Vijidudu sugu vya Malaria vyagundulika
Mbu wa Malaria Watafiti wametoa tahadhari kuwa vijidudu vya malaria visivyoweza kuuawa kwa dawa vimetapakaa katika maeneo ya mpakani kusini mashariki mwa Asia vikitishia mapambano dhidi ya Malaria. Vipimo kwa wagonjwa 1000 katika maeneo ya Cambodia, Burma, Thailand na Vietnam vimegundua vijidudu hivyo havizuiliwi na artemisinin dawa inayoaminika katika vita dhidi ya malaria. Utafiti huo umeeleza kuwa kuyarudia matibabu baada ya kukumbana na maambukizi inaweza kusaidia kupambana na kusambaa kwa Malaria katika Asia na baadae Afrika ndani ya muda mfupi. Mamia ya maelfu ya watu hufariki kutokana na Malaria kila mwaka hasa katika Afrika. -bbc