MSANII wa muziki wa kizazi kipya, David Jacob ‘Daz Baba’,
amesema video yake mpya itakayofahamika
kama ‘Mzigo Viwanjani’ ni kumbukumbu tosha ya marehemu Albert Mangwea.
Daz baba alisema aliweza
kumshirikisha Mangwea katika single ya wimbo huo.
“Tulifanya mambo
mengi sana na Mangwea, hivyo video hii imekuwa kumbukumbu kwangu,” alisema Daz
Baba.
Alisema video hiyo inafanywa
chini ya mtayarishaji
Lamar, inatarajiwa kukamilika muda wowote kuanzia sasa, hivyo mashabiki
wajiandae kuona kitu gani amewaandalia.
Maoni
Chapisha Maoni