Wolves yamsajili Sagbo kwa mkopo
Klabu ya Wolves imemsajili mchezaji
wa kimataifa wa Ivory Coast, Yannick Sagbo kwa mkopo kwa kipindi cha
miezi mitatu kutoka kwa Hull City.
Mshambuliaji huyo mwenye umri
wa miaka 26, aliyezaliwa mjini Marseille Ufaransa, na ambaye anatarajiwa
kucheza katika mchuano wa Jumatano, dhidi ya Huddersfield,atachezea
Wolves hadi mwezi Januari.Sagbo aliingiza mabao manne alipokuwa anachezea Tigers msimu uliopita, baada ya kuhama kwa kima cha pauni milioni 1.6 kutoka kwa ligi ya daraja ya kwanza nchini Ufaransa.
Kocha wa Wolves, Kenny Jackett alisema Sagbo ana uwezo mkubwa na kipawa kucheza vizuri na anaamini kuwa atashirikiana vizuri na wachezaji wengine wa timu.
Sagbo, ambaye bado hajacheza katika ligi kuu ya premier msimu huu, alichezea Hull katika ligi ya Uropa na pia katika mezhi ambayo wlaishindwa mabao 3-2 na West Bromwich Albion katika awamu ya tatu ya kombe la ligi.
Tulitazama mechi dhidi ya West Brom wiki jana,'' alisema kocha mkuu wa Wolves Kenny Jackett. "tulikuwa tunamtafuta mchezaji ambaye yuko tayati kucheza sasa hivi na ambaye yuko sawa.
Wolves walipandishwa daraja hadi mabingwa wa ligi ya kwanza mwezi Mei, kwa sasa wanashikilia nafasi ya
Maoni
Chapisha Maoni