Staa wa Nigeria Kiss Daniel kupamba tamasha la ‘MONTE CARLO CLASSIC’ Dar leo
Mwanamuziki
maarufu wa Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel anayefahamika kwa jina
la kisanii Kiss Daniel aliyetamba hasa kwa kibao chake cha ‘Woju’
kwenye anga za muziki, ametua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
uzinduzi wa Tamasha la Monte Carlo Classic lililoandaliwa na Str8up
Vibes wakishirikiana na DeJurist Global kwa udhamini wa Benki ya
Barclays Tanzania.
Kiss Daniel |
Mwimbaji
huyo wa Nigeria aliyejizolea mashabiki wengi tangu alipoachia kibao
chake cha ‘Woju’, ataongoza uzinduzi wa Tamasha hilo Jumamosi hii jijini
Dar es Salaam katika Mgahawa wa Akemi uliopo kwenye jengo la Jubilee
Towers, Mtaa wa Ohio.
Mkurugenzi Mtendaji wa Str8up Vibes, Sniper Mantana alithibitisha mbele ya waandishi kwamba maandalizi ya Tamasha hilo yamekamilika na kuwasihi Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kujumuika na msanii huyo maarufu.
Ameongeza
kwamba kabla ya Tamasha hilo tiketi zitauzwa kwa shilingi 25,000 na
itakapo timu usiku tiketi zitauzwa kwa shilingi 35,000.
Tamasha la "Monte Carlo Classic" limelenga kubadilishana uzoefu baina ya Watanzania hususani kwenye sekta ya burudani.
“Kwenye
miji kama vile;-Monte Carlo, New York, Los Angeles (L.A), Paris watu
maarufu hushiriki kwa kupamba matukio kama haya. Hii ni sawa na ambavyo
sisi tumelenga kuliimarisha tamasha la Monte-Carlo Classic jijini Dar es
Salaam, ambapo kwa usiku mmoja kila mtu anakuwa mtu wa hadhi ya juu,
huku akisherehekea na mtu maarufu aliyeteuliwa na kwenye eneo lenye
hadhi ambalo limeandaliwa na waandaaji,” alisema.
Kwa
mujibu wa Meneja Masoko wa Benki ya Bacrays Tanzania, Joe Bendera,
alisema benki hiyo imekuwa ikidhamini ligi kubwa ya soka ulimwenguni
jambo ambalo limeifanya kuisogeza karibu na jamii. Tunayo furaha kuwa
sehemu ya uzinduzi wa Tamasha kama hili kubwa jambo ambalo litatuwezesha
kukutana na wageni waalikwa mbalimbali na wateja wetu.
"Tukio
hili linatupa fursa ya kutoa elimu kuhusu matumizi ya kadi zetu na
kuhamasisha matumizi yake sehemu mbalimbali kwenye mashine za mauzo
maeneo mbalimbali nchini. Mwezi uliopita Benki ya Barclays ilitunukiwa
cheti cha ubora cha Mtoaji wa Kadi Bora za Visa nchini Tanzania.
Pia
katika kubeba fedha taslimu kuna kiwango maalumu hivyo tutapata fursa
ya kuwahamasisha wateja wetu kutumia kadi zetu za Debit na Cretid kwenye
tukio hili,".
Kwa
upande wake msanii huyo alisema alishtuka alipopata mwaliko kutoka kwa
Str8up Vibes na kumchague yeye kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hilo, na
kwa mara ya kwanza kuja hapa nchini kama msanii.
“Nimefuarahi
sana kualikwa kwenye tukio la Monte Carlo Classic hapa jijini Dar es
Salaam, ninashukuru kwa nafasi hii na ninapenda kuwashukuru waandaji kwa
kutambua umuhimu wangu.”
Msanii
huyo aliongeza kwamba, amekuja nchini kufurahia na kujumuika na watu
hadhi tofauti, wasanii wa muziki pamoja na mashabiki zake na kuwaomba
wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kufika kwa wingi siku ya Jumamosi kwenye
tukio hili.
Maoni
Chapisha Maoni