UN kutuma wanajeshi Burundi
Baraza la usalama la Umoja wa
Mataifa limeidhinisha azimio la kuweka mikakati ya kuwatuma wanajeshi wa
Umoja wa Mataifa nchini Burundi, ambapo vita vya kisiasa vilivyochukua
takriban mwaka mmoja vinatishia kuwa vita vya kikabila.
Azimio
hilo lililowasilishwa na Ufaransa limeutaka Umoja wa Mataifa kuweka
mpango madhubuti wa kuwatuma maafisa wa kurejesha amani kwa ushirikiano
na serikali ya Burundi.
Hata hivyo rais wa Burundi , Pierre Nkurunziza, amepinga hatua yoyote ya kuingilia kati Umoja wa Mataifa na pia Umoja wa Afrika.
Zaidi ya watu 400 wameuawa na robo milioni kutafuta hifadhi katika mataifa jirani tangu kuzuka kwa vurugu hizo mwaka uliopita.
Maoni
Chapisha Maoni