Rais MAGUFULI aondoa sherehe za Uhuru
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli
ameagiza siku ya sikukuu ya Uhuru, 9 December hakutakua na sherehe za
kitaifa na badala yake watu watatumia siku hiyo kufanya usafi katika
maeneo yao.
Maamuzi haya yamekuja siku chache baada ya Dk.Magufuli kutoa tena
agizo la fedha zaidi ya milioni 250 ambazo zilikuwa zitumike kwenye
sherehe za ufunguzi wa Bunge, Dodoma kuelekezwa kwenye ununuzi wa
vitanda vya wagonjwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Rais amechukua maamuzi hayo kutokana na kukerwa na ugonjwa wa
kipindupindu ambao tayari umepoteza maisha ya watu na bado umeendea
kukumba maeneo mbalimbali nchini.
Kwa niaba ya Rais, Katibu Mkuu kiongozi Ombeni Sefue baada
ya kufanya ziara katika hospitali ya muhimbili alisema Rais ameagiza
kuwa siku hiyo hakutakuwa na sherehe zozote za kitaifa na badala yake
wananchi wataitumia kufanya usafi katika maeneo yao.
“Rais amesema suala la kuwepo ugonjwa
Kipindupindu halikubaliki, jambo hili limemkera sana, tunasherehekea
miaka 54 ya uhuru lakini bado kipindupindu kinatusumbua sana, amesema
kama Watanzania lazima tulishughulikie, haiwezekani akija mgeni kama
Obama tunafanya usafi lakini akiondoka tunaendelea kuwa wachafu, ameamua
tarehe 9 December siku ya uhuru hakutakuwa na sherehe yoyote badala
yake watu wakasafishe maeneo yao”..Ombeni Sefue.
Ombeni Sefue aliongeza kuwa “Amesema
hakutakuwa na cha kwenda kwenye Gwaride, kila mkuu wa Mkoa au kiongozi
yeyote wa eneo husika wanatakiwa waanze kuandaa vifaa vya usafi, itakuwa
ni siku ya kufanya usafi ili kupunguza tatizo la uchafu..ameowaomba
sana Watanzania si kwamba tuna dharau siku hii bali tunaifanya kwa
staili nyingine…kuhusu gharama za sherehe pesa zitakazotumika siku hiyo
Rais atatafuta kazi ya kuzifanyia, atazipeleka kwenye eneo lingine lenye
tatizo “..Ombeni Sefue.
Sefue aliongeza kuwa Rais amesema hatapenda kusikia baada ya Desemba
kuna maeneo bado yatakuwa na ugonjwa wa Kipindupindi na Mkoa ambao
utakuwa bado na ugonjwa huo viongozi wake watajieleza.
millardayo.com
Maoni
Chapisha Maoni