Data zako zinaweza ‘kudukuliwa’ pindi unapofungua tovuti

Na FARAJA MASINDE,
WATU wana akili nyingi mno siku hizi, hasa wadukuzi wa mitandaoni ambao ujuzi wao umekuwa ukiongezeka maradufu kulingana na teknolojia inavyobadilika.
Najua kuwa wengi tunatumia simu, Laptop, kompyuta na vifaa vingine kwa ajili ya kufungua mafaili na tovuti mbalimbali duniani.hacking
Lakini je, umewahi kujiuliza kuwa unaweza kujikuta unaibiwa taarifa zako muhimu (data) iwapo tu utafungua baadhi ya tovuti bila ya wewe kujua?
Kila siku tovuti mpya zinafunguliwa duniani tena zikiwa na maudhui mbalimbali yanayozitofautisha japo lengo ni moja tu kupasha habari na kutoa elimu kwa umma.
Hata hivyo, kwenye tovuti hizo zinazoendelea kuongezeka, asilimia kubwa si salama ambapo unaweza kujikuta unapoteza taarifa zako muhimu pindi tu unapozifungua.
Na hivyo kujikuta ukipoteza mambo yako mengi ya siri ambayo umekuwa ukiyahifadhi kwenye simu au kifaa chako chochote cha mawasiliano ambacho umekuwa ukikiamini daima.
Hata hivyo, kama hukuwahi kujua na umekuwa ni miongoni mwa watu wanaopenda kufungua tovuti mbalimbali (Website) ili kujielimisha basi teknolojia inakuja na njia muhimu za kujikinga na janga hili.
Mara zote hakikisha kuwa unatumia njia salama unapokuwa unahitaji kutembelea tovuti, ambazo ni Google Chrome na ile ya Mozilla Firefox  huku ukihakikisha kuwa unakuwa unafuatilia maboresho yoyote yanayofanywa na vyanzo hivi vikubwa.
Njia ya pili ya kujiepusha na kudukuliwa kwa data zako ni kuepuka kuhifadhi nyaraka za siri kwenye vyanzo hivyo vikubwa (Google- Mozilla) kwani kuna muda watu wengi wasiopenda kujihangaisha wamekuwa hawapendi kuweka namba za siri (Password) na hivyo kujikuta wakitaka google au Mozilla iwakumbushe, jambo ambalo si salama kwa taarifa zako.
Ni vyema na salama zaidi iwapo utachukua uamuzi wa kuhifadhi nywila yako (Password) kichwani lakini si vinginevyo.
Jambo jingine ili kubaki salama ni kutumia Antivirus unayoilipia mwenyewe na si zile za bure zinazotolewa na baadhi ya mitandao mbalimbali tena kwa masharti nafuu.
Hii itakusaidia kuwa salama zaidi, lakini pia usisahau kuifanya Antivirus yako hiyo kuwa Updated wakati wowote wa matumizi.
Jambo jingine la kuzingatia ni kuhakikisha kuwa kompyuta Firewall ipo wazi muda wote hii itakuepusha na wadukuzi wanaoingia kwenye kifaa chako bila kuwa na taarifa pindi unapokuwa kwenye mtandao.
0653045474

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4