Boko Harama wazingira Maiduguri

 
Jeshi linakabiliwa na hali ngumu kudhibiti wapiganaji wa Boko Haram
Wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram wameuzingira mji wa Maiduguri , mji rasmi wa jimbo la Borno Kaskazini Mashariki ya Nigeria.
Wazee wa vijiji wametahadharisha kuwa jeshi linahitaji kuweka ulinzi thabiditi katika mji huo ambao una zaidi ya watu milioni 2 ili kuzuia mashambulizi kutoka pande zote za mji huo.
Kundi hilo limeteka sehemu kadhaa ambazo ziko umbali wa kilomita 50 kutoka Maiduguri.
Kadhalika kundi hilo lilitangaza maeneo iliyoyateka kama himaya zao.
Serikali haijatoa tamko lolote kuhusu taarifa iliyotolewa na wapiganaji hao.
Kwingineko wakaazi wa miji iliyozungukwa na Boko Haram Kaskazini Mashariki ya Nigeria, wameelezea hatari kubwa inayowakabili wakati wamejipata katikati mwa makabiliano kati ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo hao.

Baadhi waliokwama katika maeneo yenye milima wamelazimika kula majani kama chakula.
Kwa siku kadhaa sasa jeshi limekuwa likijaribu kuwasamabaratisha wapiganaji wa Boko Haram kutoka mji wa Michika - mji ambao ni wa hivi karibuni kudhibitiwa na wanamgambo hao.
Katika mji wa Michika watu wamekwama kati ya mabomu ya jeshi la wanahewa Nigeria na wapiganaji wa jihadi wanaomfyatulia risasi mtu yoyote anayosogea, na kwa mara nyengine hata kuwakata shingo waathiriwa.
Mwanamke mmoja ameiambia BBC kwamba watoto wengi wamekwama nyumbani mwake na hawajui wazazi wao waliko.
Miongoni mwa walioukimbia mji huo na kwenda katika milima iliyo karibu, sasa wameishia kula majani. Mwanamume mmoja amesema watu 7 wamefariki mahali alipojificha, na hawawezi kuzikwa.
Wakati huo huo kundi la viongozi wanaoheshimiwa wanasema Boko Haram wameulenga mji mkubwa Kaskazini mashariki mwa Nigeria, Maiduguri.
Viongozi hao wa Borno wanasema miji na vijiji vilivyouzunguka mji huo tayari vimedhibitiwa na wanamgambo hao.Kundi hilo limeshutumu namna serikali inavyokabiliana na hali.-bbc swahili.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4