Teknolojia iliwezesha Underwater Tennis kujengwa Dubai
NA FARAJA MASINDE UMOJA wa Falme za Kiarabu ni moja ya nchi zilizopiga hatua kubwa kwenye suala zima la teknolojia, hasa kwenye jiji la Dubai. Hii imekuwa ikichagizwa zaidi na uwepo wa wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali ambao wamejikita kuwekeza kwenye nchi hiyo. Mbali na mambo mengine, eneo la teknolojia ya majengo limekuwa ni sehemu inayoutambulisha mji wa Dubai kutokana na namna yalivyojengwa kila moja kwa muundo wake, jambo ambalo limesaidia taifa hilo kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya utalii. Lakini katika kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwa vinara kwenye kutumia teknolojia vyema, nchi hiyo imekamilisha uwanja wa tenisi, ukiwa ni mkakati wa kutaka kuboresha eneo la michezo kwa ujumla nchini humo. Pia ni sehemu ya kujikusanyia fedha kupitia uwanja huo kutoka kwa watalii ambao watakuwa wanafika kwa ajili ya kutaka kuushuhudia. Uwanja huo ambao umepewa jina la Underwater Tennis Stadium, unawawezesha wachezaji wa tenisi kucheza mchezo huo, huku pia ukitoa nafasi kwa m