Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2015

Dk Magufuli: Hakuna atakayeonewa

Picha
Dk John Magufuli Mgombea mteule wa urais kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, Dk John Magufuli ametambulishwa rasmi leo katika viwanja vya Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika viwanja hivyo, Magufuli alisema iwapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha haki inatendeka kwa Watanzania wote. “Nataka niseme kwa dhati sitawaangusha, nitafanya kazi kweli kweli, sitamuogopa mtu na wala sitapenda mtu wa chini aonewe,” alisema Dk Magufuli. Aliongeza kuwa atahakikisha anasimamia Ilani ya CCM na kuitekeleza. Magufuli aliwashukuru Watanzania kwa sala zao kwani katika mchakato mzima alikuwa akiwasihi wamuombee. “Kupitishwa kwangu inadhihirisha wazi mlikuwa mnaniombea na sala zenu zimesikilizwa na mwenyezi Mungu #UkaribishoWaMagufuli,” alisema.

Kutana na iPhone 6 ya Apple

Picha
KAMPUNI nyingi zinashindana kila siku ili kuhakikisha kuwa zinatengeneza na kuingiza bidhaa bora sokoni na zenye ushindani kulingana na ulimwengu huu wa kisasa. Kampni ya Elite Computer wauzaji wa bidhaa za Apple kama iPad, iPhone, iPod, MacBook Pro, MacBook Air, Mac mini, iMac na Mac Pro tangu 1990 nao haijabaki nyuma. Huku bidhaa zote zikiwa na dhamana kuanzia mwaka, pia zimehakikiwa na wahandisi na wataalamu wa Apple kwa lengo la ubora wa bidhaa zenyewe, Elite wamekuwa wakisifika kwa kuuza bidhaa bora ambapo awamu hii wameleta iPhone 6. iPhone 6 Hii ni moja ya bidhaa ambayo inasambazwa na  Elite ambayo siyo tu kubwa bali ni bora kwa kila namna kwanza  ina kasi ya ajabu unapoitumia, nguvu zaidi na ufanisi wa hali ya juu. Huku ikiwa na skrini yenye kioo laini kutachi na retina ya HD ambayo hii huonyesha kila kitu kwenye kioo chako.

Sterling:Mchezaji mwenye thamini zaidi Ulaya

Picha
Nyota wa Liverpool Raheem Sterling ndiye mchezaji chipukizi anayethaminiwa zaidi barani Ulaya kwa mujibu wa utafiti. Raia huyo wa Uingereza ambaye harakati za kuhamia Manchester City, zilitumbukia nyong'o amekadiriwa kuwa mwenye thamani ya pauni milioni 35 na kampuni ya utafiti ya Soccerex inayochapisha Orodha ya wachezaji wenye thamani ya juu ama 20 Football Value Index. Manchester City ilikuwa imeweka dau la pauni milioni £40 lakini ombi lao likakataliwa na Liverpool. Mlinzi wa Manchester United, Luke Shaw ameorodheshwa katika nafasi ya 9, John Stones wa Everton ameorodheshwa wa 16 huku kiungo wa Arsenal Calum Chambers akiorodheshwa katika nafasi ya 19. Kampuni hiyo ya Soccerex imefanya utafiti huo miongoni mwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 wanaocheza katika ligi za bara ulaya.

Mayweather apokonywa taji alilomshinda Pacquiao

Picha
Floyd Mayweather Bondia Bingwa wa dunia wa uzani wa Welter Floyd Mayweather amepokonywa ukanda alioutwaa baada ya kumchapa Mfilipino Manny Pacquiao mwezi Mei. Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 38 anadaiwa kushindwa kuilipa shirikisho la ndondi la WBO ada ya dola lakimi mbili $200,000 kabla ya makataa aliyopewa ya tarehe 3 Julai. Mayweather alitakiwa pia kutoa ukanda wa chipukizi wa WBO punde baada ya kumshinda mfilipino Pacquiao kwa wingi wa alama.

Lazima ruhusa ya kushika mimba Uchina

Picha
Kampuni moja ya Uchina inapanga kutoa masharti ambapo wafanyikazi wake watatakiwa kupata ruhusa kabla ya kuanza familia. Sheria hizo zimechapishwa na kuzua malalamiko mengi katika mitandao. Sheria kuu inaelezea kwamba wanawake wote walio kwenye ndoa lazima wawe wamehudumu kwa mwaka mmoja kwenye kampuni hiyo kabla ya kutuma kibali cha kukubaliwa kushika mimba.

Roboti yamuua mfanyikazi wa Volkswagen

Picha
Mfanyikazi mmoja katika kiwanda cha kutengeza magari aina ya Volkswagen nchini Ujerumani amefariki baada ya roboti kum'beba na kumuangusha katika chuma Marehemu mwenye umri wa miaka 22 alifariki hospitalini kufuatia ajali hiyo iliofanyika katika kiwanda kimoja kilichopo Baunatal yapata kilomita 100 kazkazini mwa Mji wa Frankfurt.

Lowassa: Nimechoka kuitwa fisadi

Picha
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana aliwataka wanaomhusisha na ufisadi kuacha mara moja kwa sababu hakuna hata chembe ya ukweli katika tuhuma hizo. Lowasa akizungukwa na waandishi dodoma Lowassa, aliyeonekana kuzungumza kwa hisia, alisema hayo jana mara baada ya kurejesha fomu ya kuwania kuteuliwa na CCM kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Mbunge huyo wa Monduli alikuwa mmoja kati ya makada tisa waliorudisha fomu jana, ikiwa ni siku moja kabla ya kuisha kwa muda uliowekwa na chama hicho. Wengine waliorejesha fomu jana ni Elidephonce Bilohe, Mwigulu Nchemba, Luhaga Mpina, Dk Hamisi Kigwangalla, Hassy Kitine, Mariki Marupu, Dk Asha Rose Migiro na Lazaro