Yondani ampa ujumbe mzito Pluijm
BEKI kisiki
‘roho’ ya Yanga, Kelvin Yondani amekiangalia kwa umakini kikosi cha Al Ahly na
kubaini kiungo wa miamba hiyo ya Misri,
Ramadan Sobhy, ni mchezaji hatari zaidi kwa upande wao kuelekea katika pambano
lao litakalopigwa Jumamosi ijayo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iwapo
kocha wao, Hans van der Pluijm hatashtuka mapema.
Kwa
kufahamu hilo, Yondani amemtaka Pluijm na benchi lake la ufundi kuchukua hatua
za haraka kuhakikisha anaipa mbinu za kutosha safu yao ya ulinzi kabla ya
kuwavaa mabingwa hao wa kihistoria wa Afrika.
Kati
ya mambo amabyo beki huyo amemuasa kocha wao kuyafanyian kazi, ni kusisitiza kubadilika
kiuchezaji kwa baadhi ya wachezaji wao, hasa kuongeza umakini na kuepuka
kufanya makosa ambayo aynaweza kuwaponza na kujikuta wakipigwa mvua ya mabao
siku hiyo.
“Tumewaona
Al Ahly ni timu nzuri, lakini wana mtu anaitwa Sobhy, kwa upande wetu mtu huyu ni
hatari zaidi, anajua sana na nina imani tusipokuwa makini, anaweza kutusumbua,
hivyo kunahitaji mbinu za ziada katika kumdhibti,” alisema.
Yondani
amelipsaha BINGWA kuwa Sobhy anayevaa jezi namba 27, ni fundi wa kufunga, huku pia
akiwa ni mtundu wa kupiga chenga za maudhi na kukaa na mpira, hivyo anapaswa
kupewa ulinzi wa ziada.
Mkali
huyo ambaye kwa sasa ndiye tegemeo katika kikosi cha Yanga, alisema kiungo wao
mkabaji, Pato Ngonyani, ana mapungufu machache ambayo yanaweza kurekebishika na
akacheza vizuri siku hiyo hivyo kuwapunguzia mabeki kazi ya kukaba.
Alisema
kuwa iwapo Ngonyani hatakuwa makini katika kuhakikisha ‘anamalizana’ na Sobhy
au hata El Said Abdallah ambaye naye ni moto wa kuotea mbali, hali inaweza kuwa
mbaya zaidi kwao, kwani watakuwa wakimwekea ulinzi mkali mshambuliaji hatari wa
mabingwa hao wa Misri, Malick Evouna raia wa Gabon.
Katika
siku za hivi karibuni katika michezo kadhaa ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la
F.A na ya Kimataifa, Pluijm amekuwa akimchezesha Ngonyani katika nafasi ya
kiungo mkabaji badala ya Mbuyu Twite.
Pamoja
na kupewa nafasi hiyo, bado Ngonyani amekuwa akishindwa kuimudu vyema nafasi
hiyo, hivyo kuwafanya mabeki wake wa kati, Yondani na Vincent Bossou kujikuta
katika mshike mshike mara kwa mara.
Kati
ya kasoro alizonazo Ngonyani, ni uzito wa maamuzi, kupandisha timu, kuwasaidia
mabeki wa pembeni wawapo na mpira, lakini pia wepezi wa kumwezesha kumudu
kunyambulika (flexibility) kwendana na kasi ya mchezo, zaidi ikiwa ni
washambuliaji wepesi na wajanja wanaposaka mabao.
Mathalani
katika mchezo wa juzi wa Kombe la FA kati ya Yanga na Ndanda, Ngonyani
alishindwa kukabiliana na washambuliaji wa wapinzani wao hao, wakiongozwa na Atupele
Green na nahodha wao, Kiggi Makasy, hivyo Pluijm kuamua kumtoa na kumwingiza
‘fundi’ Salumj Telela.
Kuingia
kwa Telela kulionekana kuongeza uhai katika safu ya kiungo ya Yanga ambapo
mkali huyo alionyesha kiwango cha hali ya juu, akishirikiana vena na Thaban
Kamusoko na hivyo kuwakosha vilivyo mashabiki wa timu yao waliojitokeza
uwanjani hapo, wakiwamo wale waliokuwa wakiufuatilia mchezo huo kupitia runinga
zao.
Ni
kwa kufahamu hilo, Yondani anadhani Ngonyani anatakiwa kubadili aina yake ya
uchezaji ili kuendana na kasi ya wachezaji wa Al Ahly ambao wengi wao ni wazoefu
wa michuano ya kimataifa, lakini pia wakiwa na kasi na nguvu, lakini akionekana
‘kumtupia mpira’ Pluijm ambaye ndiye mwamuzi wa mwisho katika suala zima la
kupanga kikosi.
Hivyo,
mkali huyo ambaye mashabiki wa Yanga wamempachika jina la Vidic, wakimfananisha
kiuchezaji na beki wa zamani wa Manchester United, Nemanja Vidic, amesema iwapo
Pluijm atashiondwa kurekebisha kasoro zilizopo ndani ya kikosi chao, zaidi
ikiwa ni umakini wa viungo wao, asije kushangaa wakipigwa mabao ya kumwaga.
Mara
ya mwisho timu hizo mbili zilikutana Machi 2014 ambapo walipambana kwenye mechi
ya hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika na miamba hiyo ya Misri ilifanikiwa
kusonga mbele kwa ushindi wa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-3 baada ya kila
timu kushinda bao 1-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Mbali
ya Sobhy na Abdallah, wakali wengine wa Al Ahly wanaotarajiwa kuivaa Yanga wiki
ijayo ni John Antwi, Hossam Ghaly na wengineo waliopo katika kikosi cha timu ya
Taifa ya Misri.
Bingwa
Maoni
Chapisha Maoni