Huawei yapanua mlolongo wa Y-Series kwa simu za 4G nchini
Kampuni ya Huawei Tanzania wametangaza
hivi punde kutanua mlolongo wake wa Y-Series kwa kuongeza simu mbili mpya za Huawei
Y3II na Y5II. Simu hizo mbili za Y-Series zimekuja katika aina mbili nayo ni ya
3G na 4G zikiwalenga wateja wa soko la chini na kati. Simu hizi zimekua
zikipatikana kwa watumiaji Tanzania tangu mapema mwezi Julai.
Huawei Y3II |
Simu za 4G zina kasi ya hali
ya juu ya intaneti kwa ajili ya kuperuzi, kutuma, kupokea na kupakua ujumbe,
ikiongeza matumizi ya intaneti yasiyo na matatizo. Huawei Tanzania inayoongoza
katika usambazaji wa simu za mkononi nchini Tanzania imewakumbuka kwa mara
nyingine watu wa hali ya chini kwa
kuwaletea simu hizi zenye uwezo mkubwa wa internet.
“Upanuzi wa simu zetu za bei
nafuu na zenye uwezo wa 4G nchini kote imeenda sambamba na msimamo wetu
kuwapatia wateja wetu huduma zilizo bora na za kimataifa ambazo zitaruhusu watanzania
wote kufurahia kasi ya 4G bila kujali kipato chao”, alisema Bi Jane Wang, Meneja masoko wa Huawei
Tanzania.
“Huawei Y3II na Y5II zenye
uwezo wa 4G zimekuja wakati muafaka na sahihi kwa sababu sasa naweza furahia
kupakua nyaraka mbalimbali zinazonisaidia katika masomo yangu bila usumbufu”
alisema Evangelister Isdory mwanafunzi mwaka wa pili katika moja ya vyuo
vikubwa nchini Tanzania.
“Simu hii ya Huawei Y5II yenye
uwezo wa 4G imerahisisha sana mawasiliano na wanafunzi wenzangu hapa chuo maana
sasa tunaweza kuhamisha na kupakua nyaraka zenye ukubwa wowote kwa wanafunzi
wenzangu au walimu bila usumbufu”, aliongezea.
Huawei Y3II na Huawei Y5II Zina
prosesa iliyoboreshwa zaidi. Simu hizi zina RAM ya GB 1 na pia simu zote mbili
zina kadi yenye ukubwa wa GB 8 ambayo inaweza kuongezeka hadi GB 32.
Y5II |
Kamera ya megapixel 8 ya Y5II
na megapixel 5 yaY3II za simu hizo zina uwezo mkubwa wa mwanga, kupiga picha
katika mwanga mdogo, kutoa eneo uliopiga.
Simu zote zinakuja na kifaa
kiitwacho Easy Key ambayo husaidia mtu kufika anapotaka kwenye simu hiyo kwa urahisi zaidi. Y3II ina taa ya “upinde wa
mvua” maarufu kama ‘Rainbow Light’ ambayo huwaka mtu anapopigiwa simu, kupokea
ujumbe au kuarifiwa. Y5II ina kamera ya mbele yenye flash ambayo husaidia
kupiga picha nzuri zaidi.
Y5II |
Akizungumzia ubora wa kamera
za simu hizo, Bibi Jane Wang, Meneja
Masoko wa Huawei Tanzania alisema “Ni jambo la kusikitisha kupoteza vitu
vya kipekee katika picha kwa sababu ya mwanga hafifu. Flash iliyopo katika simu
ya Huawei Y5II na Y3II inafanya kazi kwa ubora katika mwanga mdogo. Simu hizi
pia zina Easy Key ambayo hutoa urahisi wa kufanya kazi na kutumia simu hizo kwa
kugusa tu”.
Pamoja na simu hizo mbili za
Y-Series , Huawei Tanzania hivi karibuni wameleta simu nyingine katika soko la
Tanzania ijulikanayo kama Huawei GR5mini. Simu yenye muundo mzuri wa aluminium
yenye ubora mkubwa sana.
Huawei GR5mini ina uwezo wa
LTE ili watumiaji wa GR5mini wapakue na kuangalia muvi bila wasiwasi wa nafasi
maana ina GB 16.
Akiongelea jinsi GR5mini
ilivyo kasi, salama na yenye ubora zaidi, Bi
Wang, alisema “GR5mini ina kifaa cha kutambua alama ya vidole iliyoboreshwa
mara 100 zaidi ya simu zile za mwanzo, ina RAM ya GB 2 ili kuwawezesha
watumiaji kufurahia kutuma ujumbe muda wowote na betri yenye 3000mAh.” Katika
nyakati hizi za simu za kisasa tunahitaji simu yenye bei nafuu, ubora na inayo
dumu muda mrefu na kupatikana bila wasiwasi wa chaji kuisha katika mizunguko ya
kila siku. Aliongeza Bibi Jane.
Kabla ya mwaka kuisha, Huawei
imepanga kuwekeza katika upanuzi na kuboresha ubora wa vifaa pia kuongeza idadi
ya maduka nchini kote. Kuingia kwa simu zilizo za bei nafuu za 4G
kunadhihirisha uongozi wa Huawei katika ubunifu nchini Tanzania. Kwa sifa
zilizopo katika simu zake zote, hakika Huawei inatoa ushindani mkubwa katika
soko.
Maoni
Chapisha Maoni