WhatsApp ku-share namba yako na Facebook
Kama unatumia WhatsApp kwaajili ya kutuma meseji kwa ndugu, jamaa na marafiki, kaa tayari kwa facebook kukufundisha mengi zaidi yatakayo kuhusu wewe ikiwamo kukutengeneza fedha.
Mtandao wa WhatsApp umetangaza kuwa utaanza kushirikisha namba za simu na taarifa juu ya shughuli za watumiaji wake zaidi ya bilioni moja kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook ambao ni mtandao mama wa WhatsApp kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
WhatsApp wamesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kusaidia kufanya maboresho ya taarifa za wateja wao ikiwamo pia kuwasaidia watumiaji wa Facebook kubadilishana taarifa.
"Facebook na makampuni mengine ambayo yako chini ya familia ya Facebook yanaweza kutumia taarifa zako kutoka kwetu ili kuboresha uzoefu wako ndani ya huduma zao kama vile kufanya mapendekezo bidhaa na huduma mbalimbali, marafiki au uhusiano na mambo mengine yanayovutia, japo huduma hizo zitakuwa zitafanyika kwa sera zilezile za kulinda faragha za watumiaji.
Hata hivyo hatua hiyo itategemea na namna watumiaji wa mitandao hiyo husika watakavyopokea.
Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa WhatsApp wameponda uamuzi huo na kuonyesha hasira zao waziwazi kupitia mtandao wakijamii wa Tweitter na kutishia kufunga akaunti zao.
"Namba za simu?!? Hapana! Hiyo haiwezekani kabisa si sawa, hii itanifanya nifute akaunti yangu ya Facebook," amenukuliwa mmoja wa watumiaji wa WhatsApp aliyeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Mmiliki wa mitandao hiyo, Mark Zuckerberg amesema kuwa hatua hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwani itawawezesha watumiaji wa mitandao hiyo kutengeneza fedha kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii.
Pia itawarahisishia wafanyabiashara kuwasiliana na wateja wao moja kwa moja, licha ya ukweli kuwa itachukua muda kwa watumiaji kuweza kuelewa lengo la kuanzisha huduma hiyo.
Ngoja tuendelee kuusubiri uamuzi huu wa, Mark Zuckerberg kwani kila kukicha amekuwa na miakakati mipya juu ya mitandao yake hiyo, usikuse kuendelea kutembelea blog hii kwa taarifa zaidi.

Maoni
Chapisha Maoni