Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2016

Udhaifu mkubwa wagunduliwa kwenye simu za iPhone

Picha
Mfumo wa Apple wa utendaji wa iOS umegundulika ambao utawezesha kupachikwa kwenye kifaa cha uchunguzi kukiwezesha kubofya kwenye kiunganishi. Uvumbuzi huo ulifanyika baada ya wakili anayetetea haki za kibinadamu kutoa taarifa kwa watafiti wa masuala ya usalama kuhusu jumbe alizozipata bila kutarajia. Waligundua taarifa nyingine tatu za awali zisizofahamika zilizovuja kutoka kwa mfumo wa Apple . tangu wakati huo Apple imetoa taarifa ya kuelezea tatizo hilo na namna linavyoshughulikiwa na kampuni hiyo. Makampuni mawili ya usalama yaliyohusika , Citizen Lab na Lookout, yamesema yamehifadhi taarifa hizo za uvumbuzi hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi. Kampuni ya Citizen Lab inasema , simu yake ya iPhone 6 ingekuwa ''imefunguliwa'' , ikimaanisha mfumo mwingine ambao haukuidhinishwa ungelikuwa umewekwa kwenye simu yake. "Na kama simu yake ingeathiriwa , ingekuwa kifaa cha upelelezi cha digitali ndani ya mfuko wake wa nguo, yenye uwe

Maji ya dunia yanahama?

Picha
Wanasayansi wametumia picha za za setilaiti kuchunguza namna maji ya dunia yalivyohama kwa zaidi ya miaka 30. Walibaini kwamba kilo mita za mraba 115,000 za ardhini kwa sasa zimefunikwa na maji na kilomita 173,000 za maji zimefunikwa sasa na ardhi. Ongezeko kubwa la maji limetokea katika eneo tambarare la betan , huku bahari ya Aral eneo kubwa la maji sasa limegeuka kuwa ardhi. wanasayansi hao wanasema kuwa maeneo ya mwambao pia yamekuwa na mabadiliko makubwa . Utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti ya Deltares ya nchini Uholanzi umechapishwa na jarida la mabadiliko ya asili ya hali ya hewa. Watafiti walitathmini picha za setilaiti azilizochukuliwa na kituo cha wataalam wa masuala ya anga cha Nasa ,ambacho kimekuwa kikichunguza dunia kwa miongo kadhaa . Waliweza kufuatilia mabadiliko ya sehemu ya juu ya dunia inayoweza kuonekana kwenye kipimo maalum . Waliweza kubaini eneo pana ambalo wakati mmoja liliwahi kuwa ardhi ambalo sasa limekuwa na maji

Huawei yapanua mlolongo wa Y-Series kwa simu za 4G nchini

Picha
Kampuni ya Huawei Tanzania wametangaza hivi punde kutanua mlolongo wake wa Y-Series kwa kuongeza simu mbili mpya za Huawei Y3II na Y5II. Simu hizo mbili za Y-Series zimekuja katika aina mbili nayo ni ya 3G na 4G zikiwalenga wateja wa soko la chini na kati. Simu hizi zimekua zikipatikana kwa watumiaji Tanzania tangu mapema mwezi Julai. Huawei Y3II Simu za 4G zina kasi ya hali ya juu ya intaneti kwa ajili ya kuperuzi, kutuma, kupokea na kupakua ujumbe, ikiongeza matumizi ya intaneti yasiyo na matatizo. Huawei Tanzania inayoongoza katika usambazaji wa simu za mkononi nchini Tanzania imewakumbuka kwa mara nyingine watu wa hali ya   chini kwa kuwaletea simu hizi zenye uwezo mkubwa wa internet. “Upanuzi wa simu zetu za bei nafuu na zenye uwezo wa 4G nchini kote imeenda sambamba na msimamo wetu kuwapatia wateja wetu huduma zilizo bora na za kimataifa ambazo zitaruhusu watanzania wote kufurahia kasi ya 4G bila kujali kipato chao”, alisema Bi Jane Wang, Meneja masoko wa Huawei Tanz

WhatsApp ku-share namba yako na Facebook

Picha
Kama unatumia WhatsApp kwaajili ya kutuma meseji kwa ndugu, jamaa na marafiki, kaa tayari kwa facebook kukufundisha mengi zaidi yatakayo kuhusu wewe ikiwamo kukutengeneza fedha. Mtandao wa WhatsApp umetangaza kuwa utaanza kushirikisha namba za simu na taarifa juu ya shughuli za watumiaji wake zaidi ya bilioni moja kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook ambao ni mtandao mama wa WhatsApp kwa zaidi ya miaka miwili sasa. WhatsApp wamesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kusaidia kufanya maboresho ya taarifa za wateja wao ikiwamo pia kuwasaidia watumiaji wa Facebook kubadilishana taarifa.   "Facebook na makampuni mengine ambayo yako chini ya familia ya Facebook yanaweza kutumia taarifa zako kutoka kwetu ili k uboresha uzoefu wako ndani ya huduma zao kama vile kufanya mapendekezo bidhaa na huduma mbalimbali, marafiki au uhusiano na mambo mengine yanayovutia, japo huduma hizo zitakuwa zitafanyika kwa sera zilezile za kulinda faragha za watumiaji. Hata hivyo hatua hiy

Wafanyakazi wa Yahoo hawajui hatima yao?

Picha
Siku chache baada ya mtandao wa Yahoo kununuliwa na kampuni ya Verizon taarifa kutoka ndani ya wafanyakazi wa mtandao huo zinasema kuwa kwasasa hawajui hatiama yao chini ya uongozi huo mpya. Hata hivyo mtandao wa Cnn Money umeripoti kuwa mauzo ya hisa za mtandao huo ambazo zilidaiwa kuporomoka kwa kipindi kirefu kwasasa zimepanda na kurejea kwenye hali yake ya kawaida mara tu baada ya kununuliwa na kampuni ya Verizon. Yahoo wenyewe kupitia mtandao wao wamedai kuwa, kwasasa wafanyakazi wana morali ya juu ya utendaji kazi nakwamba wanajitahidi kuwapa motisha ili kuhakikisha kuwa mwaka huu wanafikia malengo. "Tuna imani kubwa ya kufanya vyema mwaka huu kwani mtandao wetu unaendelea kufanya vyema kwenye eneo la habari, michezo na uchumi kutoka mwezi hadi mwezi, hivyo tunatambua fika kuwa Yahooo chini ya Verizon utakuwa zaidi katika nyanja ya upashaji habari duniani," amenukuliwa mmoja wa maofisa habari wa Yahoo. Wadadisi wa mamabo wanasema kuwa hata baadhi ya wabunifu w

Staa wa Nigeria Kiss Daniel kupamba tamasha la ‘MONTE CARLO CLASSIC’ Dar leo

Picha
Mwanamuziki maarufu wa Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel anayefahamika kwa jina la kisanii Kiss Daniel aliyetamba hasa kwa kibao chake cha ‘Woju’ kwenye anga za muziki,  ametua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa Tamasha la Monte Carlo Classic lililoandaliwa na Str8up Vibes wakishirikiana na DeJurist Global kwa udhamini wa Benki ya Barclays Tanzania. Kiss Daniel Mwimbaji huyo wa Nigeria aliyejizolea mashabiki wengi tangu alipoachia kibao chake cha ‘Woju’, ataongoza uzinduzi wa Tamasha hilo Jumamosi hii jijini Dar es Salaam katika Mgahawa wa Akemi uliopo kwenye jengo la Jubilee Towers, Mtaa wa Ohio. Mkurugenzi Mtendaji wa Str8up Vibes, Sniper Mantana alithibitisha mbele ya waandishi kwamba maandalizi ya Tamasha hilo yamekamilika na kuwasihi Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kujumuika na msanii huyo maarufu. Ameongeza kwamba kabla ya Tamasha hilo tiketi zitauzwa kwa shilingi 25,000 na itakapo timu usiku tiketi zitauzwa kwa shilingi 35,000. T

Mitandao ya kijamii yamnyima usingizi Tiwa Savage

Picha
Staa wa muziki nchini Nigeria, Tiwa Savage, amedai kuwa anajuta kuweka wazi mambo yake ya ndoa katika mitandao ya kijamii. Msanii huyo kwa sasa kazi zake zinasimamiwa na kampuni ya Rock Nation, inayomilikiwa na mkali wa rap nchini Marekani, Jay Z. Tiwa amedai kuwa kwa siku za hivi karibuni amekuwa akiyaweka mambo yake ya ndoa katika mitandao, hasa baada ya kuhojiwa mara kwa mara, lakini kitendo hicho kimewafanya watu wamzungumzie vibaya. “Katika kitu ambacho naweza kusema kuwa nimekosea katika maisha yangu ni kuweka wazi mambo yangu ya ndoa, najuta kwa kuwa kuna watu ambao wananiongelea vibaya kutokana na taarifa ambazo niliziongea, kuanzia sasa siwezi kufanya hivyo tena kwa mambo yangu binafsi,” amesema Tiwa.

Henry apata shavu Ubelgiji

Picha
Kocha mpya wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Roberto Martinez, amemtaja mchezaji wa zamani wa timu ya Arsenal, Thierry Henry, kuwa msaidizi wake katika benchi la ufundi la timu hiyo. Henry anaweza kuchukua majukumu hayo ya ukocha baada ya kujifunza akiwa katika timu ya vijana ya Arsenal. Thierry Henry Mkongwe huyo aliifundisha timu ya vijana ya chini ya umri wa miaka 18 ya Arsenal kabla ya kulazimika kuondoka baada ya Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, kuamuru kufanya hivyo kutokana na kitendo chake cha kuendelea na uchumbuzi katika televisheni ya Sky Sport. Hata hivyo, Henry ataruhusiwa kuendelea na kazi yake ya uchambuzi wakati wa mapumziko, licha ya kuteuliwa kuifundisha timu hiyo. Mkongwe huyo ataungana na Martinez na kocha msaidizi, Graeme Jones, katika benchi la ufundi la timu hiyo. Katika kutekeleza majukumu yake, Henry anatarajia kuwafundisha wachezaji kama Eden Hazard, Morouane Fellaini na Kevin De Bruyne.

Kichuya azungumzia kukaa benchi Simba

Picha
WINGA wa timu ya Simba, Shiza Kichuya, ameanza kusaka rekodi ya mshambuliaji wa kikosi hicho, Ibrahim Ajib, baada ya bao lake kuingia katika rekodi. Kichya akiwa amebebwa na Mavugo Kichuya aliyejiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, alifunga bao hilo akimalizia kona ya Mohamed Hussein kwa shuti kali katika mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Ndanda FC wiki iliyopita katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Wekundu hao wa Msimbazi kushinda mabao 3-1. Mmoja wa watu waliopo ndani ya Bodi ya Ligi, inayosimamia ligi hiyo ameliambia MTANZANIA Jumamosi kuwa bao hilo tayari limewekwa kwenye orodha ya mabao bora ya msimu wa 2016/17. Alisema kama ilivyo kawaida, baada ya mechi kumalizika kunakuwa na taarifa zinazopelekwa bodi ya ligi pamoja na kuangaliwa kwa video ili kujiridhisha kama mechi ilichezeshwa kwa haki na hapo ndipo ilipoonekana bao la Kichuya linastahili kuwa miongoni mwa mabao bora ya msimu. “Mara baada ya Kichuya kufunga bao hilo, viongozi wa bodi ya l

Mabasi yaliyofungiwa kurudi barabarani

Picha
Mabasi yanayosafirisha abiria wanaokwenda mikoani yaliyofungiwa na Serikali kwa kusababisha ajali yameanza kuruhusiwa kutoa huduma hiyo. Mabasi hayo yameruhusiwa baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu na Majini (SUMATRA) na Wamiliki wa Mabasi ya Abiria (TABOA) kufikia muafaka. Makubaliano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita yalilenga kuleta suluhu kwa kuwataka TABOA kusimamisha mgomo wa mabasi uliopangwa kufanyika nchi nzima Agosti 22 mwaka huu. Zaidi ya mabasi 60 ya kampuni tofauti yalifungiwa na Serikali baada ya kile kilichodaiwa na serikali kwamba yalisababisha ajali kwa uzembe wao. Wamiliki wa mabasi hayo walikuwa wanahoji sababu ya SUMATRA kufungiwa leseni ya usafirishaji  kwa kampuni badala ya kupewa adhabu basi moja lililopata ajali badala ya kufungiwa kampuni nzima. Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu Mkuu wa TABOA, Enea Mrutu alisema wamekubaliana mabasi ambayo ni mazima yaliyofungiwa yaachiwe kutegemeana na utaratibu wa ukaguzi y