Sterling:Mchezaji mwenye thamini zaidi Ulaya
Nyota wa Liverpool Raheem Sterling ndiye mchezaji chipukizi anayethaminiwa zaidi barani Ulaya kwa mujibu wa utafiti.
Raia huyo wa Uingereza ambaye harakati za kuhamia
Manchester City, zilitumbukia nyong'o amekadiriwa kuwa mwenye thamani ya
pauni milioni 35 na kampuni ya utafiti ya Soccerex inayochapisha Orodha
Manchester City ilikuwa imeweka dau la pauni milioni £40 lakini ombi lao likakataliwa na Liverpool.
Mlinzi
wa Manchester United, Luke Shaw ameorodheshwa katika nafasi ya 9, John
Stones wa Everton ameorodheshwa wa 16 huku kiungo wa Arsenal Calum
Chambers akiorodheshwa katika nafasi ya 19.
Kampuni hiyo ya
Soccerex imefanya utafiti huo miongoni mwa wachezaji wasiozidi umri wa
miaka 21 wanaocheza katika ligi za bara ulaya.
Inatumia vipengee
kama umri,nafasi wanayocheza uwanjani,Klabu,urefu wa Kandarasi,mechi
walizochezea timu zao za taifa,mechi walizocheza,mabao
waliofunga,majeraha na ubora wao kitalanta.
''tukiangalia kwa kina vipengee hivi vyote tunaweza kutathmini uwezo na thamani ya mchezaji.''
''Hivyo
vyote ndivyo vilitusaidia kubaini kuwa Sterling ndiye mchezaji bora na
mwenye thamani ya juu zaidi barani ulaya kwa sasa.'' alisema bwana
Esteve Calzada
Mlinzi wa Paris St-Germain ya Ufaransa ambaye ni raia wa Brazil
Marquinhos ameorodheshwa katika nafasi ya pili na thamani ya pauni
milioni £27.8.
Mchezaji mpya wa Manchester United vilevile ye
Uingereza Memphis Depay aliyegharimu kitita cha pauni milioni £31
ameorodheshwa katika nafasi ya tatu akiwa na thamani ya pauni milioni
£23.8.
Calzada anasema kuwa sheria iliyowekwa na shirikisho la
soka la Uingereza ambayo inazilazimisha vilabu vya Uingereza kuwa na
takriban wachezaji 8 raia wa Uingereza imeongeza maradufu thamani ya
wachezaji waingereza.
Wachezaji 4 katika orodha hiyo ni raia wa
Uingereza huku9 kati ya 20 bora wakitarajiwa kucheza katika ligi kuu ya
Uingereza msimu ujao.
Maoni
Chapisha Maoni