Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2015

Kili' Stars 'OUT' Challenge

Picha
Michuano ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kama CECAFA Senior Challenge Cup yameendelea Leo November 30 kwa kupigwa mechi za kwanza za robo fainali ya michuano hiyo, miongoni mwa mechi za robo fainali zilizochezwa Leo November 30 ni mechi kati ya timu ya taifa ya Tanzania bara maarufu kama Kilimanjaro Stars ilicheza dhidi ya mwenyeji wa mashindano hayo timu ya taifa ya Ethiopia. Hii ni mechi ya robo fainali iliyokuwa inazikutanisha timu zilizokuwa kundi moja na mchezo wao wa mwisho walicheza na kumaliza kwa sare ya goli 1-1, November 30 Kilimanjaro Stars ilicheza mchezo huo ikiwa na kikosi chake kamili lakini kilikuwa na mabadiliko kidogo. Mchezo huo ambao Kilimanjaro Stars walianza kwa kupata goli la kuongoza kupitia kwa nahodha wao John Bocco dakika ya 24, dakika 90 zilimalizika kwa sare ya goli 1-1 baada ya Panom Cathuoch kuisawazishia goli Ethiopia dakika 57. Kwahisani ya Millardayo.com

Kabila Wamakua-2, Tohara ni lazima kwa kijana wa kimakua

Picha
KARIBU! Wiki hii tunaendelea kuangali kabila la wamakua kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania ambayo ni Mtwara na Lindi, licha ya ukweli kuwa kabira hili limetokea nchini Msumbiji. Wiki hii bado tupo kwenye sula zima la dini ambapo tunaelezwa kuwa jamii ya wamakua  walikuwa na utamaduni wa kudhulu kwenye kaburi na baada ya kufika hapo huanza  kuita jina la (Mluki kimila) wakiwa na maana ya Mungu. Jina ambalo hulitukuza, kitendo hicho hufanyika kwaajili ya kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu. Kwani kwa kufanya hivyo wamakua waliamini kuwa mungu alikuwa akisikia kilio chao nakwamba, ilikuwa rahisi kuwasikiliza matatizo yao kutokana na yeye kuwa mtu pekee ambaye angeweza kutatua changamoto zao. Nakwamba aliwaumba yeye na hivyo hakuwa na sababu ya kuwaona wakipata mateso na shida za maisha pasi kuwa sikiliza kilio na shida zao. Wamakua walikuwa wakimkimbilia mungu kwa kile walichoamini kuwa ni mtu pekee aliyejitolea kulipa dhambi zao, na hivy...

NYAKOREMA RIOBA aipiga tafu READ International

Picha
Nyakorema akiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Read International, Montse Pejuan Nyakorema Rioba delivered a donation of her new book ‘Nitakuwa Mfano’ (I will be a role model) to READ International on Friday 20 November.  Her books will be placed to new libraries that READ will be setting up in 2016 in Mtwara, Ruvuma, and Dar-es-Salaam. Nyakorema is a mother of 2 and a female engineer working at the Tanzania Bureau of Standards, with an interest in community development, particularly youth.  Nyakorema decided to write this book after learning that secondary schools students are only taught how to answer questions in exams, but they are not taught how to handle and solve their own pressing issues in their community and became the change they would wish to see in their community and world. This book encourages teenagers to develop a sense of vision and achieve their dreams.  It tells stories of other successful men and women who went through hardship but made ...

Rais MAGUFULI aondoa sherehe za Uhuru

Picha
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli ameagiza siku ya sikukuu ya Uhuru, 9 December hakutakua na sherehe za kitaifa na badala yake watu watatumia siku hiyo kufanya usafi katika maeneo yao. Maamuzi haya yamekuja siku chache baada ya Dk.Magufuli kutoa tena agizo la fedha zaidi ya milioni 250 ambazo zilikuwa zitumike kwenye sherehe za ufunguzi wa Bunge, Dodoma kuelekezwa kwenye ununuzi wa vitanda vya wagonjwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Rais amechukua maamuzi hayo kutokana na kukerwa na ugonjwa wa kipindupindu ambao tayari umepoteza maisha ya watu na bado umeendea kukumba maeneo mbalimbali nchini. Kwa niaba ya Rais, Katibu Mkuu kiongozi Ombeni Sefue baada ya kufanya ziara katika hospitali ya muhimbili alisema Rais ameagiza kuwa siku hiyo hakutakuwa na sherehe zozote za kitaifa na badala yake wananchi wataitumia kufanya usafi katika maeneo yao.   “Rais amesema suala la kuwepo ugonjwa Kipindupindu halikubaliki, jambo hili limemke...

Kocha Simba atimkia Indonesia

Picha
KOCHA msaidizi aliyetajwa kutua katika klabu hiyo, Mrundi Cedrick Kaze, amepata ulaji mnono nchini Indonesia. Simba walikuwa na mpango wa kumchukua Kaze ili aweze kusaidiana na Dylan Kerr baada ya msaidizi wake, Seleman Matola kuachia ngazi. Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya Klabu ya Simba zilieleza kwamba, kocha huyo amepata timu ya kufundisha Indonesia. “Tulitegemea kocha huyu angesaidiana vizuri na Kerr kwa kuiwezesha timu yetu kupata matokeo mazuri, lakini tulishindwa kumpata kutokana na kuhitaji mshahara mnono,” kilieleza chanzo chetu. Kilieleza kwamba baada ya kushindana na Simba ameamua kwenda Indonesia ambako amepata timu ya kufundisha. Hata hivyo, Simba wanaendelea na mchakato wa kupata kocha msaidizi ili aweze kusaidiana na Kerr. Simba tayari wameanza mazoezi kujiandaa na mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo leo wanatarajia kufanya mazoezi kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam.  W...

Maguli, Bocco waiua Somalia

Picha
  WASHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Tanzania Bara, ‘Kilimanjaro Stars’, John Bocco na Elias Maguli, wameiua Somalia baada ya kufunga mabao mawili kila mmoja katika ushindi wa mabao 4-0 walioupata katika mchezo wa Kundi A, wa Kombe la Chalenji uliochezwa jana   kwenye Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa, Ethiopia. Ushindi huo umewafanya Kilimanjaro Stars kuongoza kutokana na idadi ya mabao ya kufunga baada ya Rwanda kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Ethiopia. Katika mchezo wa jana, Bocco aliandika bao la kuongoza katika dakika ya 12 kwa penalti baada ya beki wa kulia, Shomary Kapombe kuangushwa eneo la hatari. Kilimanjaro Stars waliandika bao la pili kupitia kwa Maguli dakika ya 17 kabla ya Bocco kuongeza la tatu dakika ya 54. Hata hivyo, Maguli alifunga hesabu baada ya kufunga bao la nne na kukamilisha ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wapinzani wao hao. Kilimanjaro Stars iliundwa na Aishi Manula, Shomary Kapo...

Majwega ni habari nyingine

Picha
WINGA Brian Majwega anatajwa na mashabiki wa Simba kwamba ndiye atakayemaliza kiu ya mashabiki hao katika klabu hiyo hasa kutokana na kiwango chake alichokionyesha mazoezini. Nyota huyo kutoka Uganda juzi alifanya vitu adimu kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Lamada Beach Resort jijini Dar es Salaam na kuwakuna mashabiki wengi wa timu hiyo.   Brian Majwega Mazoezi hayo ya kujiandaa na mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mbali na mashabiki, Majwega alimkosha Kocha Mkuu wa timu hiyo, Dylan Kerr, kutokana na kuonyesha kuwa na vitu vingi na muhimu. Majwega anayedaiwa kusaini mkataba wa kuichezea Simba katika usajili dirisha dogo la Ligi Kuu Bara lililofunguliwa Novemba 15 mwaka huu baada ya kuwepo kwa mgogoro na klabu yake ya zamani ya Azam FC. Majwega alionekana lulu kwa mashabiki wa Simba na Kerr aliyekuwa akimfuatilia kwa karibu zaidi katika mazoezi hayo. Kerr alitumia muda mwingi kumfuatilia winga huyo kila ha...

Vigogo Yanga wampandia Maguli

Picha
YANGA wanatarajia kukamilisha usajili wa dirisha dogo la Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea mjini Addis Ababa, Ethiopia. Viongozi wa Yanga na benchi la ufundi la timu hiyo kwa sasa wako makini sana kuhakikisha wanapata wachezaji makini wa kuongeza nguvu kwenye kikosi chao ili kuhakikisha wanafanya maajabu katika michuano inayoendelea hasa ile ya kimataifa itakayoanza hapo mwakani. Maguli na Canavaro   Kutokana na hali hiyo zoezi la usajili kwenye klabu hiyo ya Jangwani limekuwa likifanyika kwa umakini mno, hasa katika kipindi hiki cha dirisha dogo na ndiyo maana hadi sasa bado hawajaweka wazi mipango yao ya usajili. Chanzo cha kuaminika kimeliambia BINGWA kwamba tayari viongozi wa Yanga wanasuka mipango ya kuvamia Ethiopia kuangalia nani anaweza kufiti kuingia kwenye kikosi chao, lakini pamoja na hivyo wanakwenda na jina la mshambuliaji wa Stand United, Elias Maguli kwa ...