Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2015

KABLA YA MZUNGU KUANZA KAZI, MATOLA KUANZA NA SIMBA GYM

Picha
Kikosi cha Simba, jana Jumanne kilianza mazoezi yake ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni siku moja tu tangu wamtangaze kocha wao mpya, Muingereza, Dylan Kerr anayetarajiwa kuwasili nchini wikiendi hii. Simba ambayo msimu uliopita wa ligi ilimaliza nafasi ya tatu, imeanza mazoezi ya gym chini ya kocha wao msaidizi, Seleman Matola, huku ikiwa na wachezaji wachache kutokana na wengine kuwa mbali na Dar ambapo mazoezi hayo yatadumu mpaka hapo atakapowasili kocha mkuu. Matola amesema kuwa jana Jumanne kikosi hicho kilianza mazoezi yake ya kujiwinda kwa msimu wa ligi kuu rasmi kwa kuanzia gym ambapo watadumu katika mazoezi hayo mpaka watakapoingia kambini rasmi.

KIBADENI APEWA KAZI YA KUWAPA SOMO WACHEZAJI STARS

Picha
Benchi jipya la Taifa Stars likiongozwa na mshauri wake wa ufundi, Abdallah Kibadeni litakutana na wachezaji wa kikosi cha Taifa Stars, keshokutwa. Kibadeni ni mmoja wa magwiji wa soka nchini, aliwahi kuwika akiwa na Majimaji, Simba na Taifa Stars. Mkutano huo kati ya Kibadeni, Kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa , msaidizi wake Ahmed Morocco watakutana na wachezaji hao katika hoteli ya Tansoma kwa ajili ya kujadili suala la uzalendo. Mkwasa amesema watafanya hivyo kwa ajili ya kuzungumza na wachezaji lakini pia kuwapa wachezaji somo la uzalendo. Tayari Mkwasa ametangaza kikosi chake hukuManyika Peter, kipa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars akiwapewa kazi ya kuwanoamakipa.

MKWASA ATANGAZA KIKOSI STARS, AWATEMA DIDA, OSCAR JOSHUA

Picha
Kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa aliyechukua nafasi ya Mart Nooij ametangaza kikosi chake kipya kwa ajili ya kuivaa Uganda huku akimtema kipa Deogratius Munish ‘Dida’ na nafasi yake amemchagua Ally Mustapha ‘Barthez’. Wengine ambao Mkwasa amewatema ni Erasto Nyoni, Amri Kiemba na Kelvin Friday kutoka Azam FC pia Oscar Joshua kutoka Yanga, Pia Ibrahim Ajibu kutoka Simba. Waliorejea ni Kelvin Yondani pia Deus Kaseke huku akimchukua Michael Idan wa Ruvu Shooting. Pia Samuel Kamuntu wa JKT, Juma Abdul wa Yanga na Mudathir Yahya kutoka Azam wamejumuishwa kwamba wanaweza kuitwa wakati wowote.

MCHA HAMIS KUKOSA MICHUANO YA KAGAME

Picha
Mshambuliaji wa Azam FC, Mcha Hamis amewekwa bandeji ngumu P.O.P kwenye mguu wake wa kushoto baada ya kupata majeruhi kwenye goti lake la mguu wa kushoto, hivyo amepewa mwezi mmoja kuwa nje ya Uwanja na atakosa mashindano ya Kombe la Kagame .  Kwa mujibu wa daktari wa Azam, Mbaruku Mlinga alisema, ili Mcha apone kabisa na kurudi uwanjani, atakaa kwa kipindi cha mwezi mmoja.  "Alivunjika kidogo kwenye goti ndiyo maana tukamwekea P.O.P ili awe sawa. Atakaa na bandeji hiyo kwa muda wa wiki mbili na tangu alipowekwa hadi leo, ameshamaliza wiki moja hivyo Alhamisi ijayo atatolewa,"alisema Mbarouk.

SIMBA YAMTANGAZA KOCHA MPYA KUTOKA UINGEREZA

Picha
Klabu ya Simba imeingia mkataba na Dylan Kerr kama kocha mpya na anatarajiwa kuanza kazi rasmi mwanzoni mwa mwezi July. Kocha huyo kutoka Nchini Uingereza ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika fani ya mpira wa miguu huku pia akiwa na umahiri wa kufundisha klabu mbalimbali duniani zikiwemo Hai Phong FC Vietnam, Hamilliton Academicals FC na Greennock Morton FC zote kutoka Scotland.

Wasanii 21 waanza kambi Pwani

Picha
WASANII  21 kati ya 50  juzi walianza kambi rasmi katika kijiji cha Wasanii Mwanzega, Mkuranga  mkoani Pwani. Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taaalib, amesema kundi la kwanza la wasanii limeweka kambi na jingine litafuata baada ya mwezi mmoja. Alisema wasanii hao ambao watakuwa na jukumu la kufanya mazoezi ya kuigiza filamu na tamthilia, pia watakuwa wanapata mafunzo ya kilimo cha bustani na michezo mbalimbali. “Wasanii hawa watakuwa wanapata masomo ya darasani

Mbaroni akituhumiwa kuua mwanawe

Picha
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Dainees Fredrick (30), mkazi wa Kambi ya Raha, wilayani Hai, kwa tuhuma za kumuua mtoto wake mchanga muda mfupi baada ya kumzaa kwa kumtumbukiza chooni. Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alifanya kitendo hicho siku moja baada ya kujifungua ambapo alimfunga mtoto huyo wa kiume kwenye kanga na kumweka kwenye mfuko wa plastiki kisha kumtumbukiza chooni. Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani, katika taarifa yake alisema tukio hilo lilitokea Juni 10, saa tatu usiku, Mtaa wa Kambi ya Raha, ambapo waliofanikisha kukamatwa kwake ni majirani anaoishi nao.

Daz Baba amkumbuka Mwangwea

Picha
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, David Jacob ‘Daz Baba’, amesema video yake mpya  itakayofahamika kama ‘Mzigo Viwanjani’ ni kumbukumbu tosha ya marehemu Albert Mangwea.  Daz baba alisema aliweza kumshirikisha Mangwea katika single ya wimbo huo.  “Tulifanya mambo mengi sana na Mangwea, hivyo video hii imekuwa kumbukumbu kwangu,” alisema Daz Baba. Alisema video hiyo inafanywa

Usaili BSS mikoa minne

Picha
Mkurugenzi wa Kampuni  ya Benchmark Production  inayoandaa shindano hilo,  Rita Paulsen MSIMU wa tisa wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba, maarufu kama ‘Bongo Star Search’ unatarajia kuanza rasmi mwezi ujao, ambapo kwa mwaka huu usaili utafanyika katika mikoa minne tu. Akizungumza  jijini jana, Mkurugenzi wa Kampuni  ya Benchmark Production inayoandaa shindano hilo,  Rita Paulsen, alisema mwaka huu watafanya usaili katika mikoa minne, baada ya kufanya uchunguzi na kugundua washiriki wanajirudia katika mikoa yote. “Mwaka huu usaili tutaufanya katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam, kila mtu mwenye kipaji atapaswa kufika kwenye mikoa tuliyoitaja na tumepanga kuchagua washiriki watano watano kutoka kila mkoa isipokuwa hapa jijini,” alisema Rita.

Muumini apora sanduku la sadaka la milioni 2/-

Picha
MUUMINI wa  Kanisa la Waadventista Wasabato la Balili wilayani Bunda, Mikael Lusenga,  anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuiba  sanduku la  sadaka za waumini   Sh milioni mbili. Lusenga alikamatwa juzi nyumbani kwao Balili  akiwa na sanduku hilo  baada ya kuwekewa mtego na waumini  na mchungaji wa kanisa hilo, Joshua  Mangai.