Japan yatumia Smartphone kuandaa medali 2020
NA FARAJA MASINDE
MJI wa Tokyo uliopo nchini Japan, unataraji kuwa mwandaaji wa michuano ya Olimpiki ya mwaka 2020 ambapo tayari harakati zimeanza ili kuhakikisha inavunja rekodi ya Brazil kwa kuweka mambo mapya.
Ichukue hii kuwa Japan imeweka wazi mpango wake wa kutaka kutumia Smartphone za zamani na vifaa vya kielektroniki kwa ajili ya kuandaa medali zake kwenye michuano ya Olimpiki 2020.
MJI wa Tokyo uliopo nchini Japan, unataraji kuwa mwandaaji wa michuano ya Olimpiki ya mwaka 2020 ambapo tayari harakati zimeanza ili kuhakikisha inavunja rekodi ya Brazil kwa kuweka mambo mapya.
Ichukue hii kuwa Japan imeweka wazi mpango wake wa kutaka kutumia Smartphone za zamani na vifaa vya kielektroniki kwa ajili ya kuandaa medali zake kwenye michuano ya Olimpiki 2020.
Licha ya kwamba bado kuna muda wa miaka minne mpaka kufanyika kwa michuano ya Olimpiki, lakini tayari taifa hilo limetangaza mpango huo kupitia jarida la Nikkei Asian Review.
Taifa hilo la Japan ambalo limekuwa mstari wa mbele kwenye teknolojia ya juu ya uundaji wa magari, limeweka wazi mpango huo wa kutaka kuona simu hizo zikitumika tena 2020 mara baada ya kutupwa kama vifaa vibovu.
Waandaaji wa michuano hiyo ya Olimpiki ambayo itafanyika mjini Tokyo wanatumaini kuwa vifaa hivyo vya zamani vitakuwa nyenzo mhimu katika kuandaa medali za dhahabu, fedha na shaba. Hizi ni kwa ajili ya washindi wa michuano hiyo na kuongeza kuwa mamilioni ya simu yanatarajiwa kukusanywa kutoka nchini humo.
Tayari taifa hilo ambalo linakadiriwa kuzalisha vifaa vya kielektroniki takribani 6,500,000, mpaka sasa takribani simu 100,000 zilizokwisha tumika zimeshakusanywa kwa ajili ya zoezi hilo, hii ni kwa mujibu wa jarida la biashara la Nikkei.
Takwimu mbalimbali ambazo zimekusanywa na SportsTechnology zinaonyesha mwaka 2014, Japan ilikuwa tayari kurejesha kiwango kikubwa cha madini ya thamani kwa watumiaji wadogo wa vifaa vya kielektroniki ambapo ilijumuisha kilo 143 za dhahabu, 1,566 za fedha na tani 1,112 za shaba.
Katika kulinganisha na kiwango cha matirio ambayo yalitumika katika michuano ya Olimpiki jijini London mwaka 2012, Japan inahitaji kuwa na madini ya kutosha ili kukamilisha mpango wake huo.
Kwani katika michuano ya London ya mwaka 2012, taifa hilo lilitumia kiasi cha kilo 9.6 cha dhahabu, kilo 1,210 za fedha na kilo 700 za shaba.
Kampuni ya ReNet ni moja ya zile zilizotambulishwa Juni, mwaka huu, kwa ajili ya kusaidia mchakato mzima wa kushauri kampuni binafsi kufanya kazi pamoja ili kuendeleza na kusogeza mkakati huo ili kufanikisha mpango huo.
“Tunahitaji mfumo utakaofanya upatikanaji wa vifaa vya kielektroniki kama simu zilizotumika kuweza kupatikana kirahisi, anasema Takeshi Kuroda, ambaye ni Rais wa ReNet Japan Group.
“Mfumo wa ukusanyaji ni lazima uundwe na sekta binafsi, serikali kuu na zile za mitaa, ili kuhakikisha kuwa mchakato huu unafanikiwa kwa kiwango cha juu, lengo ni kuhakikisha kuwa tunaitumia teknolojia katika kutengeneza medali za kipekee zitakazoleta sifa kwenye taifa la Japan.
Bado haiko wazi iwapo Japan itakuwa tayari kukusanya malighafi yote inayohitajika, lakini labda kwakuwa kuna mkono wa serikali huenda hili likafanikiwa kwa kushirikiana na sekta binafsi pamoja na serikali za mitaa.
Miongoni mwa washirika wakubwa katika kuandaa mpango huo wa,
Tokyo Olimpiki na Paralimpiki ni kamati ya mashindano, Wizara ya Mazingira, Tokyo Metropolitan na baadhi ya kampuni za vifaa vya kielektroniki.
Tokyo Olimpiki na Paralimpiki ni kamati ya mashindano, Wizara ya Mazingira, Tokyo Metropolitan na baadhi ya kampuni za vifaa vya kielektroniki.
Maoni
Chapisha Maoni