Mayweather apokonywa taji alilomshinda Pacquiao
Mmarekani huyo mwenye umri wa
miaka 38 anadaiwa kushindwa kuilipa shirikisho la ndondi la WBO ada ya
dola lakimi mbili $200,000 kabla ya makataa aliyopewa ya tarehe 3
Julai.
Mayweather alitakiwa pia kutoa ukanda wa chipukizi wa WBO punde baada ya kumshinda mfilipino Pacquiao kwa wingi wa alama.
Kufuatia kauli hiyo ya shirikisho la ndondi la WBO, Mayweather hatambuliwi tena kama mshikilizi wa taji hilo.
Taji hilo linashikiliwa na Mmarekani mwenza Timothy Bradley.
Yamkini
Mayweather alikuwa ameiahidi WBO kuwa akimshinda Pacquiao,angevua
mataji yote ya vijana ilikuwapa mabondia wapya fursa ya kuwania mataji
hayo lakini hadi kufikia sasa hajafanya hivyo.
Taarifa yao
iliyochapishwa katika mtandao wa wboboxing.comimesema kuwa ''hatukukuwa
na lingine baada ya Mayweather kushindwa kutekeleza matakwa yetu.kwa
hivyo hatutamtambua mayweather kama mshikilizi wa ukanda huo wa Welter''
Hata hivyo Mayweather, ambaye ndiye anayeshikilia mataji ya WBA na WBC ana hadi julai tarehe 20 kukata rufaa ya kauli hiyo.
Mayweather anatarajiwa kuandaa pigano lingine mjini Las Vegas tarehe 12 Septemba, japo haijabainika atazichapa dhidi ya nani.
Wakati hayo yakijiri WBO inapanga pigano la welter linalopangwa kufanyika tarehe 27 kati ya Bradley na Jessie Vargas.
Maoni
Chapisha Maoni