Boko Haram wazidisha wasiwasi Nigeria
Kumekuwa na ongezeko la wasi wasi nchini Nigeria
kufuatia hatua ya hivi karibuni ya wanamgambo wa Kiislam wa Boko haram
kuteka miji nchini humo.
Mamia ya raia wameanza kuukimbia mji wa Maiduguri baada ya wanamgambo hao kuuteka mji wa Bama.Mmoja kati maseneta ameiambia BBC kuwa raia hawaruhusiwi hata kuzika wapendwa wao waliokufa, miili ya waliofariki imetupwa kwenye mitaa na Boko Haram wakiranda randa mitaani.
Hata hivyo Serikali ya Nigeria inapinga vikali kuwa jimbo hilo la Bama limeangukia mikononi mwa Boko haram.
Mwanamke huyu anasema amelazimishwa kukimbia mji na amepoteza ndugu zake.
"Bado sijamwona baba yangu, mume wangu na watoto wangu. Hakuna askari yoyote wa serikali mahali popote. Boko haram wameuteka mji wa Bama. Nimerudi kutoka Bama. Kwa sasa nipo Maiduguri. nilichokiona wakati nilipokuwa nikiondoka Bama ni maiti za watu kila mahali. Wanaume, Wanawake na watoto. Wote wametupwa katika mitaa."
Bama imekuwa ikilengwa kila wakati na wapiganaji wa Boko haram tangu awali.
Seneta wa eneo hilo Zanna ameiambia BBC kuwa wanajeshi wa Nigeria wamekuwa wakijaribu kuulinda mji lakini ukajikuta ukiangukia kwa wanamgambo hao.
Amesema watu wengi wameuawa na kumekuwa na miili katika mitaa. Miji mingine iliyo karibu na mpaka wa nchi ya Cameroon nayo pia imetekwa ambayo ni Gwoza na Banki.
Boko haram wamekuwa wakidhibiti maeneo karibu yote Kaskazini mashariki na kuna habari kwamba wanadhibiti mipaka imewatia hofu wanigeria wengi.-BBC
Maoni
Chapisha Maoni