KARIBU! Wiki hii tunaendelea kuangali kabila la wamakua
kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania ambayo ni Mtwara na Lindi, licha
ya ukweli kuwa kabira hili limetokea nchini Msumbiji.
Wiki hii bado tupo kwenye sula zima la dini ambapo
tunaelezwa kuwa jamii ya wamakua walikuwa na utamaduni wa kudhulu
kwenye kaburi na baada ya kufika hapo huanza kuita jina la (Mluki
kimila) wakiwa na maana ya Mungu.
Jina ambalo hulitukuza, kitendo hicho hufanyika kwaajili
ya kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.
Kwani kwa kufanya hivyo wamakua waliamini kuwa mungu
alikuwa akisikia kilio chao nakwamba, ilikuwa rahisi kuwasikiliza matatizo
yao kutokana na yeye kuwa mtu pekee ambaye angeweza kutatua changamoto
zao.
Nakwamba aliwaumba yeye na hivyo hakuwa na sababu
ya kuwaona wakipata mateso na shida za maisha pasi kuwa sikiliza kilio
na shida zao.
Wamakua walikuwa wakimkimbilia mungu kwa kile walichoamini
kuwa ni mtu pekee aliyejitolea kulipa dhambi zao, na hivyo hawakuwa
na namna nyingine zaidi ya kumpatia heshima.
Jambo kubwa kwa wamakua ilikua ni kudumisha amani
na upendo hasa kwa kuabudu mungu ambaye walikuwa hawamuoni, kwani inadaiwa
kuwa kabla ya kuwasili kwa waarabu na wazungu, jamii hii ya wamakua
walikuwa wapagani na hawakujua kabisa juu ya uwepo wa mungu.
Hivyo walikuwa wakiabudu miti na sanamu kama kawaida,
na baada ya kuwasili kwa wageni hao waliharibu utamaduni wa wamakuwa
kwenye suala la kuabudu.
Tohara
Kwenye kabila hili jambo la kufanyiwa Tohara ni kitu
cha lazima, pale kijana wa kiume anapotimiza miaka 12, ni lazima wazazi
wake wahakikishe kuwa wanaandaa mkakati wa kijana wao kufanyiwa tohar.
Chifu mdogo julikanaye kama Mwene lazima afike kwa
wazazi wa mtoto kwaajili ya kupanga ni kwamna gani na siku gani mtoto
huyo atafanyiwa sherehe mara baada ya kufanyiwa tohara. Ambapo kwenye
hilo huandaliwa wanaumme wawili huku mzazi mmoja akitakiwa kushuhudia
zoezi hilo.
Baada ya mipango yote kuandaliwa na kukamilika, siku
ya siku inapowadia wazazi hujenga nyumba ndogo kwaajili ya kijana anayefanyiwa
tohara kupumzika.
Baada ya zoezi hilo kukamilika wazazi huandaa sherehe
ya ngoma ambayo hii huwahusisha ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wakiwamo
majirani kwaajili ya kufurahia kitendo hicho cha mtoto wao, ambayo huchezwa
usiku.
itaendelea...
Maoni
Chapisha Maoni