Teknolojia iliwezesha Underwater Tennis kujengwa Dubai
NA FARAJA MASINDE
UMOJA wa Falme za Kiarabu ni moja ya nchi zilizopiga hatua kubwa kwenye suala zima la teknolojia, hasa kwenye jiji la Dubai.
Hii imekuwa ikichagizwa zaidi na uwepo wa wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali ambao wamejikita kuwekeza kwenye nchi hiyo.
Mbali na mambo mengine, eneo la teknolojia ya majengo limekuwa ni sehemu inayoutambulisha mji wa Dubai kutokana na namna yalivyojengwa kila moja kwa muundo wake, jambo ambalo limesaidia taifa hilo kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya utalii.
Lakini katika kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwa vinara kwenye kutumia teknolojia vyema, nchi hiyo imekamilisha uwanja wa tenisi, ukiwa ni mkakati wa kutaka kuboresha eneo la michezo kwa ujumla nchini humo.
Pia ni sehemu ya kujikusanyia fedha kupitia uwanja huo kutoka kwa watalii ambao watakuwa wanafika kwa ajili ya kutaka kuushuhudia.
Uwanja huo ambao umepewa jina la Underwater Tennis Stadium, unawawezesha wachezaji wa tenisi kucheza mchezo huo, huku pia ukitoa nafasi kwa mashabiki kutazama michezo hiyo chini ya maji.
Krzysztof Kotala akiwa kama msanifu majengo mkuu anayehusika na ujenzi wa uwanja huo wa chini ya maji, amesema lengo ni kuona uwanja huo ukiwa ni zaidi ya uwanja, kwa kuwa na vitu mbalimbali vitakavyovuta watu wengi zaidi, akiwa na maana ya kuutumia uwanja huo kama sehemu ya utalii wa Dubai.
Uwanja huo unakuwa ni wa kwanza duniani kujengwa chini ya maji, itakumbukwa kuwa mwaka 2005, Dubai ilitajwa kama chi inayopenda zaidi mchezo wa tenisi na kujenga uwanja wa mchezo huo wenye urefu wa futi 1,000 kwenye jengo la Burj Al Arab Hotel na hivyo kwa sasa wameamua kuja na hatua hii mpya ya uwanja chini ya bahari.
Umoja ya Falme za Kiarabu, hasa jiji la Dubai lipo mstari wa mbele miongoni mwa nchi zinazotumia teknolojia vizuri, uwanja huo ambao uko chini ya maji umejengwa kati ya jengo la Burj al Arab na visiwa vya Palm Jumeirah.
Kwa mujibu wa wataalamu waliohusika na ujenzi huo, wanasema unakadiriwa kufikia kiasi cha dola kati ya bilioni 1.7-2.5, ikiwa ni kwa mujibu wa mtaalamu wa ujezi wa Uwanja huo, Krzysztof Kotala, kutoka Kampuni ya Krakow Polytechnic.
Taarifa zinasema kwamba, uwanja huo utasaidia kuinua na kuboresha kiwango cha mchezo, hasa ule wa tenisi kwenye eneo la Asia, huku akisisitiza kuwa umejengwa kuhimili majanga ya asili kama kimbunga na matetemeko ya ardhi chini ya bahari, kwa mfano, Tsunami na aina nyingine ya majanga ya asili.
Hii ni tafsri kuwa ni uwanja imara uliojengwa kwa teknolojia ya kisasa, ikiwamo kutokuruhusu maji au samaki kupenya kwenye uwanja huo.
Lakini pia anasema kuwa, uwepo wa uwanja huo utasaidia kuimarisha biashara na kuvutia wawekezaji wengi.
Huu ni uwanja pekee ambao mtu unaweza kucheza au kutazama mchezo huku ukiwa unawashuhudia samaki kwa ukaribu zaidi.
Maoni
Chapisha Maoni