Kutana na iPhone 6 ya Apple
KAMPUNI nyingi zinashindana kila siku ili kuhakikisha kuwa zinatengeneza na kuingiza bidhaa bora sokoni na zenye ushindani kulingana na ulimwengu huu wa kisasa.
Kampni ya Elite Computer wauzaji wa bidhaa za Apple kama iPad, iPhone, iPod, MacBook Pro, MacBook Air, Mac mini, iMac na Mac Pro tangu 1990 nao haijabaki nyuma.
Huku bidhaa zote zikiwa na dhamana kuanzia mwaka, pia zimehakikiwa na wahandisi na wataalamu wa Apple kwa lengo la ubora wa bidhaa zenyewe, Elite wamekuwa wakisifika kwa kuuza bidhaa bora ambapo awamu hii wameleta iPhone 6.
iPhone 6
Hii ni moja ya bidhaa ambayo inasambazwa na Elite ambayo siyo tu kubwa bali ni bora kwa kila namna kwanza ina kasi ya ajabu unapoitumia, nguvu zaidi na ufanisi wa hali ya juu.
Huku ikiwa na skrini yenye kioo laini kutachi na retina ya HD ambayo hii huonyesha kila kitu kwenye kioo chako.
Ni moja ya mwendelezo wa kutengeneza vifaa na programu bora kabisa kwa kutumia malighafi za kisasa ambazo kwa pamoja zinafanya bidhaa hizi kuwa murua na zinaendana na kizazi cha sasa cha iPhone zilizo bora kwa saizi zote.
Kwenye simu hii usalama ni wa hali ya juu kwani kwa kutumia teknolojia mpya ya tachi ID inakuwezesha kuwa salama katika kupata iPhone yako na paswedi kamili kwa kutumia finga print yako tu.
Pia uzuri wa simu hii unaweza kutumia katika kufanya manunuzi kutoka iTunes na kuhifadhi kwenye Apps yako bila kutumia paswedi.
Kamera, kama unapenda picha simu hii ni suluhisho kwani kamera yake imeongezwa ubora na sasa unaweza kuitumia katika kuchukulia video.
Ni dhahili kuwa kila mtu kwasasa anapenda kupiga picha kwa kutumia iPhone kuliko nyingine hii yote ikisababishwa na simu hii kuwa na kamera ya kisasa aina ya iSight inayofanya picha kuonekana murua na nzuri kuliko kawaida.
Kwasasa imeongezwa na kuwa kubwa zaidi ambapo imekuwa na ukubwa wa 1.5 micron na saizi yake kuwa f/2.2 ya apecture teknolojia ambayo ni maarufu Duniani kutokana na kumsaidia kila mmoja kuweza kuchukua picha kubwa bora na kwa urahis zaidi.
Upande wa Wireless simu hii inaunganisha haraka zaidi kuliko simu nyingine yeyote hivyo kufanya uitembelee dunia nzima kwa haraka kwani iPhone 6 ina kasi ya LTE na hivyo kuifanya kuwa na nguvu zaidi ya Wireless unapokuwa unaunganisha jambo ambalo ni tofauti na zingine.
Pia unaweza kuitumia kama pochi yako kwani iPhone yako inaweza kukusaidia kulipa kwa njia rahisi, salama, na binafsi.
iPad Air 2
Ukiacha iPhone 6 Elite pia wana iPad za kisasa aina ya iPad Air2 ambazo ziko kwenye ukubwa wa 6.1 mm, na wembamba ukiongezwa na kuifanya kuwa bapa zaidi jambo ambalo limeiongezea uwezo na kasi zaidi.
Ina inchi 9.7 na kioo chenye retina kilicholeta mageuzi kwenye bidhaa zenye skirini za kutachi, huku ikiwa na nguvu ya A8X chip na usanifu wa kiwango cha 64 bit.
Kuhusu kamera ni yakisasa inayoboresha picha zaidi pindi tu unapojifotoa kwa kutumia mfumo wa HD, huku ikiwa na kasi zaidi kwenye upande wa Wireless, iOS 8, iCLoud huku ikikaa na chaji kwamuda wa zaidi ya masaa 10.
iPad hii pia inakuja na programu kubwa maalumu kwaajili ya uzalishaji na ubunifu huku kukiwa na programu nyingine zaidi ambazo zinapatikana kwenye App Store.
Macbook Pro
Ikiwa na kioo chenye kuonyesha moja kwa moja, inanguvu ya dual na Quad ambao hawa ndiyo watayalishaji wakuu, hii ina uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu pamoja na mwanga wa hali ya juu hali inayokufanya ufurahie kuendelea kuitumia.
Pia utendaji kazi wake ni wa kiwango cha juu kwani imetengenezwa kwa programu za kisasa na zenye ubora wa hali ya juu na apps.
Kama ilivyo kwa iPad Air 2 hata hii pia imeleta mapinduzi makubwa kwenye bidhaa za kutachi, ikiwa na betri inayokaa kwa muda mrefu lakini vyovyote utakavyoweza kutumia ila MacBook Pro inakupa nafasi ya kufanya na kubaini vitu vingi.
Maoni
Chapisha Maoni