Mbaroni akituhumiwa kuua mwanawe
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Dainees Fredrick (30), mkazi
wa Kambi ya Raha, wilayani Hai, kwa tuhuma za kumuua mtoto wake mchanga muda mfupi baada ya kumzaa kwa kumtumbukiza chooni.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alifanya kitendo hicho siku moja baada ya kujifungua ambapo alimfunga mtoto huyo wa kiume kwenye kanga na kumweka
kwenye mfuko wa plastiki kisha kumtumbukiza chooni.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani, katika taarifa
yake alisema tukio hilo lilitokea Juni 10, saa tatu usiku, Mtaa wa Kambi ya Raha, ambapo waliofanikisha kukamatwa kwake ni
majirani anaoishi nao.
Alisema Rose Komely alisikia sauti ya kichanga
kikilia ndani ya choo baada ya kwenda kujisaidia, ndipo alipowaeleza
wapangaji wengine na kwenda chumbani kwa mtuhumiwa huyo na kumkuta akiwa amekaa
huku akiwa hana ujauzito analalamika maumivu ya tumbo.
Ngonyani alisema kuwa mtoa taarifa alimuacha mtuhumiwa akiwa na mwenzake kisha kutoa taarifa kwa balozi Editha John ambaye alitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.
Hata hivyo, licha ya Jeshi la Polisi kufanikiwa kufika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kumtoa mtoto katika choo alichokuwa ametupwa tayari mtoto alikuwa amekufa.
Mtuhumiwa wa tukio hilo la mauaji ya kichanga anashikiliwa na Polisi na kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Hai, huku akiwa chini ya ulinzi akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.-MTANZANIA

Maoni
Chapisha Maoni