Zimbabwe yanyimwa mkopo na IMF
Hazina ya fedha duniani IMF imesema
kuwa haitatoa fedha zaidi kwa serikali ya Zimbabwe kwa kuwa serikali
hiyo ina madeni chungu nzima.
Kundi la wataalam wa hazina hiyo
barani afrika liko mjini Harare kukamilisha mpango wa kuisadia serikali
kuimarisha uchumi wake huku maelezo ya mpango huo yakitarajiwa kutolewa
wiki ijayo.Naibu mkurugenzi wa hazina hiyo anayesimamia Afrika Domenico Fanniza ,ameiambia BBC kwamba utoaji wa mikopo mipya haupo katika mpango wao kwa sasa..
Bwana Fanizza pia alionyesha wasiwasi wake kuhusu hatua ya serikali kutumia robo tatu ya fedha za kodi kulipa mishahara ya takriban wafanyikazi laki mbili na nusu wa serikali.-bbc swahili
Maoni
Chapisha Maoni