajeshi wengine watano waliachiliwa baada ya ushahidi kukosekana. Wanajeshi hao 12 walipatikana na hatia ya kumfyatulia risasi Jemedari amadu Mohammed. Wanajeshi hao walikasirishwa na kamanda wao ambaye walimlaumu kwa kukataa kuchukua hatua baada ya msafara wao kushambuliwa. Jeshi la Nigeria limeshindwa kuwashinda Boko Haram na wanajeshi wamekuwa wakilalamika kuwa kila wanapokabiliana na wapiganaji wa Boko Haram hawana silaha za kutosha kukabiliana nao. Wote walikana mashtaka hayo katika Mahakama ya kijeshi mjini Abuja. Mahakama ya kijeshi ya watu tisa ilisikiza kuwa tukio hilo lilitendeka baada ya kufyatuliwa kwa risasi kwa afisa mkuu wa kitengocha 7 cha jeshi la Nigeria. Ilimbidi Generali Amadu Mohammed kuj...

Polisi 6 wauawa katika mlipuko Misri

Picha
Polisi 6 wauawa katika mlipuko Sinai  Askari polisi 6 wameuawa katika mlipuko katika rasi ya Sinai Misri wizara ya maswala ya ndani ya Misri imetangaza. Polisi hao waliuawa bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara ilipolipuka msafara wa polisi ukipita. Maafisa wawili zaidi walijeruhiwa vibaya katika tukio hilo. Wanamgambo katika rasi ya Sinai wameendeleza mashambulizi zaidi haswa baada ya kung'olewa mamlakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi mwaka uliopita. Shambulizi hili la leo lilitokea katika barabara ya kutoka mji wa rafah Kuelekea mpaka wa Palestina wa Gaza. Kundi la wapiganji wa Ansar Beit al-Maqdis wanaohusishwa na Al Qaeda ndio waliodai kutekeleza shambulizi hilo. Kundi hilo linadai kulipiza kisasi mauaji ya maelfu ya waislamu waliouawa katika mapinduzi ya Morsi.  

Mathias Chikawe akemea ndoa za utotoni

Picha
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa  Tanzania amepinga vikali tabia ya baadhi ya wazazi ya kuwaozesha watoto wao wakiwa na umri mdogo. Mathias Chikawe amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu huko Kigoma na kuwataka wakimbizi hao kuacha tabia ya kuwaozesha watoto wenye umri mdogo kwa kuwa ni kuwaingiza katika matatizo wakati wa kujifungua. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania amewataka wazazi nchini humo wawape haki watoto wao na kwamba, utamaduni wa kuwaozesha watoto wadogo sio mzuri kwani huwafanya watoto hao kukumbwa na matatizo mengi hasa wakati wa kujifungua. Wakati huo huo imeelezwa kwamba, umasikini na ukosefu wa elimu juu ya ukatili wa kijinsia miongoni mwa wanajamii nchini Tanzania ni miongoni mwa sababu zinazochangia watoto wadogo kukumbana na ndoa za utotoni. Aidha mila potofu na utamaduni mbovu wa baadhi ya makabila nchini humo inaelezwa kuwa sababu nyingine inayochangia tatizo hilo.

Ndege ya kivita ya Nigeria yatoweka katika oparesheni

Picha
Ndege ya kivita ya Nigeria imetoweka katika operesheni dhidi ya wanamgambo wa kitakfiri wa Boko Haram katika eneo lililoathiriwa na machafuko la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Wizara ya Ulinzi ya Nigeria imeeleza kuwa ndege hiyo ya kivita ilitoweka ikiwa na marubani wawili. Msemaji wa jeshi la Nigeria Meja Jenerali Chris Olukolade amesema kuwa ndege hiyo iliyotengenezwa Ujerumani, Ijumaa iliyopita  iliondoka katika kituo cha kijeshi cha Yola makao makuu ya jimbo la Adamawa kwa ajili ya operesheni ya dakika 75. Amesema tangu siku hiyo mawasiliano na ndege hiyo yamekatika. Jeshi la Nigeria limekuwa likitumia ndege za kivita kuyashambulia maeneo ya wanamgambo wa Boko Haram. Msemaji wa jeshi la Nigeria ameongeza kuwa juhudi za kuwasiliana na marubani wawili wa ndege iliyotoweka bado zinaendelea.

Ajuza amfundisha adabu jambazi

Picha
  Mtaa wa Whitstable, Kent  Ajuza mwenye umri wa miaka 80 alimpiga mwizi usoni mwake nchini Uingereza na kumuogopesha kiasi cha kutoroka. Mwanamke huyo, alikuwa anamtembeza Mbwa wake katika mtaa wa Whitstable, Kent, wakati jambazi huyo alipomvamia. Alikuwa amevalia mavazi meusi yaliyokuwa yamefunuika kichwa chake. Alipigana na jambazi huyo na kumgonga kinywani. Polisi mjini Kent wanasema kuwa wangali wanamsaka jambazi huyo. Afisaa mkuu wa polisi katika eneo hilo alinukuliwa akisema: ''Inaonekana mshukiwa huyo alimlenga mtu asiye wa kiwango chake.'' Shambulizi hilo lilifanyika wakati wa usiku Afisa mkuu wa polisi pia amewataka wakazi wa eneo hilo kutoa habari kuhusu tukio hilo. "je unamfahamu mtu yeyote ambaye alikuwa nje wakati wa usiku wakati ajuza huyo alipovamiwa na kurejea nyumbani akiwa na jereha kinywani? Tafadhali tunawaomba mtusaidie na uchunguzi wa kisa hiki,'' aliongeza kusema afisaa huyo.- Chanzo BBC swahili

Polisi wanasa vilipuzi Uganda

Picha
  Polisi Uganda wamewakamata washukiwa 19 wa Alshabab  Polisi nchini Uganda wanasema kuwa wamekamata kiasi kikubwa cha vilipuzi walipokuwa wakifanya operesheni ya kutibua jaribio la shambulizi la kigaidi la wanamgambo wa al-Shabab. Hadi sasa, watu kumi na tisa wamekamatwa na polisi na wanahojiwa kuhusiana na nia yao kutekeleza vitendo vya kigaidi, kulingana na msemaji wa polisi. Wiki iliyopita, ubalozi ya Marekani mjini Kampala ulionya kuwa kulikuwa na uwezekano wa shambulizi la kulipiza kisasi mauaji wa kiongozi wa kundi hilo la Al-Shabab. Uganda inalaumiwa kwa kutuma majeshi yake kupigana chini ya Umoja wa Afrika Amisom.   Polisi Uganda wamewakamata washukiwa 19 wa Alshabab  Marekani ilitangaza kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Alshabab Ahmed Abdi Godane baada ya shambulizi la angani Septemba 2 . Serikali inasema kuwa kundi hilo la kigaidi lilikuwa limepanga kushambuliz mji mkuu wa Kampala. Askari walisema kuwa kundi hilo lilikuwa limepanga kufanya ...

Bwana harusi aaga akienda harusini

Picha
Bwana Harusi azama baada ya mafuriko kusomba boti lao  Takriban watu 17 akiwemo bwana harusi na watoto wawili wamekufa maji baada ya boti ya uokoaji iliyokuwa imewabeba wageni kwenda kwa sherehe ya harusi kuzama katika mafuriko nchini Pakistan. Maafisa wanasema kuwa takriban watu 22 wameokolewa huku waokoaji wakiwatafuta watu zaidi. Msemaji wa shirika la kukabiliana na majanga amesema kuwa zaidi ya watu millioni 2 nchini humo waliathiriwa na mafuriko hayo ambayo yalisababishwa na mvua kubwa. Maafisa wanasema kuwa takriban watu 289 wamefariki katika mafuriko hayo nchini Pakistan kufikia sasa. Zahid Ali mwenye umri wa miaka 27,mchumba wake Mashal pamoja na wageni walikuwa katika boti hiyo iliyokuwa ikielekea katika sherehe za kundeleza harusi yao. Maafisa wanasema kuwa boti hiyo iliojaa kupitia kiasi ilikuwa ikivuka mto Chenab uliofurika katikati ya mji wa Punjab eneo lililoathirika vibaya na mafuriko nchini Pakistan. Msemaji wa huduma ya uokozi katika eneo hilo la...

Libya yamfuta kazi Gavana wa Benki Kuu

Picha
  Jengo la Banki Kuu ya Libya Bunge jipya la Libya lililochaguliwa limemfuta kazi Gavana wa Benki Kuu ya nchi hiyo. Wabunge 94 kati ya 102 wa Libya wamepiga kura wakiunga mkono kufukuzwa kazi Sadik al Kabiir baada ya gavana huyo kujaribu kuzuia fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya wabunge. Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Libya Ali al Hibri ndiye atakayekaimu nafasi iliyoachwa wazi hadi pale gavana mpya atakapoteuliwa. Libya imekuwa katika machafuko makubwa tangu baada ya kupinduliwa  kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi katika mapinduzi ya wananchi ya mwezi Oktoba mwaka 2011. Makundi hasimu ya wanamgambo yamekuwa yakipigana vikali katika miji kadhaa ya nchi hiyo hususan Tripoli ambako yalikuwa yakigombea udhibiti uwanja wa ndege wa kimataifa wa mji huo. Bunge jipya la Libya tarehe 14 mwezi uliopita liliuomba Umoja wa Mataifa utume majeshi nchini humo ili kuwalinda raia.

Boko Harama wazingira Maiduguri

Picha
  Jeshi linakabiliwa na hali ngumu kudhibiti wapiganaji wa Boko Haram Wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram wameuzingira mji wa Maiduguri , mji rasmi wa jimbo la Borno Kaskazini Mashariki ya Nigeria. Wazee wa vijiji wametahadharisha kuwa jeshi linahitaji kuweka ulinzi thabiditi katika mji huo ambao una zaidi ya watu milioni 2 ili kuzuia mashambulizi kutoka pande zote za mji huo. Kundi hilo limeteka sehemu kadhaa ambazo ziko umbali wa kilomita 50 kutoka Maiduguri. Kadhalika kundi hilo lilitangaza maeneo iliyoyateka kama himaya zao. Serikali haijatoa tamko lolote kuhusu taarifa iliyotolewa na wapiganaji hao. Kwingineko wakaazi wa miji iliyozungukwa na Boko Haram Kaskazini Mashariki ya Nigeria, wameelezea hatari kubwa inayowakabili wakati wamejipata katikati mwa makabiliano kati ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo hao. Baadhi waliokwama katika maeneo yenye milima wamelazimika kula majani kama chakula. Kwa siku kadhaa sasa jeshi limekuwa likijaribu kuwasamabarati...

Mahakama:Pistorius hakukusudia kuua

Picha
Pistorius amekana kumuua mpenzi wake kwa maksudi  Jaji anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius, amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp. Hata hivyo jaji huyo Thokozile Masipa amepinga ushahidi wa upande wa utetezi kwamba mwanariadha huyo hakunuia kutenda uhalifu alipomuua mpenzi wake Reeva. Pistorius alikiri kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwaka jana lakini amekana kumuua kwa maksudi , akisema alidhani kuwa mwizi alikuwa amevamia nyumba yake. Upande wa mshitaka unasisitiza kuwa Pistorius alimuua Reeva kwa maksudi,baada ya wapenzi hao wawili kutofautiana. Mandishi wa BBC anasema kuwa jaji Thokozile Masipa heunda akachukua hadi Ijumaa kumaliza uamuzi wake. Pia atakuwa anaangalia kwa makini ukweli wa mashahidi waliotoa ushaidi wao katika kesi hiyo akiwemo Pistorius mwenyewe. Pistorius huenda akafungwa jela miaka 2...

Cheka kidogo hapa Jambo na Vijambo

Picha

Ebola yatishia utaifa wa Liberia

Picha
  Liberia inasemekana kuwa na changamoto za miundo mbinu kuweza kukabiliana na Ebola Liberia inakabiliwa na tisho kubwa kwa utaifa wake huku janga la Ebola likiendelea kuenea kwa kasi kubwa nchini humo. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya waziri wa ulinzi nchini humo. Brownie Samukai aliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kwamba juhudi za kimataifa za kupambana na ugonjwa huo hazina tija. Shirika la afya duniani, limeonya kuwa maelefu ya visa vingine vya maambukizi huenda vikatokea nchini humo. Nchi hiyo imeathirika zaidi kutokana na Ebola kuliko taifa lengine lolote kanda ya Afrika Magharibi. Takriban watu 2,288 wamefariki kutokana na Ebola nchini Liberia, Guinea na Sierra Leone. Shirika la afya duniani linasema kuwa nusu ya vifo vilivyotokana na Ebola vilitokea wiki tatu zilizopita. Nchini Nigeria, watu wanane wamefariki kati ya 21 walioambukizwa ugonjwa huo. Nako nchini Senegal, mtu pekee ambaye alitambulika kuwa na ugonjwa huo ametibiwa na kupona. Hii ni kwa...

Manchester united yapata hasara

Picha
  Manchester United  Manchester United imerepoti kupata hasara kubwa ya kipato chake cha kila mwaka licha ya kuonesha faida nzuri wakati wa uongozi wa David Moyes kama maneja. Klabu hiyo ya Uingereza, inasema kuwa kipato chake cha kila mwaka kilishuka kwa asilimia 84, ilihali faida yake iliongezeka kwa zaidi ya asilimia ishirini. Inasema kuwa inatarajia kipato chake cha mwaka 2015 kushuka, kutokana na kuzidi kuandikisha matokeo mabaya, hasa katika mashindano ya ligi kuu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20. Aidha, matokeo hayo pia yanaonesha kuwa Moyes na wafanyakazi wake walipata jumla ya Dola milioni nane kama malipo ya kuachishwa kazi mapema mwaka huu baada ya kuwa ofisini kwa chini ya mwaka mmoja

Rais Jonathan - mabango yang'olewe

Picha
  Harakati za kampeni nchini Nigeria Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameamuru mabango ya hekeheka za uchaguzi yenye nembo ya kauli mbiu ya 'Bring Back Jonathan 2015' yang'olewe mara moja. Mabango hayo yamelaaniwa vikali kwenye mitandao ya kijamii kwani yanaonekana kuiga kauli mbiu iliyotumiwa katika kampeini ya kuitaka serikali kuwaokoa wasichana waliotekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram mwezi Aprili mwaka huu. Kundi hilo la wapiganaji wa kiisilamu bado linawashikilia wasichana hao, Wakati ambapo mabango ya Bring Back Jonathan 2015 yaliowekwa kando ya barabara kuu mjini Abuja, yalilaaniwan vikali nchini Nigeria na kimataifa kupitia katika mitandao ya kijamii. Watu walihisi kuwa ilikuwa ni kama kejeli kwa kampeini ya 'Bring Back Our Girls' ambayo ilienea kote duniani baada ya Boko Haram kuwateka nyara wasichana wa shule ya Chibok. Wasichana hao 219, bado hawajulikani waliko miezi mitano baada ya kutekwa kwao. Rais Jonathan, ameyataka mabango ...

Baba aua watoto watano-Marekani

Picha
Timothy baba wa watoto watano,aliowatoa uhai. Mwanamume mmoja raia wa Marekani anashukiwa kuwaua watoto wake watano na kuwatupa katika jimbo jingine, hii ni kwa muujibu wa polisi nchini humo. Timothy Ray Jones anakabiliwa na mashtaka kadhaa katika jimbo ambalo ndio makazi yake la Carolina ya kusini,kufuatia shutuma hizo na alikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita huko Mississippi . Watoto hao watano waliopoteza uhai kwa kuuawa na baba yao walikua na umri wa kuanzia mwaka mmoja hadi miaka nane inaelezwa watoto hao watano walipotea katika mazingira ya kutatanisha , mama wa watoto hao aliporipoti polisi baada ya mawasiliano kati yake na mzazi mwenziwe kukatika. Maafisa hao wa polisi walipofanya uchunguzi wao waligundua miili ya watoto hao imezikwa karibu na mji wa Alabama karibu na barabara kuu baada ya kuwasaka watoto hao kwa siku nzima . Jones alisimamishwa katika kizuizi cha barabarani na kushukiwa kua alikua akiendesha gari baada ya kutumia dawa za kulevya ,imethibi...

Tembo amuua mlinzi wake Marekani

Picha
Polisi walisema Tembo huyu alimkanyaga mlinzi wake kwa bahati mbaya kifuani  Polisi nchi Marekani wametoa taarifa za kumhusu mwanzilishi wa kituo cha maonyesho na mtunza Tembo kutoka nchini Marekani ambaye pia ni mmiliki wa nyumba ya matumaini kwa Tembo,amefariki dunia baada ya Tembo aliyekua akimhifadhi kumkanyaga kwa bahati mbaya. Vetenari James Laurita, aliyekuwa na umri wa miaka 56, alianguka alipokua katika kituo hicho cha matumaini kwa Tembo waliotelekezwa na kupoteza maisha yake alipokanyagwa na Tembo mmoja. Mapema wiki hii Laurita alikutwa akiwa hajiwezi katika kituo hicho yapata maili 87 sawa na kilomita 140 Kaskazini Mashariki ya Porland. Inaelezwa kua alianguka kwa kichwa chake katika zege la kituo hicho na baada ya kunaswa, Tembo akamkanyaga kifuani kwa bahati mbaya. ''Tembo aliyemkanyaga hakuwa na hasira ,ilikua ni ajali kama ajali zingine,'' anaeleza bwana Mark Belserene wa kituo cha uchunguzi wa afya. Inaelezwa kua baada ya uchunguzi ...

Wafungwa wapigwa risasi mahakamani

Picha
Visa vya ufyatulianaji wa risasi mahakamani nchini Afrika Kusini vimekuwa vikiongezeka  Wafungwa wawili wamepigwa risasi walipokuwa wakijaribu kutoroka kutoka katika mahakama moja nchini Afrika Kusini. Afisa mmoja kutoka wizara ya sheria aliambia chama cha wanahabari nchini humo kwamba wafungwa waliokuwa wanasubiri kusikilizwa kwa kesi yao waliokota silaha kutoka kwenye jaa la taka. Inaarifiwa wafungwa hao walianza kufyatuliana risasi na maafisa wa polisi. Tukio hilo lilitokea katika mahakama kuu mtaa wa Mthatha katika mkoa wa Eastern Cape. Mthunzi Mhaga, ambaye ni waziri wa sheria, alisema kuwa mfungwa mmoja alijeruhiwa mguuni wakati wa ufyatulianaji risasi. ''Walijaribu kutoroka walipoingia ndani ya majengo ya mahakama , '' alisema bwana Mhaga. ''Baada ya kuipata bunduki, walianza kufyatuliana risasi na maafisa wa polisi, '' aliongeza kusema bwana Mhaga. Alisema kuwa polisi waliweza kudhibiti hali. Kufuatia visa vya hivi karibuni vya ufya...

Marin Cilic bingwa US Open

Picha
  Marin Cilic aibuka bingwa Marin Cilic wa Croatia ameibuka bingwa wa US Open kwa kumfunga Kei Nishikori wa Japan Mpambano huo umechezwa katika uwanja wa Arthur Ashe Mjini New York Marekani. Cilic amepokea kombe la michuano ya tennis upande wa wanaume kwa mara ya kwanza baada ya kumshindilia mpinzani wake seti tatu za 6-3, 6-3 , 6-3. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya fainali za US Open ambapo mchezo wa mwisho unawakosa mmoja kati ya wachezaji wakali akiwemo Andy Murray, Novak Djokovic ama Roger Federer. Cilic anakuwa Mkroatia wa kwanza kutwa ubingwa wa moja kati ya mashindano makubwa manne ya tenis duniani tangu kocha wake Goran Ivanisevic abebe ubingwa wa Wimbledon mwaka 2001.

Bunge la Iraq laidhinisha serikali mpya

Picha
  Wabunge wa Iraq  Bunge la Iraq limeidhinisha serikali mpya itakayoshirikisha makundi muhimu nchini humo. Serikali hiyo inaongozwa na Waziri Mkuu Haidar al Abadi, huenda ikasababisha nchi hiyo kuondokana na makundi ya wapiganaji wanaotishia usalama wa nchi, endapo kutakuwa na kuaminiana miongoni mwa wananchi. Hata hivyo hakuna Waziri wa ulinzi wala wa mambo ya ndani ya nchi aliyetangazwa mpaka sasa. Lakini Waziri mkuu wa nchi hiyo amesema atafanya uteuzi wa mawaziri hao kwa muda wa wiki moja. Nafasi nyingine za mawaziri zimejazwa kwa mujibu wa makubaliano kati ya Washia walio wengi, Wasunni na Wakurd. Serikali hiyo imeonekana ni muhimu katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa kundi la Islamic State.-bbc swahili

Tuhuma za ubakaji dhidi ya AU

Picha
  Baadhi ya nchi ambazo wanajeshi wake wametuhumiwa zimekanusha madai hayo Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa ripoti kuhusu udhalilishwaji wa kijinsia wanaofanyiwa wanawake nchini Somalia na askari wa kulinda amani nchini humo. Majeshi hayo yamo nchini Somalia yakiwakilisha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kupambana na wapiganaji wa kikundi cha Kiislam cha Al Shaabab. Shirika hilo la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema liliwahoji wanawake 21, wakiwemo wasichana waliobakwa na wanajeshi hao mwaka 2013. Visa vingi vimeripotiwa katika kambi zinazosimamiwa na wanajeshi wa Burundi na Uganda. Walinda amani wa Muungano wa Afrika wamedaiwa katika ripoti hiyo, kutumia chakula cha misaada kushawishi wasichana na wanawake kufanya mapenzi nao. Wanajeshi hao wanadaiwa pia kuwabaka ama kuwadhalilisha kingono wanawake waliofika katika kambi hizo kuomba msaada wa matibabu au maji.

EURO 2015: England yaichapa Uswisi

Picha
  England yaifunga Uswisi, Welbeck ang'ara England imeanza kusaka tiketi ya kucheza fainali za kombe la Ulaya kwa kuifunga Uswisi. England imeanza harakati hizo za kucheza fainali hizo zitakazofanyika huko Ufaransa baada ya kuishindilia Uswisi mabao 2-0 usiku wa kuamkia leo. Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck, aliibuka nyota wa kocha Roy Hodgson kwa kazi nzuri ya kutumbukiza kimiani mabao yote mawili, huku akifunga bao la pili dakika ya mwisho ya mchezo huo uliopigwa mjini Basel Uswisi.

Nyama ya Kiboko yawaletea maafa

Picha
  Nyama ya Kiboko huliwa na watu wengi  Watu kumi walikanyagwa na gari lililokuwa linakwenda kwa mwendo wa kasi walipokuwa wanajaribu kujipatia angalau kipande cha nyama ya Kiboko mwishoni mwa wiki. Taarifa hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation. Kiboko huyo alikuwa amegongwa na gari na kufariki Jumamosi jioni katika mkoa wa Limpopo wakati ambapo wanakijiji walikimbia katika sehemu hiyo angalau kujipatia kipande cha nyama. Msemaji wa polisi aliambia shirika la habari la AFP kwamba mnyama huyo aligongwa na wanakijiji wakaona fursa ya nyama ya bure ambapo walikimbia kuinyakua na kuanza kuikatakata, '' ''Hapo ndipo gari lililokuwa linakwenda kwa kasi liliwagonga watu 8 walipokuwa wanakata nyama hiyo na kuwaua,'' aliongeza kusema msemaji huyo wa polisi. Watu wengine wawili walifariki kutokana na majereha yao mabaya wakiwa wanapokea matibabu hospitalini. Polisi wanasema kuwa watu wengine saba akiwemo dereva wa gari hilo wanapokea matibabu hos...

Sudan kusini na tishio la njaa

Picha
Mvua zinakwamisha usambazaji wa misaada S.kusini  Kufuatia zaidi ya miezi minane ya mapigano Sudan Kusini, sasa inakabiliwa na tishio la njaa. Umoja wa Mataifa unasema takriban watu milioni nne wako katika hatari kubwa ya kukosa chakula baada ya wakulima kukosa kupanda msimu huu. Mvua inayonyesha pia imeharibu barabara na kufanya juhudi za kutoa misaada kuwa ngumu zaidi. Wataalam wameonya kuwa baa la njaa huenda likaikumba Sudan Kusini kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Mamilioni ya watu tayari wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula.

Boko Haram wazidisha wasiwasi Nigeria

Picha
Kumekuwa na ongezeko la wasi wasi nchini Nigeria kufuatia hatua ya hivi karibuni ya wanamgambo wa Kiislam wa Boko haram kuteka miji nchini humo. Mamia ya raia wameanza kuukimbia mji wa Maiduguri baada ya wanamgambo hao kuuteka mji wa Bama. Mmoja kati maseneta ameiambia BBC kuwa raia hawaruhusiwi hata kuzika wapendwa wao waliokufa, miili ya waliofariki imetupwa kwenye mitaa na Boko Haram wakiranda randa mitaani. Hata hivyo Serikali ya Nigeria inapinga vikali kuwa jimbo hilo la Bama limeangukia mikononi mwa Boko haram. Mwanamke huyu anasema amelazimishwa kukimbia mji na amepoteza ndugu zake. "Bado sijamwona baba yangu, mume wangu na watoto wangu. Hakuna askari yoyote wa serikali mahali popote. Boko haram wameuteka mji wa Bama. Nimerudi kutoka Bama. Kwa sasa nipo Maiduguri. nilichokiona wakati nilipokuwa nikiondoka Bama ni maiti za watu kila mahali. Wanaume, Wanawake na watoto. Wote...

ICC yaahirisha kesi ya Rais Kenyatta

Picha
Rais Kenyatta anakabiliwa na tuhuma za kufadhili ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007 Kiongozi wa mashitaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC, Fatou Bensouda, ameiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa muda usiojulikan a. Hii ni baada ya malalamiko kutoka kwake kuwa Kenya imekataa kushirikiana na mahakama hiyo katika kuikabidhi ushahidi unahitajika kuendesha kesi kwa hiyo ina maana kuwa hana ushahidi wa kutosha dhidi ya Kenyatta. Katika uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo Fatou Bensouda amesema kuwa hana ushahidi wa kutosha kumfungulia mashitaka Rais Kenyatta ambaye anadaiwa kuhusuika na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2007. Zaidi ya watu 1,000 walifariki katika ghasia hizo. Bensouda amenukuliwa akisema kuwa halitakuwa jambo la busara kufutulia mbali kesi hiyo hasa ikizingatiwa kuwa Kenya haitaki kutoa ushahidi unaohitajika na mahakama hiyo. Badal...