Kocha Simba atimkia Indonesia
KOCHA msaidizi aliyetajwa kutua katika klabu hiyo,
Mrundi Cedrick Kaze, amepata ulaji mnono nchini Indonesia. Simba walikuwa na mpango wa kumchukua Kaze ili aweze
kusaidiana na Dylan Kerr baada ya msaidizi wake, Seleman Matola kuachia ngazi.
Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya Klabu ya
Simba zilieleza kwamba, kocha huyo amepata timu ya kufundisha Indonesia.
“Tulitegemea kocha huyu angesaidiana vizuri na Kerr
kwa kuiwezesha timu yetu kupata matokeo mazuri, lakini tulishindwa kumpata
kutokana na kuhitaji mshahara mnono,” kilieleza chanzo chetu.
Kilieleza kwamba baada ya kushindana na Simba
ameamua kwenda Indonesia ambako amepata timu ya kufundisha.
Hata hivyo, Simba wanaendelea na mchakato wa kupata
kocha msaidizi ili aweze kusaidiana na Kerr.
Simba tayari wameanza mazoezi kujiandaa na
mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo leo wanatarajia kufanya mazoezi kwenye
viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu
hiyo mwishoni mwa wiki walifanya mazoezi kwenye ufukwe wa Giraffe kujiandaa na
mchezo wao wa mzunguko wa 10 dhidi ya Azam.-Bingwa
Maoni
Chapisha Maoni