ilipoishia Mazungumzo yao yaliendelea, wakafika nyumbani kwa mwalimu Magdalena, wakapitiwa na usingizi, kutokana na uchovu waliokuwa nao mwalimu Magdalena na mwalimu Joka wakajikuta wakiamka saa 4 asubuhi, tena baada ya John kuwagongea kutokana na kutomuona mwalimu Magdalena shuleni. “Sasa itakuwaje, nje kuna hodi inagongwa na sauti ya huyo mtu namjua ni wa shuleni, kama akikuona itakuwa balaa upya, watahisi kuna kitu kimefanyika kati yangu na wewe, sasa naomba ujifiche humu humu ndani mi natoka kumsikiliza.’’ “Sawa.” sasa endelea Mwalimu Magdalena alipotoka nje akakutana na John, mwanafunzi anayempenda, John hakutaka kuhoji chochote hadi aingie ndani lakini mwalimu Magdalena alionyesha hofu kama ya kusita, lakini akakubaliana na yote, John akaingia akakaa kitandani huku mwalimu Joka akiwa amejificha chini ya uvungu wa kitanda cha mwalimu Magdalena. “Mwalimu mbona hadi sasa hujafika shuleni kila mtu anahofu nawe, hakuna anayeelewa somo lolote hadi wakuone, mwa...
Maoni
Chapisha Maoni