Wasanii 21 waanza kambi Pwani

WASANII  21 kati ya 50  juzi walianza kambi rasmi katika kijiji cha Wasanii Mwanzega, Mkuranga  mkoani Pwani.
http://img06.deviantart.net/877d/i/2009/138/c/3/music_is_my_life_by_lietingadiena.jpg
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taaalib, amesema kundi la kwanza la wasanii limeweka kambi na jingine litafuata baada ya mwezi mmoja.
Alisema wasanii hao ambao watakuwa na jukumu la kufanya mazoezi ya kuigiza filamu na tamthilia, pia watakuwa wanapata mafunzo ya kilimo cha bustani na michezo mbalimbali.
“Wasanii hawa watakuwa wanapata masomo ya darasani
ya kilimo kwanza na tayari tumeshawaandalia wataalamu kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo,” alisema Taaalib.
Mwenyekiti huyo alisema kundi la wasanii 30 litaondoka kijijini hapo mwishoni mwa mwezi ujao, baada ya kumaliza mafunzo ili kuwapa nafasi wengine kuhamia na kujifunza.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4