Ndege ya kivita ya Nigeria yatoweka katika oparesheni
Ndege ya kivita ya Nigeria imetoweka katika operesheni dhidi ya
wanamgambo wa kitakfiri wa Boko Haram katika eneo lililoathiriwa na
machafuko la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Wizara ya Ulinzi ya Nigeria imeeleza kuwa ndege hiyo ya kivita ilitoweka ikiwa na marubani wawili. Msemaji wa jeshi la Nigeria Meja Jenerali Chris Olukolade amesema kuwa ndege hiyo iliyotengenezwa Ujerumani, Ijumaa iliyopita iliondoka katika kituo cha kijeshi cha Yola makao makuu ya jimbo la Adamawa kwa ajili ya operesheni ya dakika 75. Amesema tangu siku hiyo mawasiliano na ndege hiyo yamekatika.
Jeshi la Nigeria limekuwa likitumia ndege za kivita kuyashambulia maeneo ya wanamgambo wa Boko Haram. Msemaji wa jeshi la Nigeria ameongeza kuwa juhudi za kuwasiliana na marubani wawili wa ndege iliyotoweka bado zinaendelea.

Maoni
Chapisha Maoni