Karani wa Basi amng'ata Mdomo mgambo wa Jiji
Mgambo wa Jiji aliye ng'atwa na Karani. |
Tukio hilo lilitokea ijumaa iliyopita saa 12 alfajiri katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani wakati mgambo huyo alipokuwa katika shughuli zake za kila siku.
shuhuda wa tukio hilo ambae pia ni bosi wa mtuhumiwa huyo James Zebedayo,alisema Mgambo huyo aling'atwa mdomo baada ya kutaka kumkamata Eliud kwakosa la kutokuvaa sare za kazi.
"Hawa mgambo walikuja asubuhi walikuwa kama sita hivi na walipofika hapa wakawa wamemuuliza kwamba kwa nini hakuwa na sare.
"Ambapo yeye aliwajibu kuwa siku hiyo ilikuwa ni siku ya Mashujaa, hivyo hakukuwa na umhimu wa kuvaa sare."alisema zebedayo.
Mara baada ya majibu hayo mgambo huyo alichachamaa na kumwijia juu na kusema kuwa ilikuwa ni lazima amkamate ili akamuadhibu kisheria, lakini karani huyo alikataa na kusema kuwa asingekubali kukamatwa mara mbili kwani siku chache zilizopita alikuwa amekamatwa kwa kosa lile lile.
Baada ya mvutano huo ndipo seke seke la kwenda katika kituo cha polisi ubungo lilipoanza ambapo muda mchache baadae karani huyo aliwazidi nguvu na kurudi.
Mgambo huyo alimfuata tena akiwa na wenzake ambapo hapo ndipo walipoanza kupambana nae, kwa bahati mbaya mgambo huyo alijikuta aking'atwa mdomo na karani huyo.
Askari wa Jeshi la polisi waliokuwapo eneo hilo ilibidi waingilie kati ambapo walimkamata mtuhumiwa huyo na kumpeleka katika kituo cha polisi kilichopo hapo.
Mkuu wa kituo cha polisi Suphian Masanga alisema kuwa majeruhi huyo alipewa pf3 na kukimbizwa katika Hospital ya Parestina iliyopo Sinza,dar es salaam huku mtuhumiwa akipelekwa katika kituo cha polisi Magomeni ambapo alifunguliwa jalada MAG/RB/7172/2014,kwa kosa la kujeruhi.
Maoni
Chapisha Maoni