Muumini apora sanduku la sadaka la milioni 2/-
MUUMINI wa
Kanisa la Waadventista Wasabato la Balili wilayani
Bunda, Mikael Lusenga, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa
tuhuma za kuiba sanduku la sadaka za waumini Sh milioni mbili.

Lusenga
alikamatwa juzi nyumbani kwao Balili akiwa
na sanduku hilo baada ya kuwekewa mtego na waumini na mchungaji wa
kanisa hilo, Joshua Mangai.
Mtuhumiwa
huyo anadaiwa kufanya tukio hilo Juni 6 mwkaa huu baada ya kupewa ufunguo
wa mlango ofisi wa ya kanisa kwa ajili ya shughuli muhimu za kanisa ndani
ya ofisi hiyo.
Viongozi wa kanisa waligundua sanduku la fedha limeibwa Juni 8 walipoingia ofisini kuchukua fedha hizo zilizokusanywa Jumamosi iliyopita ili wazipeleke benki.
Viongozi hao walidai hawakutegemea muumini huyo kufanya kitendo hicho kwa vile alikuwa muumini mzuri na mwenye bidii katika shughuli za kanisa.
Pamoja na sefu hiyo zilikutwa pia redio na vifaa vya saluni zenye thamani ya Sh 700,000 zilizodaiwa kuwa mtuhumiwa alinunua Jumatatu kutokana na fedha hizo za sadaka.

Jeshi la polisi limesema bado
linaendelea na upelelezi na litamfikisha mahakamani muda wowote.-Mtanzania
Maoni
Chapisha Maoni