Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2016

Mayanja: Azam, Yanga wasijidanganye

Picha
BAADA ya Yanga, Azam FC kutinga nusu fainali ya Kombe la FA, Kocha wa Simba, Jackson Mayanja amesema hana presha yoyote juu ya timu atakayokutana nayo katika hatua zinazofuata za michuano hiyo kati ya wapinzani wake hao ambao wamekuwa wakijitanganya wakijiona wao ni kila kitu kwenye soka la Tanzania. Kocha wa Simba, Jackson Mayanja Yanga na Azam juzi zilifanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la FA baada ya kushinda michezo yao ya robo fainali ambapo Wanajangwani waliwachapa Ndanda FC mabao 2-1, huku Wanalambalamba wakiipiga Tanzania Prison mabao 3-1 kwenye viwanja Taifa na Azam Complex, Dar es Salaam. Timu nyingine iliyotinga nusu fainali ni Mwadui, huku Simba ikisubiriwa kuungana na wenzake hao iwapo itaitoa Coastal Union wiki ijayo. Akizungumza na BINGWA jijini jana, Mayanja alisema anachokiangalia kwa sasa ni kuhakikisha timu yake inafanya vizuri ili waweze kutinga nusu fainali. Alisema wakishinda mchezo wao huo dhidi ya Coastal, hakuna timu ambayo ataihofia mbele

Yondani ampa ujumbe mzito Pluijm

Picha
BEKI kisiki ‘roho’ ya Yanga, Kelvin Yondani amekiangalia kwa umakini kikosi cha Al Ahly na kubaini   kiungo wa miamba hiyo ya Misri, Ramadan Sobhy, ni mchezaji hatari zaidi kwa upande wao kuelekea katika pambano lao litakalopigwa Jumamosi ijayo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iwapo kocha wao, Hans van der Pluijm hatashtuka mapema. Kwa kufahamu hilo, Yondani amemtaka Pluijm na benchi lake la ufundi kuchukua hatua za haraka kuhakikisha anaipa mbinu za kutosha safu yao ya ulinzi kabla ya kuwavaa mabingwa hao wa kihistoria wa Afrika. Kati ya mambo amabyo beki huyo amemuasa kocha wao kuyafanyian kazi, ni kusisitiza kubadilika kiuchezaji kwa baadhi ya wachezaji wao, hasa kuongeza umakini na kuepuka kufanya makosa ambayo aynaweza kuwaponza na kujikuta wakipigwa mvua ya mabao siku hiyo. “Tumewaona Al Ahly ni timu nzuri, lakini wana mtu anaitwa Sobhy, kwa upande wetu mtu huyu ni hatari zaidi, anajua sana na nina imani tusipokuwa makini, anaweza kutusumbua, hivyo kunahitaji mbi

Amnesty: Uturuki imewatimua wakimbizi

Picha
Shirika la kutetea haki za binadamu duniani, Amnesty International linadai kuwa na ushahidi unaoonyesha kwamba Uturuki imewarudisha nyumbani wakimbizi wa Syria kinyume cha sheria. Shirika hilo limesema maafisa wa Uturuki wamekuwa wanawakamata na kuwarudisha wakimbizi wa Syria katika makundi ya watu mia mia, wanaume, wanawake na watoto kila siku, tangu katikati ya mwezi wa Januari. Wengi miongoni mwa wakimbizi hao walikuwa wale ambao hawakusajiliwa rasmi. Hata hivyo asasi ya Amnesty International imedai kuorodhesha mikasa ya wakimbizi waliofukuzwa ambao walikuwa wamesajiliwa. Watu hao walirudishwa nchini Syria kwa sababu hawakuwa na hati zao za usajili wakati walipokamatwa. Wakimbizi wauliwa kwa kupigwa risasi Wakati huo huo shirika la Syria la kutetea haki za binadamu lenye makao yake mjini London limesema limepata ushahidi unaonyesha jinsi wakimbizi 16 walivyopigwa risasi na kufa ,wakati walipokuwa wanajaribu kuuvuka mpaka wa Syria ili kuingia Uturuki.Lakini shirik

Ripoti: Watu wanene 'ni wengi duniani'

Picha
Utafiti mpya umeonesha watu wazima wengi duniani ni wanene kupita kiasi na kwamba hakuna matumaini ya kufikia lengo la kupunguza idadi ya watu wanene duniani. Wanasayansi waliofanya utafiti huo ambao walitoka Chuo cha Imperial cha London, wakiandika katika jarida la kimatibabu la Lancet la Uingereza, wanasema miongo minne iliyopita, kuwa na uzani wa chini kupita kiasi lilikuwa tatizo kubwa kuliko unene. Wanasema idadi ya wanaume wanene imeongezeka mara tatu, nayo ya wanawake ikaongezeka mara dufu. Profesa Majid Ezzat, aliyeongoza utafiti huo, anasema ni kana kwamba kuna "mkurupuko wa unene". Wanasayansi hao wanaonya kwamba tatizo hilo ni kubwa sana kiasi kwamba haliwezi kutatuliwa kupitia njia za kawaida za matibabu au kutenga maeneo ya kuendeshea baiskeli. Wanazihimiza serikali kuchukua hatua za pamoja, hasa kuhusu bei ya vyakula. Baada ya kuchunguza takwimu kutoka nchi 186, watafiti hao walibaini kwamba idadi ya watu wanene duniani imeongezeka kutok

Mzaha wa Google Siku ya Wajinga waleta balaa

Picha
Google jana imelazimika kuondoa kitufe cha Siku ya Wajinga kutoka kwenye huduma yake ya barua pepe ya Gmail baada ya watu wengi kulalamika. Kitufe hicho kilikuwa kinatuma video za mzaha kwa watu walio kwenye anwani ya mtu. Kitufe hicho kilikuwa kimewekwa karibu na kitufe cha kawaida cha kutuma barua pepe na kiliwawezesha watumizi wa Gmail kusitisha mawasiliano ya kawaida na badala yake kutuma video fupi ya gif ya kibonzo kikiweka chini maikrofoni.

UN kutuma wanajeshi Burundi

Picha
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio la kuweka mikakati ya kuwatuma wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi, ambapo vita vya kisiasa vilivyochukua takriban mwaka mmoja vinatishia kuwa vita vya kikabila. Azimio hilo lililowasilishwa na Ufaransa limeutaka Umoja wa Mataifa kuweka mpango madhubuti wa kuwatuma maafisa wa kurejesha amani kwa ushirikiano na serikali ya Burundi. Hata hivyo rais wa Burundi , Pierre Nkurunziza, amepinga hatua yoyote ya kuingilia kati Umoja wa Mataifa na pia Umoja wa Afrika. Zaidi ya watu 400 wameuawa na robo milioni kutafuta hifadhi katika mataifa jirani tangu kuzuka kwa vurugu hizo mwaka uliopita.

Nigeria yafanya maandamano ya kumuunga mkono Sheikh Zakzaky

Picha
Wananchi wa Nigeria wamefanya maandamano kulalamikia kuendelea kuwekwa korokoroni kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo. Sheikh Ibrahim Zakzaky anaendelea kushikiliwa mahali pasipojulikana huko Nigeria bila ya kushtakiwa licha ya kupita zaidi ya miezi mitatu sasa tangu atiwe mbaroni. Wakazi wa mji wa Zaria katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria jana waliandamana kulalamikia kuendelea kuzuiliwa korokoroni Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, huku wakiwa wamebeba mabango na kupiga nara zinazosema "Muachieni huru Sheikh Zakzaky." Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maandamano hayo yamefanyika huku Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ikikanusha madai kuwa wanachama wa harakati hiyo wiki iliyopita walimteka nyara kanali mmoja wa jeshi na kumuua. Vikosi vya jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka jana viliishambulia nyumba ya Sheikh Ibrahim Zakzaky katika mji wa Zaria jimboni Kaduna na husseiniya kadhaa nchini humo, na kish

Obama: Trump haelewi sera...

Picha
Mgombea wa kiti cha urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump, hana ufahamu wowote wa sera za kigeni wala maswala ya ulimwengu! Haya ni kulingana na rais wa Marekani Barrack Obama. Obama ameyasema haya kufuatia matamshi ya Donald Trump kuwa wanajeshi wa Marekani wanafaa kuondoka Japan na Korea Kusini, na mataifa hayo yanafaa kutengeneza zana zao za kinyuklia. Mataifa hayo mawili pia hayakufurahishwa na matamshi ya bwana Trump. chanzo- bbc