Libya yamfuta kazi Gavana wa Benki Kuu

Jengo la Banki Kuu ya Libya 
Jengo la Banki Kuu ya Libya
Bunge jipya la Libya lililochaguliwa limemfuta kazi Gavana wa Benki Kuu ya nchi hiyo. Wabunge 94 kati ya 102 wa Libya wamepiga kura wakiunga mkono kufukuzwa kazi Sadik al Kabiir baada ya gavana huyo kujaribu kuzuia fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya wabunge. Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Libya Ali al Hibri ndiye atakayekaimu nafasi iliyoachwa wazi hadi pale gavana mpya atakapoteuliwa.
Libya imekuwa katika machafuko makubwa tangu baada ya kupinduliwa  kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi katika mapinduzi ya wananchi ya mwezi Oktoba mwaka 2011. Makundi hasimu ya wanamgambo yamekuwa yakipigana vikali katika miji kadhaa ya nchi hiyo hususan Tripoli ambako yalikuwa yakigombea udhibiti uwanja wa ndege wa kimataifa wa mji huo. Bunge jipya la Libya tarehe 14 mwezi uliopita liliuomba Umoja wa Mataifa utume majeshi nchini humo ili kuwalinda raia.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4