Wafanyakazi wa Yahoo hawajui hatima yao?

Siku chache baada ya mtandao wa Yahoo kununuliwa na kampuni ya Verizon taarifa kutoka ndani ya wafanyakazi wa mtandao huo zinasema kuwa kwasasa hawajui hatiama yao chini ya uongozi huo mpya.

Hata hivyo mtandao wa Cnn Money umeripoti kuwa mauzo ya hisa za mtandao huo ambazo zilidaiwa kuporomoka kwa kipindi kirefu kwasasa zimepanda na kurejea kwenye hali yake ya kawaida mara tu baada ya kununuliwa na kampuni ya Verizon.yahoo verizon logo

Yahoo wenyewe kupitia mtandao wao wamedai kuwa, kwasasa wafanyakazi wana morali ya juu ya utendaji kazi nakwamba wanajitahidi kuwapa motisha ili kuhakikisha kuwa mwaka huu wanafikia malengo.

"Tuna imani kubwa ya kufanya vyema mwaka huu kwani mtandao wetu unaendelea kufanya vyema kwenye eneo la habari, michezo na uchumi kutoka mwezi hadi mwezi, hivyo tunatambua fika kuwa Yahooo chini ya Verizon utakuwa zaidi katika nyanja ya upashaji habari duniani," amenukuliwa mmoja wa maofisa habari wa Yahoo.

Wadadisi wa mamabo wanasema kuwa hata baadhi ya wabunifu wa mtandao huo wa Yahoo kwasasa wanamorari ya juu ya utendaji kazi ikilinganishwa na miezi kadhaa iliyopita kabla ya mtandao huo kununuliwa na kampuni ya Verizon.

Na kuongeza kuwa kwasasa wanamatumaini makubwa na kwamba wanafurahia kufanya kazi na mtandao huo ikilibnganishwa na awali.

Mmoja wa watendaji wa Yahoo kwenye kitengo cha habari, Rebecca Neufeld, amesema wanautazamia mwaka 2016 kama mwaka wao wa kurejesha heshima ya mtandao huo kwa kufanya kazi bora zaidi ili kuwanufasha wateja wao na watangazaji wao.-Chanzo Cnn Money

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4