Machapisho

Udhaifu mkubwa wagunduliwa kwenye simu za iPhone

Picha
Mfumo wa Apple wa utendaji wa iOS umegundulika ambao utawezesha kupachikwa kwenye kifaa cha uchunguzi kukiwezesha kubofya kwenye kiunganishi. Uvumbuzi huo ulifanyika baada ya wakili anayetetea haki za kibinadamu kutoa taarifa kwa watafiti wa masuala ya usalama kuhusu jumbe alizozipata bila kutarajia. Waligundua taarifa nyingine tatu za awali zisizofahamika zilizovuja kutoka kwa mfumo wa Apple . tangu wakati huo Apple imetoa taarifa ya kuelezea tatizo hilo na namna linavyoshughulikiwa na kampuni hiyo. Makampuni mawili ya usalama yaliyohusika , Citizen Lab na Lookout, yamesema yamehifadhi taarifa hizo za uvumbuzi hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi. Kampuni ya Citizen Lab inasema , simu yake ya iPhone 6 ingekuwa ''imefunguliwa'' , ikimaanisha mfumo mwingine ambao haukuidhinishwa ungelikuwa umewekwa kwenye simu yake. "Na kama simu yake ingeathiriwa , ingekuwa kifaa cha upelelezi cha digitali ndani ya mfuko wake wa nguo, yenye uwe...

Maji ya dunia yanahama?

Picha
Wanasayansi wametumia picha za za setilaiti kuchunguza namna maji ya dunia yalivyohama kwa zaidi ya miaka 30. Walibaini kwamba kilo mita za mraba 115,000 za ardhini kwa sasa zimefunikwa na maji na kilomita 173,000 za maji zimefunikwa sasa na ardhi. Ongezeko kubwa la maji limetokea katika eneo tambarare la betan , huku bahari ya Aral eneo kubwa la maji sasa limegeuka kuwa ardhi. wanasayansi hao wanasema kuwa maeneo ya mwambao pia yamekuwa na mabadiliko makubwa . Utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti ya Deltares ya nchini Uholanzi umechapishwa na jarida la mabadiliko ya asili ya hali ya hewa. Watafiti walitathmini picha za setilaiti azilizochukuliwa na kituo cha wataalam wa masuala ya anga cha Nasa ,ambacho kimekuwa kikichunguza dunia kwa miongo kadhaa . Waliweza kufuatilia mabadiliko ya sehemu ya juu ya dunia inayoweza kuonekana kwenye kipimo maalum . Waliweza kubaini eneo pana ambalo wakati mmoja liliwahi kuwa ardhi ambalo sasa limekuwa na maji...

Huawei yapanua mlolongo wa Y-Series kwa simu za 4G nchini

Picha
Kampuni ya Huawei Tanzania wametangaza hivi punde kutanua mlolongo wake wa Y-Series kwa kuongeza simu mbili mpya za Huawei Y3II na Y5II. Simu hizo mbili za Y-Series zimekuja katika aina mbili nayo ni ya 3G na 4G zikiwalenga wateja wa soko la chini na kati. Simu hizi zimekua zikipatikana kwa watumiaji Tanzania tangu mapema mwezi Julai. Huawei Y3II Simu za 4G zina kasi ya hali ya juu ya intaneti kwa ajili ya kuperuzi, kutuma, kupokea na kupakua ujumbe, ikiongeza matumizi ya intaneti yasiyo na matatizo. Huawei Tanzania inayoongoza katika usambazaji wa simu za mkononi nchini Tanzania imewakumbuka kwa mara nyingine watu wa hali ya   chini kwa kuwaletea simu hizi zenye uwezo mkubwa wa internet. “Upanuzi wa simu zetu za bei nafuu na zenye uwezo wa 4G nchini kote imeenda sambamba na msimamo wetu kuwapatia wateja wetu huduma zilizo bora na za kimataifa ambazo zitaruhusu watanzania wote kufurahia kasi ya 4G bila kujali kipato chao”, alisema Bi Jane Wang, Meneja masoko wa Huawei ...

WhatsApp ku-share namba yako na Facebook

Picha
Kama unatumia WhatsApp kwaajili ya kutuma meseji kwa ndugu, jamaa na marafiki, kaa tayari kwa facebook kukufundisha mengi zaidi yatakayo kuhusu wewe ikiwamo kukutengeneza fedha. Mtandao wa WhatsApp umetangaza kuwa utaanza kushirikisha namba za simu na taarifa juu ya shughuli za watumiaji wake zaidi ya bilioni moja kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook ambao ni mtandao mama wa WhatsApp kwa zaidi ya miaka miwili sasa. WhatsApp wamesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kusaidia kufanya maboresho ya taarifa za wateja wao ikiwamo pia kuwasaidia watumiaji wa Facebook kubadilishana taarifa.   "Facebook na makampuni mengine ambayo yako chini ya familia ya Facebook yanaweza kutumia taarifa zako kutoka kwetu ili k uboresha uzoefu wako ndani ya huduma zao kama vile kufanya mapendekezo bidhaa na huduma mbalimbali, marafiki au uhusiano na mambo mengine yanayovutia, japo huduma hizo zitakuwa zitafanyika kwa sera zilezile za kulinda faragha za watumiaji. Hata hivyo hatua hiy...

Wafanyakazi wa Yahoo hawajui hatima yao?

Picha
Siku chache baada ya mtandao wa Yahoo kununuliwa na kampuni ya Verizon taarifa kutoka ndani ya wafanyakazi wa mtandao huo zinasema kuwa kwasasa hawajui hatiama yao chini ya uongozi huo mpya. Hata hivyo mtandao wa Cnn Money umeripoti kuwa mauzo ya hisa za mtandao huo ambazo zilidaiwa kuporomoka kwa kipindi kirefu kwasasa zimepanda na kurejea kwenye hali yake ya kawaida mara tu baada ya kununuliwa na kampuni ya Verizon. Yahoo wenyewe kupitia mtandao wao wamedai kuwa, kwasasa wafanyakazi wana morali ya juu ya utendaji kazi nakwamba wanajitahidi kuwapa motisha ili kuhakikisha kuwa mwaka huu wanafikia malengo. "Tuna imani kubwa ya kufanya vyema mwaka huu kwani mtandao wetu unaendelea kufanya vyema kwenye eneo la habari, michezo na uchumi kutoka mwezi hadi mwezi, hivyo tunatambua fika kuwa Yahooo chini ya Verizon utakuwa zaidi katika nyanja ya upashaji habari duniani," amenukuliwa mmoja wa maofisa habari wa Yahoo. Wadadisi wa mamabo wanasema kuwa hata baadhi ya wabunifu w...

Staa wa Nigeria Kiss Daniel kupamba tamasha la ‘MONTE CARLO CLASSIC’ Dar leo

Picha
Mwanamuziki maarufu wa Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel anayefahamika kwa jina la kisanii Kiss Daniel aliyetamba hasa kwa kibao chake cha ‘Woju’ kwenye anga za muziki,  ametua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa Tamasha la Monte Carlo Classic lililoandaliwa na Str8up Vibes wakishirikiana na DeJurist Global kwa udhamini wa Benki ya Barclays Tanzania. Kiss Daniel Mwimbaji huyo wa Nigeria aliyejizolea mashabiki wengi tangu alipoachia kibao chake cha ‘Woju’, ataongoza uzinduzi wa Tamasha hilo Jumamosi hii jijini Dar es Salaam katika Mgahawa wa Akemi uliopo kwenye jengo la Jubilee Towers, Mtaa wa Ohio. Mkurugenzi Mtendaji wa Str8up Vibes, Sniper Mantana alithibitisha mbele ya waandishi kwamba maandalizi ya Tamasha hilo yamekamilika na kuwasihi Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kujumuika na msanii huyo maarufu. Ameongeza kwamba kabla ya Tamasha hilo tiketi zitauzwa kwa shilingi 25,000 na itakapo timu usiku tiketi zit...

Mitandao ya kijamii yamnyima usingizi Tiwa Savage

Picha
Staa wa muziki nchini Nigeria, Tiwa Savage, amedai kuwa anajuta kuweka wazi mambo yake ya ndoa katika mitandao ya kijamii. Msanii huyo kwa sasa kazi zake zinasimamiwa na kampuni ya Rock Nation, inayomilikiwa na mkali wa rap nchini Marekani, Jay Z. Tiwa amedai kuwa kwa siku za hivi karibuni amekuwa akiyaweka mambo yake ya ndoa katika mitandao, hasa baada ya kuhojiwa mara kwa mara, lakini kitendo hicho kimewafanya watu wamzungumzie vibaya. “Katika kitu ambacho naweza kusema kuwa nimekosea katika maisha yangu ni kuweka wazi mambo yangu ya ndoa, najuta kwa kuwa kuna watu ambao wananiongelea vibaya kutokana na taarifa ambazo niliziongea, kuanzia sasa siwezi kufanya hivyo tena kwa mambo yangu binafsi,” amesema Tiwa.