Machapisho

KOCHA STARS ASIKIA KILIO CHA WATANZANIA, AITA NYOTA WAPYA STARS

Picha
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajiwa kuingia kambini kesho jumatano katika hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri kuwania kufuzu kwa AFCON.                         Kocha Mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij, amewaita wachezaji 16 kuingia kambini kesho siku ya jumatano kwa ajili ya kupimwa

"TOROKA UJE" BAA YA WIKI SHINDANO LA FANYAKWELI KIWANJANI"

Picha
Meneja Vipoozeo na mwonekano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Baraka Mandara (Kushoto) akikabidhi zawadi ya Tisheti kwa Bw. Seth Noel(Katikati) kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa wapenzi wa bia ya Tusker waliojumuika

Kombe la FA England labadilishwa jina

Picha
Michuano mikongwe barani Ulaya ya kombe la FA sasa imefikisha miaka yake 144 tangu kuanzishwa kwake, Habari mpya kutoka ndani ya bodi ya kombe la hilo la FA ni kwamba kwa sasa

Kaseja, Mgosi watoa mapya kuhusu Simba

Picha
WAKATI kukiwa na tetesi za Simba kutaka kuwarudisha kundini wachezaji wake wa zamani Juma Kaseja na Mussa Hassan ‘Mgosi’ ili kuimarisha kikosi chao msimu ujao, wachezaji hao kila mmoja ametoa lake la moyoni.

TFF yatembeza adhabu kali Ligi Kuu

Picha
MWAMUZI wa mechi kati ya Azam FC na Kagera Sugar, Stephen Makuka na msaidizi wake namba mbili Said Mnonga wameondolewa kwenye orodha za waamuzi wa Ligi Kuu na kufungiwa kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kushindwa kumudu mchezo huo. Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein anapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kutoa lugha ya matusi kwa waamuzi na kutaka kumpiga mwamuzi msaidizi namba 2, Said Mnonga kwenye mechi namba 158 dhidi ya Azam FC iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 38(1) ya Ligi Kuu. Katika mechi hiyo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo hata hivyo Kagera walikuwa walilalamikia bao la pili lililofungwa na Gaudence Mwaikimba kuwa

Owino yuleee Yanga

Picha
George Owino WAKATI mashabiki wa Simba wakiendelea kuugulia maumivu ya kuondokewa na mfungaji wao bora wa msimu uliopita, Amis Tambwe huenda wakalia zaidi baada ya Yanga kuwa kwenye mikakati mizito ya kumsajili beki la nguvu la timu hiyo Mganda, Joseph Owino. Owino anamaliza mkataba wake ligi itakapomalizika Mei mwaka huu ambapo taarifa za uhakika kutoka kwa kigogo mmoja wa Kamati ya Usajili ya Yanga zinaeleza kocha Mkuu wa Klabu hiyo, Hans Van de Pluijm anataka saini ya Owino ili kuimarisha safu yake ulinzi. Tangu kuwasili kwa kocha wa sasa wa Simba, Goran Kopunovic, Owino amekuwa akisugulishwa benchi na kusubiri hadi aumie kati ya Jjuuko Murushid na Hassan Isihaka.Owino alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Simba mwanzoni mwa msimu huu timu hiyo ilipokuwa chini ya kocha Patrick Phiri kiasi cha kupewa unahodha. Ujio wa kocha mpya wa timu hiyo Goran

Tambwe aweka rekodi ya kutisha Ligi Kuu

Picha
STRAIKA wa Yanga, raia wa Burundi, Amissi Tambwe, ameweka bonge la rekodi ya kutisha kwa kuwa mchezaji wa kwanza kupiga hat-trick (mabao matatu mechi moja) ya pili msimu huu, ikiwa ni ya nne kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mrundi huyo ni mchezaji pekee aliyeweka rekodi hiyo ambayo haijawahi kuwekwa na mchezaji yeyote tangu uwanja huo ulipoanza kutumika. Mechi ya kwanza kwa straika huyo kufunga hat trick kwenye uwanja huo ilikuwa ni Februari Mosi, 2014, dhidi ya JKT Oljoro, akiwa na Simba, ambayo ilishinda 4-0. Mechi nyingine ambayo Mrundi huyo alifunga hat trick ilikuwa ni Septemba 19, 2014 dhidi ya