Museveni amfuta Waziri Mkuu kazi
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemfuta kazi waziri mkuu na mwandani wake Amama Mbabazi.
Kwenye
taarifa yake Museveni alimshukuru bwana Mbabazi kwa mchango wake kwa
nchi ya Uganda ambapo pia alimtangaza mrithi wake Ruhakana Rugunda
ambaye sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge.Bwana Mbabazi alikuwa anatarajiwa na wengi kuwa mpinzani wa Museveni katika uchaguzi ujao.
Rais Museveni ametangaza kuwa amemteua daktari Ruhakaan Rugunda kama waziri mkuu mpya ambaye ataaanza kushikilia wadhifa wake mara moja.
Mapema mwaka huu chama kinachotawala kiliidhinisha azimio kikisema kuwa rais Museveni ambaye amekuwa uongozini kwa muda wa miaka 28 atakuwa mgombea wa pekee kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.
Hata hivyo mkewe Mbabazi ambaye pia ni afisa wa cheo cha juu chamani amesema kuwa mumewe ameonewa.
Waziri mkuu mpya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya awali alikuwa amehudumu kama waziri wa afya.-
Maoni
Chapisha Maoni